Hii dhana kwamba Waislamu hawakwenda shuke imetumiwa tangu kupata Uhuru kuwaengua Waislamu. Kuna bwana mmoja alitoa orodha ya Waislamu 300 wenye PHD za fani mbali mbali, karibuni zote, hata Marine sciences (PHD). Hiyo ni Zaidi ya miaka 10 iliyopita! Mtu akitaka kutukana hachagui tusi wala hajali facts. Ukweli ni kwamba, kama angekuwa rais ni Mwislamu na akafanya uteuzi kama huu, Wakristo wote mngeruka na kupaaza sauti kuwa ni 'mdini'. Tumeyaona hayo wakati wa Mwinyi na wakati wa Kikwete ambaye aliponzwa kuteuwa 30% tu ya Waislamu katika baraza lake, lo! Kauli mbiyu ya "Mdini' ilizagaa kote Tanzania! Nani asiyejua sakata la kuzongwa kwa Dr. Dau?, Kighoma Malima, Iddi Simba etc. kwa tuhuma za 'udini'? Hao wala hawakuwa viongozi wa juu!!!
Ili mradi, kila anayezungumzia ubaguzi dhidi ya Waislamu ni 'mdini'. Wanaoishiria hapa kukosekana kwa Waislamu si wadini, ni watu wanaosema ukweli tu. Na muda wa kuwa hatuambiani ukweli nchi hii itaangamia. Rais Magufuli mwenyewe kila mara anasema "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu" Sasa asikie ukweli huu, kwamba hakufanya uadilifu katika Baraza hili na lile lililopia kwa kuwatenga 'makusudi' Waislamu. Lau wangefanyiwa Wakristo, wao pia wangesema hivyo, wazi wazi.
Why Christians in Tanzania are taking Muslims for granted? Having a proportionate representation of ethnic, religious and gender group in a cabinet make-up in Africa is not just a luxury....it saves a very important role of ensuring equitable service delivery to all citizens. In Africa where people's loyalty is mainly to their tribes, religions, and other attachments rather than 'a state' , a wide spread disenfranchisement of a particular category of people has severe consequences on that group's equal enjoyment of government services. If President Magufuli is not aware of this fact, I just wonder what type of a leader is he. No. I believe this flagrant bias is a conscious and deliberate act.
The more we could speak about this openly, the better will be the future of a united Tanzania. This CAN NOT GO ON- business as usual!