Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
More or less the same..ila wataalamu wanasema Benz ni bora zaidi.
Ebana hivi Chancellor wa Ujerumani anatumia gari gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
More or less the same..ila wataalamu wanasema Benz ni bora zaidi.
Ebana hivi Chancellor wa Ujerumani anatumia gari gani?
Mkuu hiyo ni bei gani hiyo?
Inaweza ikawa ghari sana kuliko zetu hizi?
Sober argument yako nzuri.Wakuu, hapa tunachemsha,
Maana mpaka sasa hakuna, alietaja exact specifications na capabilities za hizo gari vis a vis bei yake. Zile gari sio za JMK kama JMK, ni za ulinzi wa rais wa JMT.
Rais wa JMT kununuliwa BMW 5 kwa ajili ya usalama wa msafara wake nayo tunafanya nongwa?...Say zimecost 1bn haya, hivi taasisi ya urais tunaichukuliaje?
Hapohapo tunamtaka apambane na mafisadi mamafia kama kina Jeetu Patel, Y. Manji na RA,... Hapohapo tulishangilia alipomtosa mshkaji wake mzee wa ten percent EL, halafu inapokuja kwenye kuimarisha ulinzi wake, tunalalamika tena...
Mzee Icadon kule kwenye thread ya ulinzi wa viongozi amelichambua vizuri BMW X5(special purpose) na capabilities zake wakati wa hekaheka za kuokoa maisha ya VIPs kama msafara ukivamiwa na maharamia...
Ifike mahali tupime kidogo kabla ya kulalamikia KILA kitu.... IT DOESNT MAKE SENSE SOMETIMES!... Kwa hili hapana as tunabank kwenye kuangalia mtu badala ya issue.
Kumbe wenzetu kiongozi analipa kodi kwenye nyumba ya serikali!Huyo chancellor aliyepita (Shroeder) aligoma pia kuishi kwenye nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya chancellor akidai inastahili matajiri na kwamba yeye na mshahara wake hataweza kulipa kodi.
...😀 te he he, "kula uliwe!"
Mkuu hiyo ni bei gani hiyo?
Inaweza ikawa ghari sana kuliko zetu hizi?
Audi zinatumia engine ya VW. Hivyo haina tofauti na VW. Ni gari za kati ndiyo maana aliamua kutumia.
Aligoma kutumia benz au bmw akidai ni gari za kifahari kwa ajili ya watu wenye pesa.
Huyo chancellor aliyepita (Shroeder) aligoma pia kuishi kwenye nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya chancellor akidai inastahili matajiri na kwamba yeye na mshahara wake hataweza kulipa kodi.
Mazee...sidhani kama Benz Ujerumani iko regarded kama ni gari ya kifahari maana taxi (cab) zao nyingi ni Benz. Kama mtu hujawahi kupanda Benz na ukapata bahati ya kwenda Ujerumani....basi kodi taxi na utaendeshwa kwenye Benz...
Sober argument yako nzuri.
Umenifanya nikarinie bubu na argument yako.Inanifanya kwa shingo upande nikubali ununuzi wa hayo magari.Labda niongezee.
Ulinzi wa Raisi ni kazi ya wananchi wote si kazi ya magari na ma-bouncer wale wanaotembea na Raisi pekee..Ndiyo maana Raisi akipendwa sana na wananchi Ulinzi huwa mdogo sana.Maana hakuna hitman wa hit and run fast aweza thubutu kujaribu kumshambulia Raisi iwe kwa jiwe au kombora.Raisi apendwaye sana na wananchi anakuwa ni high risk target kwa wazoefu wa hit and run maana waweza jikuta wananchi wampendao Raisi wao wanawakimbiza kama mbwa bila kujali silaha walizonazo wakijaribu ku-hit raisi wao mpendwa.
Ndiyo maana Raisi yeyote ambaye hutaka kuimarisha ulinzi wake kitu kimoja akifanyacho huwa ni kuwa mchapa kazi anayejali wananchi na huchagua wasaidizi wazuri wachapa kazi wazuri wanaosimamia maslahi ya wananchi ili wananchi wampende Raisi wao na wawe tayari kumlinda na kumtetea popote alipo.Ukiwachagua wasaidizi wabaya,wanafiki na wapotoshaji na wasiokuwa wachapa kazi ina maana taasisi ya Raisi itadharaulika na watu wahuni watataka kichwa cha Raisi na gharama za kumlinda zitaenda juu sana.Gharama za kumlinda Raisi asiyependwa na wananchi ni kubwa mno.Kwa ufupi ni hatari kumlinda raisi asiyependwa.Mlinzi hulali hupumziki na saa yoyote waweza jambishwa cheche na wananchi wasiompenda Raisi asiyesimamia maslahi yao.
