Ikulu sasa ni BMW kwa kwenda mbele

Status
Not open for further replies.

Kazi kweli kweli...sasa hawa viongozi wetu wana tofauti gani na Mangungo wa Msovero?
 
Kazi kweli kweli...sasa hawa viongozi wetu wana tofauti gani na Mangungo wa Msovero?

Ndugu, Mangungo wa Msovere alikuwa na nafuu sana tu, kwani yeye alikua hakupiga kitabu kama hawa wazee, hawa wamepiga na ma-economics lakini waapi! vichwa vigumu. Sijui tutajikomboaje kifikra waafrika?!
 
Hapa patamu sana..

Kwa hiyo hawa waarabu ktk yooote wamepima wameona Tz tuna upungufu wa magari ya msafara wa Rais? Wajameni huu ni uungwana kweli?
 
Watu wa matawi ya juu wanatudhibitishia kuwepo kwao out of touch kabisa.

Juzi tu hapa marekani ma CEO wa makampuni ya magari hapa waliitwa kwenye mahojiano na congress hapa na kila mmoja wao akaenda na ndege binafsi...Wakaulizwa ni kwanini hawakutumia akili hata wakapanda ndege moja wote?

Uchumi uko hoi na matajiri ama serikali kubwa zinafikiria namna ya kupunguza matumizi makubwa ya kifahari...Lakini sisi ambao wananchi wetu wamekuwa masikini kwa muda wote bado tunafanya kinyume.

Sijui nimlaumu mtoa zawadi ama mpokea zawadi...Lakini unaweza kuona kuwa wale wanaojiita wafadhili wanawajali na kuwalinda watawala kwasababu wanajuwa watawala hao ndiyo wenye nguvu na si wananchi.....Ni hadi hapo waafrika tutakapogeuza kibao na kufanya the opposite...Kwamba kama unataka urafiki na sisi basi sisi THE PEOPLE ndio wenye nguvu....Kwanini hawakusaidia masikini na badala yake wanadai eti ni usalama wa Rais?

Hao waarabu ndio wanahakikisha usalama wa rais kwa kuwaambia usalama wa Taifa kuwa BMW za Ghadafi ndiyo zenye usalama zaidi?

Hapo ni kama ni kweli zimetolewa kama msaada....Kama zimenunuliwa na jasho la mwananchi....Then kula uliwe itaigeuka serikali ya ccm kwani kama wakiwala wananchi kihivyo basi na wao wasishangae wakiliwa kwa kutoswa na wananchi.
Kweli ni kama mazingaombwe.
 
Lazima kuna cha juu hapo. Watu wamekaa chini, wametafuta pa kutokea, wakaamua kubadilisha magari ya msafara wa Rais.

Nadhani Ikulu yetu imevamiwa na wabaingaizaji. JK akae chonjo anaingizwa mkenge ambao kujinasua haitawezekana; sidhani kama kuna utafiti umefanyika kujua uimara wa magari hayo.

Isijekuwa kama lile Benz la Ikulu ya Zanzibar wakati wa Komandoo!
 

Wananchi waliwahi kudanganywa kuwa pesa za Meremeta haziwezi kujadiliwa kwa sababu zilihusika na mambo ya Usalama wa Taifa. Lakini ukweli ni kwamba yote yaliyofanyika under Meremeta ulikuwa ni UFISADI ULIOKUBUHU. Naona kuna mbinu mpya ya UFISADI nayo ni kutumia Usalama wa nchi, Rais. What about USALAMA wa AFYA na MAISHA ya Watanzania wengine???????? Je kamati ya Bunge ya Usalama ilijua haya????? Tusikubali kuingizwa mkenge kila wakati kwa kutumia mgongo wa Usalama.
 
Jamani;

Naomba muwe wapole. BMW ni za msaada. Huyu mwandishi alistahili kuchunguza kwanza kabla ya kuhitimisha na kutaja ma bei.

FP

.....mmmhhhh........msaada!!!......kutokea wapi aisee?
 
Msaada mpaka magari ya rais? Wakiyawekea vi bug katika ma espionage moves je?
 
Wakuu, hapa tunachemsha,

Maana mpaka sasa hakuna, alietaja exact specifications na capabilities za hizo gari vis a vis bei yake. Zile gari sio za JMK kama JMK, ni za ulinzi wa rais wa JMT.

Rais wa JMT kununuliwa BMW 5 kwa ajili ya usalama wa msafara wake nayo tunafanya nongwa?...Say zimecost 1bn haya, hivi taasisi ya urais tunaichukuliaje?

Hapohapo tunamtaka apambane na mafisadi mamafia kama kina Jeetu Patel, Y. Manji na RA,... Hapohapo tulishangilia alipomtosa mshkaji wake mzee wa ten percent EL, halafu inapokuja kwenye kuimarisha ulinzi wake, tunalalamika tena...

Mzee Icadon kule kwenye thread ya ulinzi wa viongozi amelichambua vizuri BMW X5(special purpose) na capabilities zake wakati wa hekaheka za kuokoa maisha ya VIPs kama msafara ukivamiwa na maharamia...

Ifike mahali tupime kidogo kabla ya kulalamikia KILA kitu.... IT DOESNT MAKE SENSE SOMETIMES!... Kwa hili hapana as tunabank kwenye kuangalia mtu badala ya issue.
 
Hii ni aibu ya karne. Usalama (eneo la usafiri) wa kiongozi mkuu wa nchi unakuwa monitored remotely na waarabu!
 
Mpaka sasa naona mauza uza tuu mara msaada kutoka Libya mwingine anasema kutoka Saudi Arabia, mwandishi wa hii habari si angepiga japo simu kwa huyo dealer waliyenunua.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa gari hizo ziliingizwa nchini kwa ndege kutoka Afrika Kusini na kwamba, lengo la kuhama Mercedes Benz ni kuimarisha zaidi usalama wa rais na msafara wake. Habari kamili
 

Baiskeli ya kipepe.
 

Read "Confessions of an Economic Hitman" by John Perkins ..eti bure!
 
Msaada huu wa magari una masharti gani? Kuna sharti la kuzuia magari hayo yasiuzwe kwa mabilionea wa ndani ama nje ya nchi na fedha zikatumika kwa shughuli zingine za maendeleo? Kama ilivyoripotiwa, Rais alishakataa yasinunuliwe. Ni busara kuheshimu maamuzi ya Rais, tuwashukuru waliotoa msaada na baada ya hapo yapigwe bei! Kiusalama kama Rais aliweza kutumia Benz zenye nyenzo za kiusalama na hakuna jambo lililoharibika, BMW za nini yarabi?
 
Mkuu Icadon,

Kwenye masuala haya nakukubali sana tu. Hebu tupe ushauri, ni gari gani la gharama nafuu linaweza kumfaa rais wetu? Be frank, kama hawajakosea tusiwabebeshe mzigo wa lawama bure


Thomas Sankara alitumia VW yake aliyokuwa nayo kabla ya kupindua nchi. Wote tunajua yaliyompata!
 
Thomas Sankara alitumia VW yake aliyokuwa nayo kabla ya kupindua nchi. Wote tunajua yaliyompata!
FM,
Lakini Sankara aliuawa na rafiki yake wa karibu. It was an inside job. Hata kama angekuwa anatumia kifaru cha kijeshi Compaore angemtaimu tu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…