Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Sio nia yangu kupingana na serikali yangu, lakini acha ukweli uwe ukweli. NIlishasema humu JF kwamba, kama viongozi wetu wanataka tuamini kwamba hatuna tatizo la COVID-19 nchini na hata kuutangazia ulimwengu kwamba hapa kwetu Tanzania tuko salama kabisa, basi angalau kwa wiki mbili mfululizo tupime watu angalau 50 kwa siku pale Kariakoo sokoni, Manzese, Temeke na Kinondoni. Tukiona hawa watu 200 tutakaowapima kila siku, hata kama ni juu kidogo ya 50% hawana COVID-19 basi tuutangazie ulimwengu kwamba hatuna COVID-19.
Lakini serikali yetu haitaki kufanya hili. Swali ni kwa nini?
Japo hatutaki kufanya hivyo, watu wakijitokeza, kama ubalaozi wa Marekani, na kutangaza hadharani kwamba raia wake wanapokuja Tanzania wajihadhari na maambukizi ya COVID-19, au Kenya kusema wataweka vizuizi dhidi ya abiria kutoka Tanzania, tunaanza kuwapigia kelele - ooh mabeberu nyie, hamuitakii mema nchi yetu nk. Hivi tuna akili sawasawa sisi? Uwezo wetu wa kufikiri ndio unaishia hapo, kupiga kelele mabeberu?
Yapaswa iwe wazi sana kwetu kwamba ikiwa ni upumbavu kusema Tanzania kuna COVID-19 bila kuwa na takwimu za kuthibitisha hilo, basi iwe pia ni upumbavu kusema Tanzania hakuna COVID-19 bila kuwa takwimu za kuthibitisha hilo!