Langu ni hilo!
Vyeti feki, ni wahujumu nchi kama ilivyo Kwa mafisadi na wezi wengine!
Wameisababishia Serikali hasara kubwa, Kwa elimu yao ndogo, wamesababisha vifo vya wananchi Kwa kutoa huduma chini ya kiwango.
Endapo Serikali itawalipa hao vyeti feki, nimekusudia kuipeleka mahamani Serikali.
Itajulikana ikiwa Serikalini kuna wanufaika wa malipo haya chini ya mwamvuli wa wafoji vyeti.
Unaandika kwa hisia zako zisizo na ushahidi na kwa kulishwa maneno tu ya watawala waovu..
Una ushahidi hata mtu mmoja unayedai "amesababisha hasara au kifo cha mtu yeyote" kwa sababu ya hiki inachosema "walikuwa na elimu ndogo..?"
Ukitoa ushahidi hapo, mimi pia nitakupa ushahidi wa "wenye elimu kubwa - stashahada, shahada, masters, PhD nk" lakini wenye ufanisi zero kazini kiasi cha kusabisha hasara kwa taifa na pengine vifo kwa watu wengi...!
KWA HIYO SASA;
Kesi yako hiyo ukifanikiwa kuifungua, basi juwa na hakika ya jambo moja kuwa, utashindwa asubuhi na mapema kabla jogoo hajawika...!!
Kazi haifanywi na makaratasi yaitwayo "vyeti". Kazi hufanywa na mtu na matokeo kuonekana...
Kwa mantiki hiyo, watu hawa walikuwepo physically kila mtu akiwaona wakifanya kazi zao vyema na taifa kunufaika na kazi ya mikono yao. Hawakuwa "watu hewa..."
Kwa hiyo hawajaiba popote, hawajamwibia mtu yeyote. Kilicholipwa ni stahili yao..
Na ofcoz kama ni mashitaka, basi ni serikali ndiyo inayopaswa kufunguliwa mashitaka kwa kunyima/kunyang'anya watu haki zao na kuwadhalilisha na wengine kuugua magonjwa ya shinikizo la damu kiasi cha wengi wao kupoteza maisha na familia zao kuvurugika/kusambaratika..
Watu ambao serikali yenyewe iliwapa ajira hizo kwa kupitia michakato halali ya kuajiri na ile ya malipo. Iweje ghafla serikali hiyohiyo iwaone watu hao hao hawana sifa na ni wezi...??
No way..! Yenye makosa makubwa hapa ni serikali...
Iwarudishe watu kazini na iwalipe haki zao zote na pia ilipe gharama za usumbufu iliyowapatia...!