Itoye
JF-Expert Member
- Sep 29, 2017
- 531
- 1,023
Wakuu Salaam,
Jana Mh. Rais kwa mamlaka aliyonayo amewafutia adhabu ya kifo wafungwa zaidi ya 200 waliokuwa wanasubiri kutekelezwa kwa adhabu hiyo na ni mara ya pili binafsi nimemsikia Mh. Rais akizungumza juu ya adhabu hii kuwa na kuonyesha hayuko tayari kuitekeleza maana dhamiri yake inamwambia si jambo sahihi kulifanya.
Binafsi namuunga mkono kwenye hilo maana kama sheria inasema kuua mtu ni kosa sasa kwa nn sheria nyingine tena imruhusu mtu mwingine kuua na mbaya zaidi inamruhusu kuua wengi sana kama Mh. Rais alivyogusia, lakini pia kutuoa uhai wa mwanadamu mwenzako katika mazingira yoyote yale si jambo dogo na jepesi.
Ni wakati sasa sheria hii ikafutwa na hukumu ya juu kabisa ibaki kifungo cha maisha, Mwigulu Nchemba Mheshimiwa waziri wa Sheria jambo hili limekaaje kwa upande wako au kuna mchakato unaendelea?
Cc: Pascal Mayalla