Raisi Nyerere alikuwa kabla ya kutembelea mahali alikuwa anatuma advance team ya wasaidizi wake wa karibu muda mrefu kabla ya ziara zake.Lengo kuu la advance team hizo lilikuwa si kutathmini hali ya ulinzi na usalama wake tu kule aendako bali sehemu kubwa ilikuwa kutathmini utendaji wa watendaji aliowateua kule aujue kama utendaji wao unafanya apendwe au achukiwe na kuangalia kama kweli wanatekeleza kwa vitendo yale yaliyoagizwa.Akijua kuwa utendaji wao kule ni wa mashaka alikuwa akibadilisha uongozi kule kabla hajatembelea hapo aendapo.Akiwasili anaanza kucheka na kuwaambia wananchi nimewaletea kijana mwingine mchapa kazi hapa hivyo hasira za wananchi zinakuwa zimeisha afikapo kule na wananchi humshangilia mno.Sio wanashangilia hotuba hasa bali wanashangilia yale mabadiliko aliyofanya.
Kitendo cha Raisi kushambuliwa mfano na mawe kule Mbeya ni ishara tosha kuwa advance team za Kikwete zina walakini.Hazikutoa feedback nzuri ya watendaji kule au emotions za wananchi kuhusiana na utendaji wa Rasi.Si kitu tu cha kulaumu wananchi wa kule,polisi au walinzi wa msafara wa Kikwete.Yawezekana kabisa watendaji wa kule aliowateua Kikwete ni bogus hawakidhi matarajio ya wananchi hivyo wananchi wakaona walipize kisasi kwake.Naiomba serikali iwaachie huru wale waliorusha mawe iwashugulikie watendaji ambao hawakukidhi matarajio ya wananchi kiasi cha kufanya Raisi atupiwe mawe.
Sasa hivi advance team hivi kazi yao ni nini sasa hivi? Raisi hadi inafikia kwenye mkutano wa hadhara azomewe kaa chizi halafu hadi anafikia hatua ya kuuliza mnanizomea mimi au huyu kiongozi niliyemsimamisha? Hivi vitu Ilibidi wasaidizi na Raisi waelewe mapema waviwekee mkakati pamoja na Raisi mwenyewe kabla ya kutembelea hilo eneo wajue kama kuna mzembe wamtimue wambadilishe kabla ya Raisi kutua pale badala ya Raisi kufika pale halafu anazomewa mfululizo yeye na watendaji wake wakati watendaji ndio wanasababisha mara ingine azomewe.
Ili ulinzi wa Raisi uwe imara unahitaji ushirikiano wa kila upande Raisi achape kazi vizuri,wasaidizi wake ateue wazuri wachapa kazi wazuri na walinzi wake na advance team zake ziwe nzuri za watu wenye akili sana na serious wenye kutoa feedback nzuri za ukweli na uhakika kuhusu utendaji wa serikali kila eneo.Kazi za advance team zisiwe kutafuta nani haipendi serikali au Raisi bali kiongozi gani nani hatekelezi kazi sawasawa na maagizo ya serikali anayefanya serikali na Raisi achukiwe na wananchi kwa utendaji mbovu.Serikali iache kuwa kali kwa wananchi iwe kali kwa watendaji wasiofikia malengo na viwango vinavyotakiwa na wananchi.Kwa kufanya hivyo ulinzi wa Raisi utakuwa imara zaidi.
Mazee...sidhani kama Benz Ujerumani iko regarded kama ni gari ya kifahari maana taxi (cab) zao nyingi ni Benz. Kama mtu hujawahi kupanda Benz na ukapata bahati ya kwenda Ujerumani....basi kodi taxi na utaendeshwa kwenye Benz...
Benzi ni gari la kifahari. Na Benzi ziko model nyingi. Hivyo ufahari unatokana na model.
Marekani, Tanzania, na nchi nyingi wanatumia magari ya zamani kama taxi.
Kuna nchi taxi ni sehemu ya utalii. Hiyo huwezi kuchukua gari kutoka junk yard na kulitumia katika biashara ya taxi. Na vilevile kutumia Benz kama taxi ni sehemu ya promotion ya magari.
Na kihistoria. Benz ilipoanza ni watu wachache na matajiri walioweza kununua magari. Hivyo biashara yao ilikuwa Taxi. Hivyo toka mwanzo wa magari, Benz ilitumika kama taxi.