IKULU Ubia upo, tuwajue wabia -Jenerali

IKULU Ubia upo, tuwajue wabia -Jenerali

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
614

Ubia upo, tuwajue wabia

Jenerali Ulimwengu
Julai 15, 2009

(Baada ya kuomboleza hasara kubwa iliyotupata kutokana na kifo cha ghafla cha Haroub Othman, sasa tuendelee na hoja yetu).

Katika makala ya mwisho nilijadili jinsi ambavyo watawala wetu wamekumbwa na kile nilichokiita ‘mbano wa zama’ (time warp) unaowafanya waamini kwamba wanaweza kutenda kama Mwalimu Nyerere katika utawala wake, bila hata hivyo kufuata nyayo za Nyerere katika masuala makuu aliyoyasimamia.

Dalili mojawapo ya kile nilichokiita u-Nyerere-nusu ni yale matamshi niliyowahi kuyasikia mara tatu kutoka kwa watawala wetu wakuu. Mara ya kwanza niliyasikia kutoka kwa Rais Benjamin Mkapa, na mara ya pili nimeyasikia kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete: “Urais Wangu Hauna Ubia.”

Ukitazamwa kwa haraka msemo huu hauna tatizo. Ni kweli kwamba raia wa Tanzania wanapomchagua mtu kuwa rais wao hawataraji kwamba ataingia ubia na mtu mwingine ambaye kwa hakika watakuwa hawamjui. Katika mpangilio wa kikatiba, labda ni makamu wa rais ndiye anaweza kuonekana kama mbia kwa maana alikuwa ‘mgombea mwenza,’ na ‘mwenza’ ni aina ya mbia.

Isitoshe, kama ambavyo nilikwisha kuonyesha huko nyuma, Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inamfanya Rais wa Jamhuri kuwa na madaraka makubwa kiasi kwamba mawaziri ni kama watumishi wake, washauri wasiokuwa na uwezo wa kuamua jambo lo lote isipokuwa kwa kuelekezwa na Rais. Anaweza kufanya lo lote: kumfukuza ye yote kati ya mawaziri wake (Rais Mwinyi alifukuza baraza zima mwaka 1990); kubadilisha majina na miundo ya wizara; kuamua wizara gani ifanye nini na nini isifanye… na kadhalika.

Mbali na baraza la mawaziri, Rais anaweza kukataa kutia saini muswada wa sheria, na akikataa unabaki kuwa muswada tu, na anaweza kuvunja Bunge katika mazingira fulani. (Kwa njia fulani ambayo si rahisi kuielewa Rais pia ni sehemu, nusu, ya Bunge!)

Pia ndiye anayeteua msururu mrefu wa watendaji na wakuu wa watawala kutoka ngazi ya Taifa hadi wilayani, hata kama mara nyingi jina lake linatumiwa na wajanja kujipachikia watu wao halafu wananchi wanaambiwa, “Rais kamteua” fulani.

Yote haya, na mengine mengi sana, yanadhihirisha ukweli ule, kwamba rais wetu hana mbia; yeye ndiye Bwana Mkubwa, Alfa na Omega nchini. Huo ndio ukweli.

Lakini si ukweli wa kusherehekea, wala si jambo la kujivunia. Ni jambo la kutafakari kama tatizo na kulitafutia ufumbuzi, baada ya kutambua madhara yake. Nilikwisha kueleza katika makala zilizotangulia kwamba mpangilio tulo nao ni ule tulioachiwa wakati tunapata Uhuru wa Tanganyika, na kwa kiasi kikubwa ni utaratibu uliowekwa na Waingereza.

Leo hii hautufai tena. Wala tusijidanganye kwa kusema kwamba tumekuwa tukifanya marekebisho ya Katiba ya mara kwa mara na kuweka sawa yote yaliyotakiwa kuwekwa sawa (viraka vinavyozungumziwa). Hili si kweli kwa sababu masuala ya kimsingi ya falsafa na nadharia ya utawala bora hayajaguswa, na mojawapo linalojitokeza ni hili linalosikika kama “Urais Wangu Hauna Ubia.”

