Ikiwa watalipwa vyeti feki, nimekusudia kuishitaki Serikali

Hahaa! Mkuu, ulichoandika embu rudia kusoma uone kama utakielewa!
 
Utashtaki na hao waliowaajiri? Maana kama wangekuwa makini na waadilifu wangegundua hivyo vyeti feki.
Likija jangiri livunje nyumba yako na kukuibia, tukushitaki na wewe kwa kutoweka vitasa vigumu zaidi? Hawa walifoji. Maana yake walifanya kitu kikaonekana kama ni cha kweli. Baada ya uchunguzi mkali ndipo kosa likadhihirika. Sasa aliyemuajiri huyu mfojaji ana kosa gani? Kama ikithibitishwa muajiri alifahamu kwamba hivyo vyeti ni vya kufoji, hapo kweli naye achukuliwe hatua.
 
Wakati unatumia cheti cha huyo wa kidato cha nne hadi kufika udaktari majina ulikua unatumia yapi??

Yako au ya mwenye cheti cha kidato cha nne??
cheti kina badirishwa jina?!!ninachopingana nacho ni kuniambia eti kwa kutumia cheti cha kidato cha nne,cha mtu nikajiendeleza hadi nikawa DR.bingwa bado nitaonekana kuwa cwezi kuwa dr.mzuri,au kuwa injinia mzuri?!
 
Mkuu wa kaya yeye anahangaika kutengeneza legacy yake kwa kupindua mambo ya mtangulizi wake, badala ya kutatuma matatizo aliyotengeneza na wateule wake ya umeme na maji. Ametulia huku huduma za jamii zikitolewa kwa ratiba.
Maji yanatokana na mvua,ofisi ya rais haizalishi/leti maji,tatizo la miundo mbinu ya umeme siyo la Leo na halitoisha kesho,suala la vyeti feki ni utata,huko nyuma watu hawakuwa makini na kubadili majina taasisi za elimu,Leo ukimkagua utasema kafoji vyeti,Sasa alifanya kazi,akakatwa pspf,ni pesa yake,haki apewe
 
kunge kuwa na Uchunguzi mkali ungewaacha je kina bashite?na watu kibao tu waliokuwa na ukaribu na wakubwa?!!mbona jeshini na polisi hawakugusa?na huko ndiko walipo wengi sana
 
Mkuu wa kaya yeye anahangaika kutengeneza legacy yake kwa kupindua mambo ya mtangulizi wake, badala ya kutatuma matatizo aliyotengeneza na wateule wake ya umeme na maji. Ametulia huku huduma za jamii zikitolewa kwa ratiba.
ungekuwa wewe ungemshauri atatue vipi tatizo la maji ambalo kimsingi chanzo chake ni ukame?
 
Sasa kwann hadi sasa hamshinikizi wakamatwe na kuchunguzwa.
 
Mfumo mbovu wa Elimu ndio umesababisha vyeti feki kwa sababu umekaa katika mfumo wa elimination. Watu wenye uwezo na akili wanaenguliwa na mfumo kisa tu madarasa yako machache unavyozidi kwenda juu kuazia la Saba, Form 4 hadi Form Six ni mwendo wa mchujo. wengine ndio hapo sasa wanatufuta majina ya waliokosa ada wanasongesha unakuta mtu for one kaenda na jina lingine au form six ukimtrace kunzia primaru kuna mahali anapotea na wengine hasa kwenye majeshi wametumia vyeti vya ndugu zao kuombea kazi.
 
Wanalipwa makato waliokatwa kutokana na kufanya kazi kipindi hicho, ni haki yao kupewa.
 
Umeambiwa kuwa malipo ni Ile michango yao pekee kwenye mifuko ya kijamii na sii michango ya mwajiri🥱
 
kunge kuwa na Uchunguzi mkali ungewaacha je kina bashite?na watu kibao tu waliokuwa na ukaribu na wakubwa?!!mbona jeshini na polisi hawakugusa?na huko ndiko walipo wengi sana
Hata kwenye majeshi nako kulikuwa na double standards na ndio maana upande wa uhamiaji waliwatoa wenye vyeti feki pamoja na kwamba nao ni jeshi lakini Kwa vile kelele zao zisingewaathiri kama majeshi mengine wakawafukuza!
 
Wewe umeeleza process ndefu! Mimi nina kakaa angu ni mwalimu kwasasa shule ya msingi, alipata F form 4 yake lakini anatumia cheti cha kakaangu mwingine ambae alipata Division 4.28! Alichukua kile cheti cha brother mwingine akaenda kusomea ualimu na mpaka sasa huko vyeti vya shule vinatambulika kwa jina la brother mwingine ila mtaaani anatambulika kwa jina lake halisia, ili panga lilimkosa cos Brother mwenye cheti si mwajiliwa issue inakuja kama we mwajiliwa na huyo mwenye cheti nae mwajili alafu wote mko Government hapo hutoki salama.
 
Anza na Bashite
 
You nailed it.

Pia hata mfumo wa elimu ulikua umekaza sna hapo nyuma. Haukupi nafasi ya Kurudia na kurekebisha makosa kw aurahisi.

Hivyo mtu anaona bora kufoji tu.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
mwajiri ana uwezo wa kuamuru mfuko wa hifadhi ya jamii usimlipe mwajiriwa mafao yake yote, ili hali mkataba ulikuwa baina ya mwajiriwa na management ya mfuko wa hifadhi ya jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…