The Diplomat
Katika muendelezo wa kutengeneza mazingira bora na rafiki ya Biashara na Uwekezaji nchini, Leo Mei 31, 2021, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na Viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Ikumbuke kuwa Sekta Binafsi ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu kupitia uwekezaji unaofanywa na wafanyabiashara, ambao umekuwa ukizalisha ajira na mapato kwa Serikali kupitia kodi zinazolipwa.
Kwa kulitambua hilo, Mhe. Rais katika kikao na viongozi hao amewapongeza wadau wa Sekta Binafsi kwa kuendelea kutekeza wito wake wa kukuza uchumi kwa vitendo na kuwahakikishia Serikali yake itaendelea kuwapa ushirikiano na kuwaunga mkono katika juhudi hizo.
Kwa upande wa viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi, wamemueleza Mhe. Rais kuwa wapo tayari kutekeleza vipaumbele vya Serikali yake alivyotoa wakati akihutubia Bunge, na kuongeza kuwa wao kama Sekta Binafsi kwa kiasi kikubwa wameanza kuvifanyia kazi.
Pia wamejadili namna ya kuongeza vyanzo vya Mapato kwa Serikali kwa maana ya walipa Kodi na Mazingira ya kibiashara yanayohitajika kufanikisha hilo, ambayo kwa kiasi kikubwa Serikali ya Rais Samia inaendelea kuyatengeneza.
Kwa upande wa ajira, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo amesema, Wamezungumza namna ya kuongeza tija ili kuweza kuzalisha ajira kwa wingi kwa Watanzania kushirikishwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
Aliongoze kuwa yote haya ni katika kuunga Serikali mkono jugusu za Serikali ili kuvutia wawekezaji wengi nchini.
Mwisho, Mhe. Rais ameahidi kuyafanyia kazi maoni yaote yaliyotolewa na yatakayotolewa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Juni 2021.