Haiwezekani kuendesha nchi kubwa kama Tanzania, kubwa kwa eneo, kubwa kwa wingi wa watu na kubwa kwa wingi na ugumu na uzito wa matatizo, bila ubia. Haiwezekani kumrundikia mtu mmoja madaraka ya kila aina na katika ngazi zote nchini halafu ukamwacha afanye kazi zake bila ubia.

Hivi, hata chama chake kilichomweka madarakani hana ubia nacho? Ni kweli, najua, na nimekwisha kulijadili, dhana ya chama katika nchi zetu haina maana kubwa, na chama kimebakia ni chombo cha kuvukia (aina ya pantoni) kwenda kwenye madaraka ya dola, basi. Lakini si ungelidhani kwamba hilo ni tatizo la kutatuliwa na si jambo la kujigamba nalo?

Kila mtu anayetaraji kufanya kazi kubwa, kwa mfano ya kuendesha nchi kama hii, atahitaji kuwa na wabia wengi, tena wabia makini, kama anataka kufanikisha kazi yake. Aidha ni bora ubia huo na wabia hao wakajulikana wazi, na ikajulikana ubia huo umeundwa ili ufanikishe shughuli gani.

Hili lisipofanyika kwa uwazi, na kama kauli itaendelea kuwa ile ile ya “Sina Ubia na Mtu” tutakuwa tunapigwa “changa la macho” ili tusijue ni nini kinaendelea, kwa sababu ubia utakuwapo tu, tutake tusitake. Ni kwamba utakuwa ni ubia uliojengeka kizani na unaoendelezwa kwa kificho, lakini ubia utakuwapo.

Wananchi hawataweza kujua kwa uhakika ubia huo ni wa mtawala wao na watu gani, na mara nyingi watakuwa wakipashana habari hizo kwa minong’ono, uvumi, tetesi na umbeya.

Kwa mfano Rais atafanya jambo linaloonekana jipya na la kushangaza kidogo, labda likiwa linatoa maslahi na faida kwa kundi fulani la raia. Ili kueleza ni kwa nini Rais wao kafanya hivyo, raia wanaweza kuanza kuunganisha kitendo cha mtawala wao na uhusiano wa ki-ukwe uliopo kati yake na familia fulani, au urafiki wa utotoni na mtu fulani, au kitu cho chote kingine wanachoweza kukikisia na kukifanyia hesabu za “mbili ongeza mbili”.

Haya ninayoyasema hapa si mambo ya kudhania tu, wala sikuyaota; yametokea hapa hapa nchini, na mfuatiliaji wa masuala haya atayatambua. Wakati Mwalimu Nyerere anasema, katika miaka ya 1990, kwamba kiongozi asiwe mtu wa kulala kitandani na mkewe, na mkewe akamnong’oneza neno, na kesho yake neno hilo likawa ni sera ya serikali, alikuwa analizungumzia hili ninalolisema.

Najua wako watu waliodhani kwamba Mwalimu alikuwa akimsema mrithi wake aliyekuwa madarakani wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, lakini binafsi naamini alikuwa anajaribu kueleza maamuzi yanayofanyika kutokana na mchakato usiokuwa rasmi, uwe ni kati ya mume na mke, ndugu na ndugu, rafiki na rafiki, shemeji na shemeji, mkwe na mkwe, au “mshikaji” na “mshikaji.”

Muhimu kutambua hapa ni kwamba katika mzingira yetu, mtawala amelimbikiziwa majukumu mengi ambayo yeye peke yake hawezi kuyamudu. Aidha, kwa jinsi mambo yalivyo, ni kwamba yeye ndiye Qasim, mgawaji wa riziki kwa kugawa nafasi za ajira nono, na wakati mwingine kuamua nani apate kandarasi nono na nani aruhusiwe kufanya biashara kubwa.

Tunalo kabila kubwa sana la watu ambao maisha yao yote yamekuwa ni ya kutegemea kuajiriwa katika nafasi za serikali, mashirika yake au ndani ya chama-tawala. Hawa wote wanalazimika kujiwekea mazingira ya kukubalika na kupendeka kwa Bwana Mkubwa siku zote, na ikiwa wanaweza kuunga urafiki na watu wanaodhaniwa kwamba ndio “washikaji” wa Mkubwa, watafanya hivyo.

