Ikiwa Siku ya sensa hakutakuwa na mapumziko, basi sensa inaweza kuchukua zaidi ya wiki kukamilika

Ikiwa Siku ya sensa hakutakuwa na mapumziko, basi sensa inaweza kuchukua zaidi ya wiki kukamilika

Sensa ya watu na makazi ni siku 6 na sensa ya majengo siku 2.Kuanzia tarhe 23/8.Afsa akija atataka taarifa za waliolala usiku wa kuamkia tarehe 23. Kuhusu kutokuepo watakao kuwepo wataatoa taarifa alafu zitakazo bakia afsa anakuja kuzimalizia kwa muda huo utakao kuwepo,hata ikiwa saa 11 alfajiri ndoo muuda wako wakuwa nyumbani atakuja.Taarifa zote zitachukuliwa bila wasiwasi.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Hili zoezi haliko serious kabisa kuna watu wengine watakuwa wasafiri wengine watakuwa na majukumu yao kwa mfano wakaazi wa Mijini unakuta nyumba ina. Wapangaji sita wote wamepanga lakini mwenye nyumba hana taarifa zao muhimu na kuwapata ni kipengele.
 
Hivi ni watu huwa hatuna kumbukumbu au elimu haijatolewa ya kutosha?

Usiku wa sensa huwa mmoja,

Ila zoezi la kukusanya taarifa huwa ni karibu week nzima.

Unatakuwa kuweka kumbukumbu za wageni na watu watakolala kwako usiku wa kuamkia tarehe 23. Karani atakuja siku yoyote baada ya tarehe 23.


Lakini pia hawawezi kupata taarifa kamili huwa ni makisio, kwa sababu kuna watu wanakufa siku hiyo, na wanazalia pia. Kuna wasafiri na kuna watu wanakesha sehemu tofauti tofauti.
 
Kwa mujibu wa Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mama Anna Makinda ametoa tangazo kwamba siku ya sensa, tarehe 23/08/2022 ambayo itakuwa Jumanne, haitakuwa siku ya mapumziko. Haya ni maajabu.
View attachment 2322941

Kwa mujibu wa historia ya sensa za miongo miwili iliyopita, inaonesha ili kuwapata watu wote majumbani basi sensa zilifanyika siku za mapumziko yaani Jumamosi na Jumapili.
Mwaka 2002 sensa ilianza kufanyika usiku wa tarehe 24 kuamkia 25 Agosti ambayo ilikuwa ni Jumamosi kuamkia Jumapili. Mwaka 2012 sensa ilifanyika tarehe 26 Agosti ambayo ilikuwa Jumapili.
Cha kushangaza sensa ya mwaka huu 2022, tarehe iliyopangwa ni 23 Agosti ambayo itaangukia siku ya Jumanne, siku ambayo ni ya kazi, na wanasema hakutakuwa na mapumziko.

Hapa bila hata ya kutumia akili za rocket science hawatapata data zote kwa siku hiyo maana wengi watakuwa makazini, na hata wale watakaowakuta majumbani watakuwa na data nusunusu maana wengi watakuwa watoto na wafanyakazi wa majumbani ambao wanajua majina tuu, huenda hata wasijue nyumba wanayoishi ni ya wazazi wao ama ni ya kupanga.

Kwa jinsi nilivyosikia hii sensa inahitaji data nyingi mpaka viwanja na nyumba anazomiliki mtu, namba za NIDA, taarifa za walemavu, taarifa za vifo vya wazazi, taarifa za vifo vitokanavyo na uzazi, nk basi tutegemee hii sensa kuchukua zaidi ya wiki sababu ya kutopatikana kwa watu watakaotoa data zote kwa siku moja.
Si walishaambiwa waache taarifa zao siku ya kuamkia 23
 
NAONA BAADHI YA WATU KUGOMEA HILI ZOEZI NA HATA DATA HAWATAZIPATA ZA KUTOSHA

Mathalani nyumbani ninapokaa wote tunatoka asubuhi na kurudi night kali, hizo data watazipata wapi?
Bandiken raarifa zenu kwenye milango yenu siku za kuamkia 23 kabla hujatoka.
 
Kwangu Mimi hata ingekua mapumziko , nisingeacha kwenda mishe ,kujitafutia ugali wangu .
Naunga mkono hoja , taarifa zangu watazikuta nyumbani
Mimi najua hiyo siku kwa asilimia kubwa sitakuwa nyumbani na nitatoa maelekezo nisihesabiwe hata kama watakuwa na taarifa zangu.

Wakinikuta huko mtaani wataweza kunihesabu wakitaka, ikishindikana itakuwa imeisha hiyo.
 
Ngoja wawakute wahousegirl hata kusoma na kuandika hawajui ...Wahusika wako kazini
 
Mtaani kwangu kuna nyumba zaidi ya 10 ninazozifaham wanaishi jamaa na marafiki zangu hizi nyumba kwanza mwenye nyumba haishi hapo anaishi mkoani kodi anatumiwa na wapangaji wake wote ni watumishi na hawana familia kwahyo asubuh wote wanatoka mpaka usiku ndo wanakuja au weekend ndo wanakuepo sasa nyumba kama hizo unapataje data na wakitoka wanafunga gate kabisa kwasababu hakuna mtu anaye baki nyumbani
 
Mtaani kwangu kuna nyumba zaidi ya 10 ninazozifaham wanaishi jamaa na marafiki zangu hizi nyumba kwanza mwenye nyumba haishi hapo anaishi mkoani kodi anatumiwa na wapangaji wake wote ni watumishi na hawana familia kwahyo asubuh wote wanatoka mpaka usiku ndo wanakuja au weekend ndo wanakuepo sasa nyumba kama hizo unapataje data na wakitoka wanafunga gate kabisa kwasababu hakuna mtu anaye baki nyumbani
Hili zoezi kuna atakae achwa hata mmoja

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Ilitakiwa watu wakutwe nyumbani

Hata mkuu wa kaya akiwataja watoto zipo kumbukumbu nyingine ambazo ni lazima mhusika azitoe.

Ni kama wahesabu sensa wengine ni wazee tu , eti wale wasahili nao wanahesabu na wengine wastaafu kama Mamndenyi pia wapo.

Naona sensa kufanikiwa kwa asilimia siyo nyingi.
 
Kimeeleweka huku 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220818-122918.png
    Screenshot_20220818-122918.png
    152 KB · Views: 3
Back
Top Bottom