Inaonekana hata hujui chanzo cha tatizo lilikuwa ni wapi?!! Yaani mimi nimetumia cheti cha mtu cha elimu ya kidato cha nne, nikakitumia nikasomea kidato cha sita, nikafaulu, nikaingia chuo kikuu kusomea udaktari, nikapiga miaka yangu sita, nikafaulu vizuri, nikapiga masters yangu, nikapata kazi ya kutibu wagonjwa hapo utasemaje nimesababisha vifo kwa watu?
Inshu kubwa haikuwa vyeti vya taaluma bali ni cheti cha kidato cha nne na hizo pesa wanazolipwa sio za Serikali ni michango yao waliyochangia kwenye mifuko ya jamii.