Kati ya wasaka vyeo na wasaka kandarasi na wale wanaodhaniwa kwamba wako karibu na kiti cha enzi, kimezuka kiwanda cha mahusiano ya kifisadi ambacho ndicho kinachukua nafasi ya asasi za uongozi wa nchi.

Hali hii inakuwa haiepukiki katika mazingira ambamo asasi kama chama cha siasa kinachojiita chama tawala hakina nguvu za kifalsafa, kiitikadi wala kisiasa kuweza kuisimamia serikali au kumwelekeza Bwana Mkubwa katika kazi yake.

Unapowadia wakati wa uchaguzi, kiwanda hiki kinaingia katika gia kubwa kuhakikisha kwamba Bwana Mkubwa, chama chake na watu “wake” wanabakia, au wanaingia, madarakani. Zinakusanywa fedha kutoka kila mahali isipokuwa kule kunakokubalika kihalali.

Kwa kuwa hakuna ubia unaokubalika kwamba upo, na ubia uliopo ni wa kificho, ukusanyaji wa fedha za kampeni unafanyika, kama mambo mengine, katika kificho, na wananchi hawelewi vyema ni wapi fedha hizo zimetoka, ni akina nani waliochanga na maslahi yao ni yapi katika uchangaji huo.

Haya nayo sikuyazua, ni mambo yanayojulikana na ambayo yatatuathiri kwa muda mrefu ujao. Neno la Kiingereza 'opacity’linaeleza dhana yangu ya msingi, kwamba kila kitu ni opaquemambo mengi yanaendeshwa katika kiza, na ni machache mno yanayoonekana kwa uwazi.

Msomaji akirudi nyuma kidogo atakumbuka nilivyoelezea watu wanaoingia katika serikali, tuseme Baraza la Mawaziri, kwa sababu wanatakiwa “wamsaidie” Rais katika kuendesha nchi. Itakumbukwa vile vile nilivyoeleza jinsi wanavyojitahidi sana kutokuwa na fikra zao, na badala yake wanasubiri busara za Bwana Mkubwa, na wao wanakuwa watekelezaji - aina fulani ya matarishi.

Haya ndiyo matunda ya “Urais Wangu Hauna Ubia,” na matokeao yake ni serikali kukosa mwelekeo, kuhaha kila siku toka jambo moja hadi jingine, na hatimaye kumfanya mtawala anayeondoka madarakani kuondoka na kila kitu alichokuwa akikisimamia (kama alikuwa nacho) wakati akiwa madarakani. Ndiyo yaliyotokea kwa Nyerere (yeye alikuwa nacho), na ndivyo yatakavyotokea kwa wengine waliomfuata.

Wakati tukisubiri hayo kujidhihirisha, wale wanaopewa angalau vijinafasi vya ‘uongozi’ watakuwa wanahangaika kwa nguvu zao zote kutengeneza viota vyao, kukusanya fedha za kampeni zijazo, kujenga majumba, kununua magari, mashamba na hisa za makampuni na kupokea rushwa kushoto, kulia na kati, yote hayo wakitumia nafasi walizopewa katika utawala. Hapo hakuna tumaini la kujenga uongozi wa aina yo yote; tunachojenga ni kundi la watu, kabila zima, watu wanaoishi kwa ajili ya leo.

Haishangazi, basi, kwamba hakuna jambo linaloashiria uendelevu. Sana sana watawala wetu wakitaka kuangalia mbali, hawaendi zaidi ya miaka iliyosalia kabla ya uchaguzi ujao. Januari 2006 ilibaki miaka mitano; leo imebaki miezi 18. Huo ndio upeo.

Wala haishangazi kwamba tunazidi kushuhudia jinsi umasikini unavyozidi kuwatesa watu wetu. Pasipokuwa na ubia wa wazi, hakuna njama inayodumu ya kuleta maendeleo, na badala yake kila mmoja anatafuta maslahi yake ya muda mfupi. Pale panapokuwa na dalili ya ubia, unakuwa ni ubia wa ‘kiushikaji’, na huu hauendi masafa marefu, kwani kinachofanyika ni kunyakua, kukwapua, kunyofoa kila kinachoonekana kuwa na maslahi ya sasa hivi.

