SoC02 Iko wapi dhana ya uwajibikaji?

SoC02 Iko wapi dhana ya uwajibikaji?

Stories of Change - 2022 Competition

Fauster Mlilimko

New Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
4
Reaction score
5
Na mwandishi Fauster Fredricky, twende pamoja,
Dhana ya uwajibikaji ni dhana ya muhimu katika maisha ya maendeleo kwani ni moja kati ya mambo ya msingi katika kuleta maendeleo, dhana hii hufanya watu kutekeleza majukumu yao husika katika wakati sahihi na hivyo kurahisisha ufikiwaji wa malengo binafsi na nchi kwa ujumla. Tunapowajibika na majukumu yetu kwa wakati sahihi tunatumia pia muda wetu vizuri na hivyo kutuwezesha kuweza kufanya mambo mengi kwa mpangilio mzuri.

Katika masuala ya sheria na haki kuna msemo unasema kuwa "kila mtu ana haki na wajibu" na hivyo huwezi kupata haki yako kama hautekelezi wajibu wako kwani mambo haya ni sambamba nayo yanaenda pamoja.

Hali ngumu ya maisha pamoja na dhana ya umasikini vinaweza pia kuchochewa na uwajibikaji katika majukumu yetu na hivyo japo hali imekuwa ngumu lakini hatupaswi kukata tamaa katika kuwajibika kwani hali ya uchumi ni kama upepo ikiwa na maana kuwa kuna wakati ambapo unakosa muelekeo maalumu.

Hali ngumu ya maisha imekuwa changamoto kubwa inayowakumba watu wengi katika zama hizi hapa nchini kwetu kiasi cha kupelekea kukata tamaa na kukosa matumaini kuwa ni mambo ambayo ni ya kawaida katika jamii zetu.Ile kauli ya waswahili kuwa "kila kukicha ni afadhali ya jana" imekuwa ikidhihirika wazi wazi kati ya watu, vilio vinasikika wanyonge wanalia lakini hakuna wa kuwafuta machozi.

Wanyonge wamebaki wakiienzi ile kauli ya hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoisema kuwa "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe" na hivyo kila mtu kwa nafasi yake anaweka bidii katika kujitafutia ridhiki japo kuweza kukidhi mahitaji ya chakula kwa familia.

Katika hali ya maisha yaliyo na tumaini dogo sisi vijana tunapaswa kutumia hazina ya elimu tuliyoipata ili kuweza kujinasua na janga hili la ugumu wa maisha kwa kuwajibika. Kijana unahitaji kuachana na dhana potofu inayosema"kijana ni taifa la kesho" dhana hii so ya kweli kwani kijana ni taifa la leo na hivyo unahitaji kuipambania leo ili kutengeneza kesho iliyo njema kwa kuitumia elimu tunayopata kutoka shuleni na katika maisha yanayotuzunguka ili kuweza kuwajibika katika kujipatia maendeleo.
Kijana usiiache elimu kwenye makaratasi ya vyeti tu na kusubiri kuajiriwa, dunia tunayoishi ina mengi zaidi ya hayo yale ambayo ni mazuri zaidi na yenye tija katika jamii na maisha yako. Elimu tunayoipata isiishie pale darasani tu bali tuitumie vyema kwa kuona fursa zote zinazotuzunguka katika jamii na kujifunza kuzitumia vyema hizo fursa.

Ingawa mfumo wa elimu hapa nchini kwetu hautuandai vyema katika kujiajiri na kutumia ujuzi wa nje ya vitabu lakini yatupasa kuendana na kasi ya mabadiliko ya dunia na hivyo hatuna budi bali ni kuwajibika zaidi ili tuweze kuzifikia ndoto zetu bila kukata tamaa huku tukiichukua Ile hatua muhimu ya kuanza kwani kutoka hapo tutasonga mbele daima kumbuka "mabadiliko yanaanza na mimi"
Dhana ya uwajibikaji imepokea mabadiliko hasi pamoja na yale yaliyo chanya ambayo yamerahisiha dhana hii na kuiongezea maana zaidi. Mfano wa mabadiliko chanya katika uwajibikaji ni maendeleo ya sayansi na teknolojia kupitia mashine mbali mbali , kompyuta, simu na ongezeko la utandawazi kwanamna ambayo imefanya kuweza kurahisisha utendaji kazi kwa watu na kupelekea kuchochea maendeleo binafsi ya jamii kwa ujumla .

