Ni bahati nzuri kuwa uongozi hautegemei miguu na mapafu bali utimamu wa akili na uwezo wa kupambanua mambo na kufanya maamuzi sahihi. Kama ingekuwa kukimbia ndiyo kigezo sidhani kama katika wote walioko madarakani kama kuna ambaye angestahili kukaa kwenye nafasi yoyote ile, haswa kwa sababu wengi wao ni wagonjwa. Kwa hiyo kama utaliangalia hilo kwa mapana stahiki ni wazi aliyelizungumza amekurupuka tu, ni mropokaji wa kawaida au ana uelewa mdogo wa kuchanganua mambo hasa kutokana na uwezo wake wa kufikiri na kufanya upembuzi yakinifu. Kwa hiyo ningeshauri kauli kama hizo ZIPUUZWE TU.
Pia siyo vizuri kulifumbia macho tatizo la uongozi wa sasa ambapo nchi ina-colapse kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Mifano ichukuliwe kwenye elimu na sera yake, Uchumi wetu na hali ya sarafu ya taifa, hali ya vipato vya wananchi na bei za bidhaa! hii ni sawa na kusema hata hao mnaofikiri wako sawa kuongoza wamefeli.
Wamefeli labda ni kwa sababu pamoja na uwezo wao wa kukimbia "marathon nyingi" lakini wana afya dhaifu za roho na nafsi kiasi cha kuangalia anguko la taifa huku wakijitia hawajali na haiwaumi. Au ni kwa sababu wana maradhi ya kushindwa kutoa maamuzi yenye tija kwa ustawi wa taifa. Au pengine ni kwa sababu nchi yetu imejulikana sana kama shamba la bibi na kumekuwa hakuna nia ya dhati ya kukomesha uzembe, wizi na kukosekana kwa uadilifu miongoni mwa viongozi na wananchi kwa ujumla!
Vyovyote vile kila anayeangalia hali ilivyo, kama na yeye siyo mgojwa wa akili au mvivu wa kufikiri, ni wazi ataona kuwa kwa tulipofikia, ili Tanzania inayokalika iendelee kuwepo hakuna jinsi zaidi ya kubadilisha uongozi tulionao. Na msiniambie ---- ya Upinzani hauwezi kwa sababu wananchi wanastahili ustawi regardless ni nani ameusababisha.