Ikulu: Kikao cha kusaini hati za kuondoa hoja tano za Muungano zilizotatuliwa. Sasa rasmi mafuta na gesi kila mtu kivyake

Ikulu: Kikao cha kusaini hati za kuondoa hoja tano za Muungano zilizotatuliwa. Sasa rasmi mafuta na gesi kila mtu kivyake

Kwa muhtasari, hoja hizo ambazo hii leo zinasainiwa katika hati ya makubaliano katika kuziondoa katika zile hoja ambazo tayari zimeshapatiwa ufumbuzi ni pamoja na ushirikishwaji wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwenye masuala ya kikanda na kimataifa.

Hoja nyingine iliyopatiwa ufumbuzi ni ushiriki wa Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Hoja ya tatu ni gharama za kushusha mizigo bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar.

Hoja ya nne ni utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia. Hoja ya namna ya kugawana mapato ya rasilimali ya mafuta na gesi asilia yatakapopatikana. Maelezo yanatolewa na Balozi Joseph Sokoine ambae ni naibu katibu ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na mazingira.

Balozi Sokoine: Ufumbuzi; Serikali zetu baada ya kujadiliana ziliamua kumtumia mshauri muelekezi, OPEC ya Uingereza ili atoe ushauri wa kitaalam kuhusu mgawanyo wa rasilimali ya aina hiyo kwa nchi za muungano. Kampuni ya OPEC ilikamilisha kazi hiyo na kuwasilisha mapendekezo kwa SMT na SMZ. Hata hivyo hoja nyingine ilijitokeza kwamba suala la mafuta na gesi asilia liondoshwe katika orodha ya mambo ya Muungano.

Baada ya majadiliano pande zote mbili zilikubaliana kuondoa masuala ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano hivyo sheria ya mafuta namba 21 ya mwaka 2015 mamlaka ya kuanzisha vyombo vya kusimamia mafuta na gesi asilia kwa kutumia sheria ya Zanzibar.

Hoja ya tano ni utaratibu wa kikao vya kamati ya pamoja ya serikali ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kushughulikia masuala ya Muungano.
========

Sawa
 
Mi hata sielewi, wameondoa hoja tano, kisha wamezipeleka wapi, mwanzoni hizo hoja zilikuwa zimehefadhiwa wapi na sasa zimepelekwa wapi?.
 
Utaratibu wa sasa wa serikali ni kuwa kunapopatikana rasili Mali za madini kama gesi, mafuta, dhahabu asilimia 3% ya pato linarudishwa kwa halmashauri husika.

Tanzania ni nchi kubwa sana. Mfumo wa serikali kuu ambapo mtu mmoja tu ambae ndie rais aweze kuwahudumia RAIA zaidi mil 60. Ni lazima maeneo jamii za maeneo mengine yatasahaulika tu.

Mfumo wa State kama huu wa tz ambapo imeamua kuwa na state moja, unapaswa upanuliwe na kuwa na serikali 10 za majimbo na sio serikali tatu kama wengi wanavyotamani.

Kwani hakuna nchi moja duniani yenye marais 2. Ukweli ni kuwa kule znz wanachagua gavana. Hata kama ataitwa Rais.

Sasa kama tutaogopa kijiji kudai uhalali wa kumuliki rasilimali zinazoyoka kijiji husika kwanini Leo serikali ya Tanganyika na ile ya znz zimetia saini kukubali rasilimali ya znz isimamiwe na serikali ya znz pekee?!?!?
Naunga mkono kwenye utekelezaji wa sera za serikali lakini Serikali za majimbo hapana.

Watu wenye kuleta maendeleo ya haraka kwa ufanisi na ueledi ni mameya wa majiji na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Hawa watu ndo iwe jicho la maendeleo ya kwa maeneo hayo ambayo wewe watamani yawe ni majimbo.

Mfano ni mvua kubwa zilizonyesha mkoani Dar-es-salaam wa kulaumiwa ni serikali kuu au serikali za mitaa kupitia meya wa jiji na timu yake ya uongozi mkoani Dar?

Je, jiji la Dar lapaswa kuendelea kuachiwa ili siku yale maziwa na majito yarudi kama ilivyokuwa miaka ya 50s?

Maana dalili zote zaonyesha wazi kwamba sehemu kubwa ya mji huu ilikuwa ni maziwa na vijito.

Hivyo ukusanyaji kodi mikoani na wilayani hufanywa kabla ya kuangalia ni asilimia ngapi iende serikali kuu.

Pa kupigania ni kufahamu ni mfumo upi watumiwa kupeleka fedha za mapato serikali kuu.