Iko wapi dhana ya uwajibikaji?, viongozi kwa wananchi , wananchi katika majukumu yao ni ukweli usiofichika kuwa dhana ya uwajibikaji imekuwa ikipuuziwa na baadhi yetu, hali inayochochea hali ngumu ya maisha lakini pia kukosa maelewano baina ya watu na migogoro isiyokwisha katika familia na jamii.Kama raia yatupasa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yetu ili kuleta maendeleo yetu.
Serikali pia bila kuupizia sekta hata moja inapasa kuwajibika kwa kifuata sheria zilizowekwa kwenye katiba yetu na kuwajibika kwaajili ya manufaa ya taifa letu hii italeta chachu kwa vijana na kuwatengenezea fursa mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Iko wapi dhana ya uwajibikaji?, mabadiliko ya teknolojia na sayansi pamoja na utandawazi kwa njia ya simu janja yameiba dhana hii na kuidhoofisha hasa kwa vijana kwani matumizi ya simu janja yamekuwa yakiochochea upotevu wa muda wa kazi miongoni mwa vijana na hivyo kupeleka utendaji kazi hafifu na chini ya viwango, kufuatilia kirasa za udaku na michezo isiyo na maadili imekuwa na sehemu ya vijana wengi na hivyo kupoteza dhana ya uwajibikaji.

Iko wapi dhana ya uwajibikaji , hali ya maisha inawafanya wazazi kutokufuatilia malezi ya watoto wao na hivyo kujikita katika kutafuta pesa za mahitaji ya familia na hivyo kuwaachia jukumu la malezi wafanyakazi wa ndani na kumpelekea matukio ya ajabu na kitisha kama vile mauaji ya watoto pamoja na ulawiti pia watoto kukosa malezi sahihi ya wazazi wao kunatengenza taifa la kesho lenye watu wasio na maadili na nidhamu.

Iko wapi dhana ya uwajibikaji? ikiwa walimu mashuleni wamekuwa hawafundishi kama invyowapasa wito wao bali nao wanafanya ili mradi mwisho wa mwezi ufike nao waweze kupata mishahara yao, ule ufuatiliaji wa mwanafunzi endapo atakuwa Hana matokeo mazuri katika masomo au nidhamu nzuri hakuna tena na badala yake sikuhizi kuna dhana ya anayetaka kuelewa na ajipambanie naye aonekanaye kuwa mjinga basi atabaki na ujinga wake. Mwishowe ni ongezeko la wimbi wa vijana wasio naelimu ya kutosha ambao wanakuwa mzigo kwa wazazi wao.

Iko wapi dhana ya uwajibikaji? ikiwa serikali inafanya maamuzi bila kupitishwa na bunge ambayo ndio wawakilishi wa wananchi na kuweka tozo ambazo zimezidi kuwakandamiza wanyonge na kuwasukuma katika dimbwi la umasikini zaidi, dhana hii muhimu inataka serikali kuwajibika kwaajili ya wananchi wake nayo sasa yapuuzwa na hivyo maamuzi yasiyo na tija kwa wananchi yanafanywa hata leo.

Iko wapi dhana ya uwajibikaji, mauaji yamekuwa yakiongezeka kila leo katika nchi yetu, ajali za barabarani zitaendelea kuwepo na wengi watazidi kupoteza maisha kwasababu rushwa inayotokana na ukosefu wa uwajibikaji miongoni wa maaskari wa barabarani itaendelea kuwepo pia uzembe baina ya madereva kwa kukosa uwajibikaji na wengi wao kuendesha magari wakiwa wameolewa au kuchezea simu.

Mwisho yatupasa kukumbuka kuwa kutimiza wajibu wetu ni chanzo cha maendeleo yetu na hivyo ni rai yangu kwa vijana kutumia nguvu zetu kuwajibika ili tuweze kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko, tuwajibike katika sekta zote ikiwa ni siasa, uchumi na jamii.Tukumbuke ule msemo usemao "timiza wajibu wako upate haki yako".
 
Upvote 1
Back
Top Bottom