CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
===
Msemaji wa IKULU ni mtu muhimu sana kwani ndio mtu wa kwanza kumpaka Rais mafuta mbele ya umma wa Tanzania.
Mkurugenzi wa IKULU Mawasiliano anazungumza badala ya Rais wa nchi hivyo lazima ajue karibu Kila kitu kinachomzunguka Rais Kwa mapana yake.
Kazi ya Mkurugenzi wa IKULU sio kusema tu Rais amekwenda Korea Kwa ziara na kutuma picha NO, Ni zaidi ya hayo.
Mkurugenzi wa IKULU kazi yake ni kuonesha faida ya hiyo ziara kitakwimu , Matumizi na kila faida iliyopatika kitakwimu huku akiwa na rejea mbalimbali za anachokisema.
Msemaji wa IKULU lazima aijue vizuri Tanzania ikiwa ni pamoja na Mila na desturi za Kila kundi,
Msemaji wa IKULU lazima aweze kufanya propaganda vizuri hasa Political Numbers hii hapa lazima aiweze sawa sawa.
Msemaji wa IKULU lazima awe source ya habari nyingi hapa ndani ya nchi na ajue vizuri kuitumia media ya local na internation media.
Msemaji wa IKULU lazima ajifunze kusema uongo Mtakatifu hasa pale anapogundua boss wake kateleza kimatendo au kimaneno.
Msemaji ya IKULU anapashwa kuwa na maarifa zaidi ya Kiuchumi na kisiasa kwani ndio agenda kubwa za Taifa hili.
Huyu David Kafulila pamoja na kwamba sio Msemaji wa IKULU ila anaitetea Serikali kwa kiasi kikubwa
Mtakubaliana na mimi kama kweli tunataka habari za IKULU zipate nguvu mbele ya umma wa Watanzania hakuna namna tutamkwepa Kafulila kwa sasa.
Kwa mtazamo wangu Kafulila ndio kijana pekee asiye Mbunge Wala Waziri anayeweza kuwa Msemaji wa IKULU kwa wakati huu ili kuifanya IKULU kutoka kuwa reporter wa habari mpaka kuwa source wa habari.