Ila masuala kama vito vya asili na maliasili kama mafuta ni jukumu la Zanzibar kuhakikisha vyatumika kuchochea maendeleo.
 
Yaani huwaga sielewi hz Habari za Muungano. Nafikiri Wazanxibar wapewe Haki yao, wawe huru, FAIDA ya wao kuwa huru, fursa zitakuwa kubwa sana. Kwa ushirikiano wa kimataifa assume wanapeleka maafisa ubalozi nchi 50, maana yake zaidi ya wazanzibar 200 atakuwa ubalozini, bado kwenye madhirika ya Kimataifa, bado nk. Yaani watakuwa juu sana. Tatizo kuna Viongozi wananufaika sana na Aina hii ya muungano ndio wanaendelea hii hali. Wamejenga zenji, dar na Dodoma. Lkn WANANCHI wa kawaida kwao hakuna jipya lolote. Ngoja tuone kinachoendelea hapo 28/10 ambapo wazanzibar wataamua hatuma yao.
 
Kinachojadiliwa ni kero za muungano kwenye mambo ya muungano sio za Tanganyika au za Zanzibar!!! huelewi?.Umeona hapo wanajadili kero za nchi moja moja? Hapo ni kamati ya mambo ya muungano

"Nchi moja moja"!! Kwani zipo nchi ngapi?
 
Hivi mnafahamu lakini km hoja za Muungano zimepunguzwa Sana. Fwatilieni TBC mujue Mambo makubwa yaliyofanywa ya kupunguza hoja za Muungano


==
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania zimekutana kutia saini makubaliano ya kuondoa hoja tano za Muungano ambazo zimeshapatiwa ufumbuzi

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania zimekutana kupiga saini makubaliano hayo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zunguwa amesema zipo hoja nyingine sita zimeshatatuliwa bado kufikia makubaliano

Zungu ametaja hoja zilizoondolewa ni Ushirikishwaji wa Zanzibar kwenye masuala ya kimataifa na kikanda, Ushiriki wa Zanzibar katika ushiriki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, gharama ya kushusha mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar

Pia utafutaji na uchimbaji wa mafuta ya gesi asilia na utaratibu wa vikao vya kamati ya pamoja serikali ya mapinduzi ya zanzibar na serikali ya muungano ya kushughulikia masuala ya muungano
Kwa 7bu ya uchaguzi?
 
Wakati serikali inahamasisha watu waende kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi mkuu, Chadema walikua wakihamasisha watu wasiende kujiandikisha mpaka ipatikane katiba Mpya Chakushangaza baada ya matokeo kutangazwa watasema wameibiwa kura.
Walitakiwa kususia Uchaguzi Mkuu kama walivyosusia chaguzi za serikali za mitaa.Sababu zilizofanya wasusie chaguzi za serikali za mitaa bado ziko varied hata uchaguzi mkuu huu.
Upinzani wangetumia nguvu nyingi kuilazimisha serikali kutunga katiba mpya kwanza,uchaguzi baadae.
Hata hii 28 October wanaenda kulia tu.
 
Hivi sisi huku bara gas yetu tunachimba wenyewe au ni hao mnaowaita mabeberu ndo wanachimba na kuuza. Najua utabisha ila kaka Bujibuji atakufafanulia hapa manake mie niko songosongo huku naona ni wale mnaowaita mabeberu wako bizee huku lau ningemuona polepole ningeelewa kuwa sasa gas inachimbwa na wazalendo
Swali langu moja tu kwa CCM na Mataga kwa ujumla, Kiko wapi kitalu cha uchimbaji cha TPDC?
 
Mi hata sielewi,,wameondoa hoja tano,kisha wamezipeleka wapi,,mwanzoni hizo hoja zilikuwa zimehefadhiwa wapi na sasa zimepelekwa wapi?.
Ukishapata jibu waulize mwakilishi wa Tanganyika alikuwa nani kwenye hayo mazungumzo?
 
Wakati serikali inahamasisha watu waende kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi mkuu, Chadema walikua wakihamasisha watu wasiende kujiandikisha mpaka ipatikane katiba Mpya Chakushangaza baada ya matokeo kutangazwa watasema wameibiwa kura.
Kwa taarifa yako wapiga kura ni 29m+, nusu ya watanzania wote, kama mlipika data mkitegemea kunajisi box la kura, basi safari hii mmeliwa.
 
Hahahaaa... CCM, CCM,... acha kichaa. Tangu 1964? Leo majuma 2 kuelekea kwenye uchaguzi eti umetatua kero? Anayeiamini CCM kichaa tu - kama Magufuli na Mpina.
kwaiyo kwa sababu tunaelekea kwenye uchaguzi ulitaka mambo yote yasimame ?
 
Back
Top Bottom