Ikulu: Kikao cha kusaini hati za kuondoa hoja tano za Muungano zilizotatuliwa. Sasa rasmi mafuta na gesi kila mtu kivyake

Ikulu: Kikao cha kusaini hati za kuondoa hoja tano za Muungano zilizotatuliwa. Sasa rasmi mafuta na gesi kila mtu kivyake

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Kwa muhtasari, hoja hizo ambazo hii leo zinasainiwa katika hati ya makubaliano kuziondoa katika zile hoja ambazo tayari zimeshapatiwa ufumbuzi ni pamoja na ushirikishwaji wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwenye masuala ya kikanda na kimataifa.

Hoja nyingine iliyopatiwa ufumbuzi ni ushiriki wa Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Hoja ya tatu ni gharama za kushusha mizigo bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar.

Hoja ya nne ni utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia. Hoja ya namna ya kugawana mapato ya rasilimali ya mafuta na gesi asilia yatakapopatikana. Maelezo yanatolewa na Balozi Joseph Sokoine ambae ni naibu katibu ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na mazingira.

Balozi Sokoine: Ufumbuzi; Serikali zetu baada ya kujadiliana ziliamua kumtumia mshauri muelekezi, OPEC ya Uingereza ili atoe ushauri wa kitaalam kuhusu mgawanyo wa rasilimali ya aina hiyo kwa nchi za muungano. Kampuni ya OPEC ilikamilisha kazi hiyo na kuwasilisha mapendekezo kwa SMT na SMZ. Hata hivyo hoja nyingine ilijitokeza kwamba suala la mafuta na gesi asilia liondoshwe katika orodha ya mambo ya Muungano.

Baada ya majadiliano pande zote mbili zilikubaliana kuondoa masuala ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano hivyo sheria ya mafuta namba 21 ya mwaka 2015 mamlaka ya kuanzisha vyombo vya kusimamia mafuta na gesi asilia kwa kutumia sheria ya Zanzibar.

Hoja ya tano ni utaratibu wa kikao vya kamati ya pamoja ya serikali ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kushughulikia masuala ya Muungano.
========

 
Hivi mnafahamu lakini km hoja za Muungano zimepunguzwa Sana. Fwatilieni TBC mujue Mambo makubwa yaliyofanywa ya kupunguza hoja za Muungano


==
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania zimekutana kutia saini makubaliano ya kuondoa hoja tano za Muungano ambazo zimeshapatiwa ufumbuzi

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania zimekutana kupiga saini makubaliano hayo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zunguwa amesema zipo hoja nyingine sita zimeshatatuliwa bado kufikia makubaliano

Zungu ametaja hoja zilizoondolewa ni Ushirikishwaji wa Zanzibar kwenye masuala ya kimataifa na kikanda, Ushiriki wa Zanzibar katika ushiriki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, gharama ya kushusha mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar

Pia utafutaji na uchimbaji wa mafuta ya gesi asilia na utaratibu wa vikao vya kamati ya pamoja serikali ya mapinduzi ya zanzibar na serikali ya muungano ya kushughulikia masuala ya muungano
 
Saa mbaya utumbo huo hauna nafasi kwa sasa,watajijua wenyewe hapa kazi au sio? Tunamwondosha adui CCM hayo mambo si muhimu kama watu wanaheshimiana, nchi inakuwepo katika umoja amani na utendaji wa haki na ufuatwaji wa sheria.
Kama hayo hayapo hizo geresha hazina mashiko wakae nazo tu kwenye madroo.

Adui CCM amebakia na kura za wizi tu ndizo atakazopata, wananchi wote hapo mwanzo ilikuwa walio wengi, lakini sasa wananchi wote walio serikalini na kwengine kote wametia nia kuiondoa CCM wanasema liwalo na liwe,adui nambari one Tanzania.

CCM nuksi na wanatia fitna baina ya waTanzania ,inafikia waTanzania wanachukiana raia anamchukia polisi, polisi anamchukia raia hivyo hivyo kwa vyombo vingine vya serikali vikiwemo vya ulinzi na usalama,CCM wabaya sana ni chama kimekuwa kibaya sana na imewabidi wakiweke pembeni,watu hawafahamiani kwa ajili ya upandikizaji wa chuki,ccm wanapandikiza chuki hata baina ya ndugu na ndugu.
 
😀😀😀😀😀
Haya ni maigizo, hakuna jambo la muungano lililopungua, mambo ya muungano yapo kwa mujibu wa katiba.

Hizo zinazoitwa 'hoja za muungano' ni harakati tu za kujifurahisha za CCM.

Kichekesho zaidi ni Zanzibar inajadiliana na Tanzania!
 
Wakati serikali inahamasisha watu waende kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi mkuu, Chadema walikua wakihamasisha watu wasiende kujiandikisha mpaka ipatikane katiba Mpya Chakushangaza baada ya matokeo kutangazwa watasema wameibiwa kura.
 
Maccm na beberu Tanganyika wanaoikalia zanzibar kwa mabavu yanatapatapa...... Baada ya uchaguzi tu yanazirudisha tena....

Watz wamesema sasaaaa baaassaaa.......
Mpeni Maalif Seif nchi yake
Mpeni Tundu Lissu nchi yake
 
Wakati serikali ina hamasisha watu waende kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi mkuu, Chadema walikua wakihamasisha watu wasiende kujiandikisha mbaka ipatikane katiba Mpya Chakushangaza baada ya matokeo kutangazwa watasema wameibiwa kura.
Unamaanisha, watu milioni 29 walioandikishwa katika daftari la wapiga kura wote ni CCM?

Hivi akili zingine ziliumbwa na nani?

Au CCM inawaumbia akili zilizojaa ujinga?
 
Si walisema mambo ya muungano yaliishia kwenye ule mchanga so hatuwezi yatenganisha wamewezaje hawa watu.

Hizi ni porojo ila tuseme wote kwa pamoja ccmm wameshikwa pabaya wakitingishika tuu inazama
 
Mafuta na gesi sio jambo la muungano tena. Kila upande ukijigundulia mafuta yake na gesi yake ni mali yake binafsi kila upande wa Muungano.
 
Shime wazanzibari chukueni majembe sasa mkachimbe mafuta na gesi yenu. Sio Jambo la Muungano tena.
 
Back
Top Bottom