Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF)

Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF)

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau wa JF

Nawasalimi kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TPSF.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani leo Mei 31, 2021 amekutana kwa mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Sekta binafsi Nchini ( TPSF)

Mkutano huo uliofanyika Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es salaam ulijadili njia za kukuza biashara, kuongeza uwekezaji pamoja na kupanua wigo wa kodi nchini

Viongozi wa TPSF wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi Angelina Ngalula wamepongeza sana Mama Samia kwa kuimarisha mahusiano baina ya Serikali na Sekta binafsi nchini.
 
The Diplomat

TPSF.jpg

Katika muendelezo wa kutengeneza mazingira bora na rafiki ya Biashara na Uwekezaji nchini, Leo Mei 31, 2021, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na Viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Ikumbuke kuwa Sekta Binafsi ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu kupitia uwekezaji unaofanywa na wafanyabiashara, ambao umekuwa ukizalisha ajira na mapato kwa Serikali kupitia kodi zinazolipwa.

Kwa kulitambua hilo, Mhe. Rais katika kikao na viongozi hao amewapongeza wadau wa Sekta Binafsi kwa kuendelea kutekeza wito wake wa kukuza uchumi kwa vitendo na kuwahakikishia Serikali yake itaendelea kuwapa ushirikiano na kuwaunga mkono katika juhudi hizo.

Kwa upande wa viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi, wamemueleza Mhe. Rais kuwa wapo tayari kutekeleza vipaumbele vya Serikali yake alivyotoa wakati akihutubia Bunge, na kuongeza kuwa wao kama Sekta Binafsi kwa kiasi kikubwa wameanza kuvifanyia kazi.

Pia wamejadili namna ya kuongeza vyanzo vya Mapato kwa Serikali kwa maana ya walipa Kodi na Mazingira ya kibiashara yanayohitajika kufanikisha hilo, ambayo kwa kiasi kikubwa Serikali ya Rais Samia inaendelea kuyatengeneza.

Kwa upande wa ajira, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo amesema, Wamezungumza namna ya kuongeza tija ili kuweza kuzalisha ajira kwa wingi kwa Watanzania kushirikishwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati.

Aliongoze kuwa yote haya ni katika kuunga Serikali mkono jugusu za Serikali ili kuvutia wawekezaji wengi nchini.

Mwisho, Mhe. Rais ameahidi kuyafanyia kazi maoni yaote yaliyotolewa na yatakayotolewa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Juni 2021.
 
Mama anakutana kila siku na makundi mbalimbali ya watu.

Ni muda muafaka sasa aanze ziara ya kukutana na wananchi.

Hayo makundi sio yaliyompigia kura kama makundi. Aende kwa wananchi.
 
Alipigiwa kura?
Kwani kwenye zile karatasi za kura za mwaka 2020, ukilinganisha na za miaka ya nyuma, jina lililoanza lilikuwa la mgombea uRais au Umakamu?

Kumbukumbu Zangu zinaniambia, jina lililoanza lilikuwa la makamu, kwa CCM, alianza kuandikwa Samia Kisha akafuata mwendazake. Hivyo ukilinganisha na karatasi za kura za miaka ya 2015, 2010, 2005, 2000, tunakuwa tulisetiwa toka kwenye hizo karatasi kuwa tunampigia kura Samia Suluhu Hasan kuwa Rais.

Mwendazake kwenye kampeni alikuwa anatoa kauli kuwa
Mwinyi, Mkapa na Kikwete mliwapa miaka 10, mbona Mimi mnataka niishie mitano
Na majamaa yalifanya kweli, aliishia miaka 5 na siku 131 tu Kama Rais wa Tanzania.

Jumlisha, toa Kisha zidisha.
 
Mama anakutana kila siku na makundi mbalimbali ya watu.

Ni muda muafaka sasa aanze ziara ya kukutana na wananchi.

Hayo makundi sio yaliyompigia kura kama makundi. Aende kwa wananchi.
Ndio maana ana wasaidizi kama RCs na DCs
 
Kwani kwenye zile karatasi za kura za mwaka 2020, ukilinganisha na za miaka ya nyuma, jina lililoanza lilikuwa la mgombea uRais au Umakamu?

Kumbukumbu Zangu zinaniambia, jina lililoanza lilikuwa la makamu, kwa CCM, alianza kuandikwa Samia Kisha akafuata mwendazake. Hivyo ukilinganisha na karatasi za kura za miaka ya 2015, 2010, 2005, 2000, tunakuwa tulisetiwa toka kwenye hizo karatasi kuwa tunampigia kura Samia Suluhu Hasan kuwa Rais.
Nalijua hilo,sasa mbona time ilitutangazia matokeo ya uraisi tu,umakamu hatukutangaziwa?
 
Rais Samia amekuwa na kikao na viongozi wa wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es salaam.

Katika kikao hicho wafanyabiashara hao wamemweleza Rais Samia namna walivyojipanga kutekeleza vipaumbele vya serikali ya awamu ya sita kama vilivyotangazwa na Rais pale bungeni.

Source: ITV habari!
Awe macho. Wafanyabiashara kimsingi ni watu wabinafsi wenye uchu wa faida kubwa tu. Lazima ajue sheria kudhibiti biashara ndio hufanya kushamiri biashara kuleta maendeleo kwa kila mtu.
 
Awe makini tuu wasije wakamuingiza "kingi" wafanyabiashara wa nchi hii tunawajua.hasa hawa asians!
 
Jambo jema Sana kwa ustawi wa sekta binafsi nchini
 
hamna hata picha

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI TPSF

MICHUZI BLOG AT MONDAY, MAY 31, 2021 HABARI, IKULU, MATUKIO,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) mara baada ya Kikao chao kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Kikao na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi mbalimbali (Wanawake) wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) mara baada ya Kikao chao kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali (Wanaume) wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) mara baada ya Kikao chao kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Source : https://issamichuzi.blogspot.com/2021/05/rais-samia-akutana-na-kufanya_31
 
Nalijua hilo,sasa mbona time ilitutangazia matokeo ya uraisi tu,umakamu hatukutangaziwa?
Ili ujue kuwa kura zilipigwa mahsusi kwa Samia, aliyetangazwa kuwa kashinda uRais, alitoboa kwenye huo uRais hata kwa miezi sita(nusu mwaka) tokea alipotangazwa na tume?

Calculation.
 
Rais Samia amekuwa na kikao na viongozi wa wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es salaam.

Katika kikao hicho wafanyabiashara hao wamemweleza Rais Samia namna walivyojipanga kutekeleza vipaumbele vya serikali ya awamu ya sita kama vilivyotangazwa na Rais pale bungeni.

Source: ITV habari!
Mama Fanya ziara mikoani. Paper work zilizalisha escro.
 
Sekta binafsi kwa hakika ndiyo injini imara ya kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Sijui ni kwa nini mwendazake hakuona kabisa umuhimu wa sekta hii!
 
Back
Top Bottom