Hivyo sivyo mataifa yanavyoendelea.

Itaendelea

jenerali@gmail.com

Source: Ubia upo, tuwajue wabia
 
Last edited by a moderator:
Sasa hapa itakuwa kutafuna ugomvi; mwenye kigoda kasema hana ubia.. Jenerali anasema anao.. well.. something got to give!
 
Sina tatizo na Wabia hata kama wapo. Issue hapa je hao wabia wanatupeleka wapi? Kama ni wabia wazalendo, basi haina shida lakini kama ni wabia wafisadi, then what is the point?

Mwalimu kuna watu aliwaheshimu na mpaka anafariki walikuwa ni marafiki wa karibu kama akina Kawawa, Malecela n.k. lakini urafiki huo haukufanya asimpangie kazi "yoyote" Rashidi au asimtungie Kitabu Malecela.
 
Scholarship in the tradition of Haroub Othman. Kikwete alivyosema hana ubia originally nili raise swala hili alilosema Ulimwengu, kwamba je hiki ni kitu cha kujivunia? Wakati wenzetu wanajaribu kuficha nguvu zisizo kiasi za marais sisi rais wetu anajigamba nazo? Kweli tuna demokrasia iliyokomaa?
 
Sina tatizo na Wabia hata kama wapo. Issue hapa je hao wabia wanatupeleka wapi? Kama ni wabia wazalendo, basi haina shida lakini kama ni wabia wafisadi, then what is the point?

Mwalimu kuna watu aliwaheshimu na mpaka anafariki walikuwa ni marafiki wa karibu kama akina Kawawa, Malecela n.k. lakini urafiki huo haukufanya asimpangie kazi "yoyote" Rashidi au asimtungie Kitabu Malecela.

Actually rais anatakiwa awe na wabia, wabia wenye national interests at heart. Ndiyo maana nchi zenye demokrasia iliyokomaa kama Marekani au Uingereza huwezi kumsikia rais au Waziri Mkuu akisema "uongozi wangu hauna mbia", itakuwa hubris itakayoleta political suicide.

Kikwete anaonekana kutoelewa kuwa urais si rais, urais (the presidency) is an institution far and beyond rais (the person).Inaonekana kama Kikwete anafikiri urais na rais ni kitu kimoja.

Yaani Kikwete mwenyewe aliona ana project independence na positive incorrigibility kumbe anachemsha.

Lazima tuwe humble.
 
Sasa hapa itakuwa kutafuna ugomvi; mwenye kigoda kasema hana ubia.. Jenerali anasema anao.. well.. something got to give!

-Tatizo la Jenerali ni credibility, hata na yeye alishakuwa mbia wa Mwalimu, Mkapa na Miwnyi, hakuwa na kelele mpaka walipomuweka pembeni na mlo ndio sasa anajua tatizo la ubia wa mlo na viongozi wa juu.

- Uongozi wa Mwalimu pia ulikuwa na ubia na kina Bomani, Kahama, na Rupia, ulianzia na wazazi wao na ukahamia kwa watoto wao, akamshambulia Kawawa na kumtungia kitabu Malecela ili atuachie Mkapa Mr. Clean.

- Mwinyi, Mkapa, na sasa Kikwete wote ni wanafunzi wa Mwalimu, lets say hawakuwa wabia wake kiuongozi, je walikuwa what? Lini Wa-Tanzania tutazinduka na kukubali kwamba toka uhuru wetu tumekua tukiongozwa na viongozi wasiokuwa na sound vision inayofaa kwa taifa letu, na kwamba hatukufika hapa tulipo kwa bahati mbaya ila ni sababu ya uongozi mbovu na uliooza na ni regardless ya who was kiongozi, Mwalimu alikuwa better kidogo kuliko wengine lakini ukweli unabaki pale pale kwamba viongozi wote tulionao leo ni wabia wake Mwalimu, historia haiwezi kupindishwa maana tupo tuliokuwepo na bado tupo na kuyaona ya sasa.

