Hata makamu kutajwa na jambazi mahakamani ni aibu kubwa alipaswa ajiuzulu mana alishiriki ujambazi wa kidola alipokua waziri.
Watanzani tumekubali kuwapa waovu nchi iliyoumbwa na Mungu mwenye sifa zote za haki na utakatifu kuwa mali yao.
Katiba kamwe haitapatikana chini ya CCM ,labda jeshi liwe limeshika nchi kwa muda ili lisimamie hawa wanasiasa wanaoua maslahi ya nchi kwa kulinda vyama vyao huku majeshi yetu wakitumika kama manamba na maslahi duni tofauti na wanasiasa waliojaa ubinafsi na starehe kupitiliza.
Watu wanalesha kwenye mabaa na magesti mwaka mzima halafu tutegemee wapate muda wa kufikiri mustakabali wa nchi.?
Haiwezekani !
Hakuna katiba mpya itakayosimamiwa na wanasiasa hawa wanaowaza kuitafuna nchi.
Katiba ya Warioba imejaa mambo mengi ya msingi lakini wapuuzi na vyama vyao waliona mambo mawili tu :- Serikali mbili,serikali tatu na madaraka ya kuingia ikulu( madaraka).
Hawana muda wa kujadili maslahi ya umma kama makazi bora , ardhi na rasilimali za asili kuwanufaisha wote mana ni mali ya Mungu. Kodi ndio ijenge barabara ila gesi,wanyama ,madini, misitu, mafuta,mlima kilimanjaro n.k. iwe na fungu la kumpa kila mtanzania asiye na ajira wala kumiliki ardhi na nyumba yenye thamani kubwa.
Ujinga wa wanasiasa ulipelekea Dr. Mvungi akauwawa na majambazi ya kisiasa yasiyotaka katiba mpya kwa sababu alikataa kununuliwa . Alisema ni bora abaki jalalani kuliko kusaliti kazi nzuri ya Tume ya Warioba.
Lakini pia suala la Serikali Tatu na mbili ni upuuzi tu mana maendeleo hayawezi kuletwa na Wahuni hata pangekua na serikali mia moja.
Maendeleo yataletwa na watu waaminifu ,wachamungu wa kweli na watenda haki sio magavana wahalifu na wale kama walivyotajwa na Sabaya mhalifu aliyetumia uhalifu kulinda mali za Chama badala ya kwenda mahakamani.
Hata wao hawaiamini mahakama zaidi ya kufanya ujambazi wa kidola kwa wanaowatuhumu kukwepa kodi . Mtu kama amekwepa kodi au ameiba mali za chama alipaswa ashitakiwe mahakamani na sio kupigwa au kutishiwa maisha.
Kuliko kuibadili katiba hii chini ya mivutano ya Chadema na CCM na vyama visivyo na msimamo vinavyokaa katikati kusubiri mshindi waungane naye ni bora tubaki na hii iliyotungwa wakati wa Mwalimu akiwa hai. Kidogo wale waasisi walikua na ubinadam na kujali utaifa.
Hawa CCM madaraka na Chadema wajuaji wa kila kitu hawatatuletea Kamwe katiba mpya labda Mungu aingilie kati itokee serikali ya mpito chini ya majenerali wa Jeshi.
Eti nchi imekaa kimya inawasikiliza familia ya kina Gwajima na wale wasemaji wa vyama sijui kijana gani yule na makatibu wake waajabu ajabu. Kweli tutegemee Katiba mpya. ?
Tumtegemee mtu mmoja kama Mungu ndio ikimpendeza alete katiba mpya?? Duuh,
Bora tumtegemee Mungu asimame mwenyewe mana hatishwi,hahongwi, haogopi, hashindwi, hadhulumu , hasemi uongo na hadanganywi na yeyote.