YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Kwa muhtasari, hoja hizo ambazo hii leo zinasainiwa katika hati ya makubaliano kuziondoa katika zile hoja ambazo tayari zimeshapatiwa ufumbuzi ni pamoja na ushirikishwaji wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwenye masuala ya kikanda na kimataifa.
Hoja nyingine iliyopatiwa ufumbuzi ni ushiriki wa Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Hoja ya tatu ni gharama za kushusha mizigo bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar.
Hoja ya nne ni utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia. Hoja ya namna ya kugawana mapato ya rasilimali ya mafuta na gesi asilia yatakapopatikana. Maelezo yanatolewa na Balozi Joseph Sokoine ambae ni naibu katibu ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na mazingira.
Balozi Sokoine: Ufumbuzi; Serikali zetu baada ya kujadiliana ziliamua kumtumia mshauri muelekezi, OPEC ya Uingereza ili atoe ushauri wa kitaalam kuhusu mgawanyo wa rasilimali ya aina hiyo kwa nchi za muungano. Kampuni ya OPEC ilikamilisha kazi hiyo na kuwasilisha mapendekezo kwa SMT na SMZ. Hata hivyo hoja nyingine ilijitokeza kwamba suala la mafuta na gesi asilia liondoshwe katika orodha ya mambo ya Muungano.
Baada ya majadiliano pande zote mbili zilikubaliana kuondoa masuala ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano hivyo sheria ya mafuta namba 21 ya mwaka 2015 mamlaka ya kuanzisha vyombo vya kusimamia mafuta na gesi asilia kwa kutumia sheria ya Zanzibar.
Hoja ya tano ni utaratibu wa kikao vya kamati ya pamoja ya serikali ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kushughulikia masuala ya Muungano.
========