- Taifa halizalishi viongozi wabovu in 24 years tu na wala hatuna kiongozi wa juu na fisadi mwenye miaka 24 yaani toka Mwalimu alipoacha uongozi, na si kweli kwamba walianza ufisadi baada tu ya Mwalimu kuondoka, lakini huko nyuma walikuwa clean, ubia wa uongozi haukuanza leo that is my point umekuwepo na utaendelea kuwepo, labda as a nation tuamue kisheria ni ubia gani unafaa na upi haufai kwa masilahi ya taifa na ni lazima tuangalie tulianzia wapi badala ya kujaribu kupindisha ukweli maana tutaishia kupata results zilizopinda na kuzunguka pale pale kama tunavyofanya sasa, kwa sababu kuna tunaomini kwamba Mwalimu alikuwa malaika.

Respect.

Kamanda FMEs!
 
got it! ufisadi wa watawala wetu leo hii unatokana na ubia wao na ufisadi wa Mwalimu! straight to the point. Easy to understand.
 
Mwalimu kuna watu aliwaheshimu na mpaka anafariki walikuwa ni marafiki wa karibu kama akina Kawawa, Malecela n.k. lakini urafiki huo haukufanya asimpangie kazi "yoyote" Rashidi au asimtungie Kitabu Malecela.

- I know hapa si amewekwa as the role model wa ubia na uongozi, ndio nasema hivi ni kiongozi gani wa juu bongo leo mwenye umri wa miaka 24 maana peke yake ndiye mwenye justification ya kuwa anything he or she is as a leader.

Respect.

Kamanda FMEs
 
- I know hapa si amewekwa as the role model au

Respect.

Kamanda FMEs

nimesoma hiyo.. but in the light of your post ina maana hakuna mtu aliyekuwa rafiki au karibu na Mwalimu ambaye alisalimika na ubia wa ufisadi wake. WOTE wameambukizwa uongozi mbovu toka kwa Nyerere. Ndioy maamiaka 24 baadaye viongozi wote waliokuwa wanafunzi wa Mwalimu wanaonesha dalili zile zile za ubia na mwalimu.
 
Ili tuweze kuachana na uongozi mbovu ambao chanzo chake ni ubia wa Mwalimu inatubidi sasa tutizame elsewhere kutafuta uongozi mzuri ambao hautakuwa na uhusiao wa kiubia na Mwalimu.Tuachane na chama cha CCM cha ubia wa Mwalimu.
 
Well, aliyosema Ulimwengu ni maneno muafaka kwa si-hasa zetu za kibongo. La maana ni kujiuliza mpaka lini tutaendelea na rais mungu- mtu? Ulimwengu kuwa mbia wa Nyerere si dhambi na at least mambo wakati huo yalikua si mbof mbof kama sasa. Nchi za wenzetu ktk chaguzi timu-wabia wa upngozi hufahamika wazi na misimamo yao lakini si hapa bongo uteuzi wa kishkaji a nifae kwa mvua nami nikufae kwa jua. 4me we still have a loooooooong way to go.
 
Actually rais anatakiwa awe na wabia, wabia wenye national interests at heart. Ndiyo maana nchi zenye demokrasia iliyokomaa kama Marekani au Uingereza huwezi kumsikia rais au Waziri Mkuu akisema "uongozi wangu hauna mbia", itakuwa hubris itakayoleta political suicide.

Kikwete anaonekana kutoelewa kuwa urais si rais, urais (the presidency) is an institution far and beyond rais (the person).Inaonekana kama Kikwete anafikiri urais na rais ni kitu kimoja.

Yaani Kikwete mwenyewe aliona ana project independence na positive incorrigibility kumbe anachemsha.

Lazima tuwe humble.

Mkuu, hii uliyo andika ni moja ya sababu kubwa sana zinazodidimiza Africa kwa ujumla. Hii ni kitu ambayo iko kama imekuwa wired vichwani mwa waafrika. Mentality ya kuwa watawala. Title au rank ya mtu pahala katika institution inamfanya afikirie kuwa yeye ndiye hiyo institution. Ile slogan ya Nyani Ngabu somewhat huwa inaelekea ku-describe hii phenomenon miongoni mwa waafrika wengi. Hulka za utawala tawala zimetujaa popote tulipo, si pale tunapomiliki mali zetu binafsi tu, bali hata pale tunapopewa madaraka ya kijamii kutuongoza.

