Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan anawaapisha mawaziri muda huu.
Wanaoapishwa leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma ni pamoja na Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya, Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali walioteuliwa Jumamosi Januari 8, 2022.
Mawaziri wapya wanaoapishwa ni;
- Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari)
- Hamad Masauni (Mambo ya Ndani)
- Dk Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu)
- Anjelina Mabula (Ardhi)
- Hussein Bashe (Kilimo).
Naibu mawaziri wapya walioteuliwa ni;
- Anthony Mavunde (Kilimo)
- Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani)
- Dkt. Lemomo Kiruswa (Madini)
- Ridhiwani Kikwete (Ardhi)
- Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).
Mawaziri wanaopishwa baada ya kubadilishiwa Wizara ni
- Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora),
- Ummy Mwalimu (Afya)
- George Simbachawene (Katiba na Sheria)
- Profesa Joyce Ndalichako (Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
- Innocent Bashungwa (Tamisemi)
- Profesa Adolf Mkenda (Elimu)
- Dk Doroth Gwajima (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu)
- Mohamed Mchengerwa (Utamaduni, Sanaa na Michezo)
- Dkt Ashatu Kijaji (Uwekezaji, Viwanda na Biashara).
Naibu Mawaziri waliohamishiwa wizara ni pamoja na;
- Khamis Khamis (Muungano na Mazingira)
- Hamad Chande (Fedha na Mipango)
- Mwanaidi Khamis (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu)
Updates;
Prof. IBRAHIM JUMA, JAJI MKUU WA TANZANIA
Kwa mwananchi wa kawaida yeye anaangalia dola moja tu katika kutoa zile huduma ambazo mamlaka tumegawana. Lakini wote, wote tunaelekea kwenye ustawi wa jamii – kwenye umoja, amani, utulivu na maendeleo ya nchi. Nawapongeza sana kwa Imani ambayo mmepata ya kuweza kuchangia katika kustawisha maendeleo ya wananchi.
NAIBU SPIKA, TULIA ACKSON
Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii
RAIS SAMIA SULUHU
Nataka niseme jambo moja tu nina kaka zangu, Lukuvi na Kabudi mko wapi? Kaka zangu wawili hawa nimewavuta waje kwangu wanisaidie ili waje kunisimamia ninyi, kwa hiyo kuwaacha kwangu kwenye hiyo listi watakuja kwangu tuwasimamie ninyi.
Kuwaacha kwangu kwenye hiyo list ni kwakuwa wote ninyi hapa ni wadogo wadogo na mnahitaji kusimamiwa vizuri.
Kaka yangu Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia mazungumzo ya serikali na mashirika. Na ndiyo kazi sasa nataka nimkabidhi kindakindaki aendelee na kazi hiyo. Ila kazi yake kwakuwa haipo kwenye muundo haitangazwi wala nini. Kazi zote tutakazoingia ubia mashirika na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwahiyo yeye ni Baba Mikopo, Baba Negotiations.
Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi
Nimeona meseji, “Afadhali Lukuvi ametoka”, hajatoka! Mpo? Wengine wameanza kuletea meseji za ajabu ajabu wakijua atagombania Uspika. Hatagomania! Hatagombania, ana kazi na mimi.