Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli ateua Baraza la Mawaziri lenye Wizara 23. Aunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli ateua Baraza la Mawaziri lenye Wizara 23. Aunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

kwa nini tunaingiza udini? sioni kosa lolote hapo maana watanzania wote tunataka maendeleo tu sio dini za watu, maaana hata akiwa mkiristo kinacho takiwa ni awe mwadilifu kwa watu wote,
Kwa wewe hakuna shida lakini kiuhalisia haya ni mambo ya kibaguzi
Baraza hili ni la muungano hakuna mzanzibari hata mmoja
Magufuli tangu ameingia madarakani target yake ni kuondoa waislamu na wachaga serikalini na kwa kiasi kikubwa amefanikiwa
 
Acheni wanga kwenye kazi za wengine, mtu unamwanzia nani atumbuliwe dah, tutafute pesa tuache mawazo ya kimaskini
 
Kuna watu hawatalala leo kwa msongo wa mawazo, kwa kukosa uteuzi.

Dkt. Kigwangalla hana option, zaidi ya kwenda kugombea nafasi ya uongozi Simba SC, ili apate nguvu ya kumdai na kumchamba Muddy zile hela alizo ahidi wakati ananunua hisa.

Pasco Mayalla amejitutumua sana kuweka makala za kumkosha Admini, ila nafasi zimejaa so asubiri uteuzi wa mwaka 2035.
Pascal Mayalla
Leslie Mbena

kazi na siasa
 
Hii ina shape picha ya Raisi ajaye kama mheshimiwa atapumzika. Kama watafuata mazoea ya kubalishana kidini basi Jaffo au KM, otherwise namuona Dotto Biteko Raisi ajaye.
 
Matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma kuhusu Uteuzi uliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo tarehe 05 Desemba 2020



========
Rais Magufuli pia amewateua kuwa Wabunge Dkt. Dorothy Gwajima(Alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI - Afya) na Dkt. Leonard Chamuliho (alikuwa Katibu Mkuu Uchukuzi).

Pia Rais Magufuli ameunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Orodha ya Mawaziri kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi.

1. Wizara ya Maji - Juma Aweso

2. Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo - Innocent Bashungwa

3. Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu - Jenister Mhagama

4. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Dkt. Doroth Gwajima

5. Wizara ya Uwekezaji ofisi ya Rais - Profesa Mkumbo Kitila

6. Wizara ya Katiba na Sheria - Dkt. Mwigulu Nchemba

7. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Profesa Joyce Ndalichako

8. Wizara ya Mifugo na Uvuvi -Mashimba Mashauri Ndaki

9. Wizara ya Maliasili na Utalii - Dkt. Ndumbalo Damas

10. Ofisi ya Rais TAMISEMI -Suleiman Jaffo

11. Wizara ya Madini - Dotto Biteko

12. Wizara ya Nishati - Dkt. Medard Kalemani

13. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho

14. Wizara ya Kilimo - Profesa Adolph Mkenda.

15. Wizara Viwanda na Biashara - Mwambie Geofrey Idelphonce

16.Wizara ya Mambo ya Ndani - George Simbachawene

17. Wizara ya Muungano na Mazingira - Ummy Mwalimu

18. Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari - Dkt Faustine Ndugulile

19. Wizara ya Fedha na Mipango - Dkt. Philip Mpango

20.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Profesa Paramagamba Kabudi

21. Wizara ya Ardhi na Makazi -William Lukuvi

22. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Elias John Kwandikwa

23. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Capt Mstaafu George Mkuchika


Manaibu Waziri

1. Wizara ya Viwanda na Biashara- Kigae Silaoneka

2. Wizara wa Ardhi- Angelina Mabula

3. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira- Patrobas Katambi

4. Wizara ya Mambo ya Ndani- Hamis Hamza Hamisi

5. Wizara ya Fedha- Mwanaida Ali Khamis

6. Wizara ya Elimu- Kipanga Juma Omar

7. TAMISEMI- Dk Festo Ndugange

8. Wizara ya Nishati- Stephen Byabato

9. Menejimenti Utumishi wa Umma- John Ndejembi

10. Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Kundo Mathew

11. Wizara ya Mifugo- Pauline Gekul

12. Wizara ya Madini- Ndulane Kumba

13. Wizara ya Ujenzi- Godfrey Kasekenya

14. Ofisi ya Waziri Mkuu wenye ulemavu- Ummy Ndelinanga

15. Wizara ya Maji- Maryprisca Mahundi

16. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Abdallah Ulega

17. Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Mwita Waitara

18. Wizara ya Mambo ya Nje- William Olenasha

19. Wizara ya Maliasili na Utalii- Mary Masanja

20. Ofisi ya rais TAMISEMI- David Silinde

21. Wizara ya Kilimo- Hussein Bashe

22. Wizara ya Afya- Dk Godwin Mollel

23. Wizara ya Katiba na Sheria- Pinda Mizengo

View attachment 1642517
View attachment 1642518
View attachment 1642519
View attachment 1642520

Du yule mzee mstaafu wa CRDB hayumo? nilitegemea baada ya Plan kurudishiwa wizara yake ya njuruku mzee wa watu angekuwemo kwenye baraza .
 
Mwita Waitara
Patrobas Katambi
David Silinde
Prof.Mkumbo
Shonza
Geguka


Next Dada angu Halima mdee namuona ndani ya Baraza.

Ester bulaya
Nusrat wanje Hawa Ukuu wa mkoa na wilaya nao unawanyemelea.



JPM anaendelea kudhihirisha Ni mtu mwenye maono haswaa kwa kuwapa nafasi vijana wote Tz pasipo na chuki ya upinzani wao wa mwanzo.

Tz I aendelea kujengwa kutokea Kila pembe ya nchi hii.
 
nawapa pongezi wteule wote lakini pia nawapa pole kwani awamu hii ya 5 usisherehekee kama umeula bali unatakiwa ukaze mkanada wako na uchape kazi mchana na usiku bila kuchoka, ukubali kujitoa kwa ajili ya wananchi.

Hongera za kipekee ziende kwa mhe. Awesu kwani anastahili kabisa kufika hapo alipo fika naamini kama mawaziri wengine wataiga utendaji wa mhe Awesu wataendelee kutetea nafasi zao,
We uko bize unapongeza tu una matatizo gani? Au ni upungufu wa akili
 
Du yule mzee mstaafu wa CRDB hayumo? nilitegemea baada ya Plan kurudishiwa wizara yake ya njuruku mzee wa watu angekuwemo kwenye baraza .
Hiyo wizara huwa ina manaibu waziri wawili, kwaio tuendelee kutega sikio.
 
Kati ya mawaziri 23 waislamu wawili tu duh
Waislam inabidi mpige shule sio kukimbilia madrasa tu someni elimu zote mbili
 
Haya sasa tukalijenge Taifa Letu pendwa.
 
Back
Top Bottom