Ikiwa ni upumbavu kusema Tanzania kuna COVID-19 bila kuwa na takwimu, basi iwe pia ni upumbavu kusema Tanzania hakuna COVID-19 bila takwimu

Ikiwa ni upumbavu kusema Tanzania kuna COVID-19 bila kuwa na takwimu, basi iwe pia ni upumbavu kusema Tanzania hakuna COVID-19 bila takwimu

Kwa sababu si wote tunachagua kwa makusudi kuwa wapumbavu. Kama huna Corona, kwa nini unakataa kufanya testing chache kwa muda mfupi kuthibitisha huna Corona? Unaogopa nini?...
Nafikri wenye matatizo ni wale wanaosema ipo kisha unakuta wamekiuka masharti yote ya kujikinga na wamerundikana pamoja kama vitoto vya panya
 
Nafikri wapumbavu ni wale wanaosema ipo kisha unakuta wamekiuka masharti yote ya kujikinga na wamerundikana pamoja kama vitoto vya panya
Kwa hilo ninakuunga mkono bila upendeleo
 
Aisee takwimu inakuwaje kwenye kitu akuna.

Yaani sifugi kuku alafu nikupe takwimu za kuku.
Si swala la takwimu, covid-19 haionekani kama kuku wako. Tunajivua ufahamu kwa kushabikia ujinga. Ni maabara yenye uwezo kupima na kutoa matokeo ya kuwepo au kutokuwepo kwa ugonjwa.

Tanzania midomo ya wanasiasa ndio maabara. 'Nyambhisa bhisa ubhurweri ni kiriro kirimbhuura', methali ya Kanda ya ziwa. Kampeni punde zitaanza, mafuriko kwenye mikutano yatakuwepo(walau kupunguza sononi) kwa kuwa tumeaminishwa Mungu kajibu maombi yetu, corona free State.
 
Corona ugonjwa wa akili ukipuuza haupati..
Mheshimiwa Rais Magufuli kwa hili kapatia bongo ni business as usual...

Watu wangekua wanaumwa mamia kwa mamia hakuna mtu ambaye angrpeleka pua yake hayo maeneo uliyotaja bila tahadhari
 
Kapime wewe na Ukoo wako
Mnalazimisha vitu vya Ajabu kwanini
Mmeishiwa hoja
Acheni Kampeni mseme kuna Korona
 
Hivi kwani mnautamani huo ugonjwa? Bila kuusema hampumui? Kitu chenyewe kibaya lakini mnavyokipenda kukitaja taja chanini jamani? Si muache shetani apite aende zake?
Jamaa anataka tuanze kuchokonoana pua na koo!!
Yale madude bwana wanakuchokonoa hadi unajisikia kufakufa.
 
Jamaa anataka tuanze kuchokonoana pua na koo!!
Yale madude bwana wanakuchokonoa hadi unajisikia kufakufa.
Yaani huwa nikitizama vile unaomba Mungu akuepushie mbali, sasa watu wamekazana takwimu si wakapime wao?
 
Unaangaika na takwimu,kwani huko Kenya hiyo takwimu imewasaidia nini hata sasa,kama si kuwatia hofu tu..Hakuna korona Tanzania
 
Tumekuelewa.
Unajua tofauti ya typo na ujinga? Ushauri wangu ni ule ule jifunze kuandika! Ona ulivyo kilaza mpaka unadhani kuandika neno ''korona'' kwenye kiswahili ni kosa! Kiswahili sahihi ni korona na siyo corona!
 
Back
Top Bottom