SteveD.
 
Ili tuweze kuachana na uongozi mbovu ambao chanzo chake ni ubia wa Mwalimu inatubidi sasa tutizame elsewhere kutafuta uongozi mzuri ambao hautakuwa na uhusiao wa kiubia na Mwalimu.Tuachane na chama cha CCM cha ubia wa Mwalimu.

...if alternatively put!
 
Kazi kweli tunayo mpaka huyu MNYARWANDA leo anakuwa na ubavu wa kutukosoa...kazi kweli kwelo...i wonder who will be next katika hilo kundi lao la ma INTERAHAMWE!
 
GT,
Acha ukabila. Interahamwe walikuwa Wahutu. Jenerali ana asili ya Kitusi. Ni kama vile umwite Myahudi Mnazi wa Kijerumani.
 
Well, aliyosema Ulimwengu ni maneno muafaka kwa si-hasa zetu za kibongo. La maana ni kujiuliza mpaka lini tutaendelea na rais mungu- mtu? Ulimwengu kuwa mbia wa Nyerere si dhambi na at least mambo wakati huo yalikua si mbof mbof kama sasa. Nchi za wenzetu ktk chaguzi timu-wabia wa upngozi hufahamika wazi na misimamo yao lakini si hapa bongo uteuzi wa kishkaji a nifae kwa mvua nami nikufae kwa jua. 4me we still have a loooooooong way to go.

GOBELAGOBELA!

Usitupotezee muda hapa jamvini. Brother Jenerali is right yES! Wabia wa IKULU tunawajua wa kwanza nimtaje ni aliyekuwa MWEKA HAZINA WA CCM Rostam Aziz na kwa kuwa Kamati kuu ya chama cha majambazi iliridhia uteuzi wake kwa hiyo top brass ya ccm inao ubia Ikulu tatizo kwa sababu ni wezi hizo hisa hazijulikani . hakuna haja ya kuandika hadithi ndefu na kumkumbuka Nyerere.

Kwa bahati mbaya Waislamu hawaamini kwenye ufufuo kwa hiyo nakusihi kaka Jenerali umwache Nyerere apumzike wasemavyo wakatoliki kwenye raha ya milele.Ukimtajataja utatufanya tukufuru kama Suleiman Rushidie aliye fanya blasphemy dhidi ya waisalamu na kuiita QUARAN TAKATIFU satanic verses!! Yaliyomkuta wayajua fika!!! Marehemu Nyerere made a big mistake kumnadi fisadi Mkapa sitomsamehe!!!

Kama RA and Co. sio wabia let JAKAYA WA KIKWETE AJITETEE HAPA KWENYE HII FORUM vinginevyo angojee kiama akiondoka Ikulu itakuwa mbaya kuliko ya jambazi Mkapa. AS A SITTING PRESIDA BADO NAMTAFUTIA JINA!!! Kama hachukui time out akasoma JAMMII basi sa usual yeye ni mvivu wa kusoma ndio maana amekuwa rais kioja !!!

"Power tends to corrupt, and absolute power corrupts absolutely." (Lord Acton, 1887)
 
Kazi kweli tunayo mpaka huyu MNYARWANDA leo anakuwa na ubavu wa kutukosoa...kazi kweli kwelo...i wonder who will be next katika hilo kundi lao la ma INTERAHAMWE!

GT,

Ukweli utabaki ukweli tu, kama umesemwa na interahamwe au GT. When you come come correct if not don't come at all.Kuleta distractions za interahamwe na sideshows zingine kama hizo hakuondoi ukweli uliosemwa.

Gari likiwa linakuja kukugonga interahamwe akakwambia gari hilo linakuja kukugonga hutasikiliza kwa sababu huyu anayekwambia ni interahamwe?

Jadili hoja, kama hoja ina u interahamwe that is another matter, elezea vizuri tutakusikiliza.Lakini kujitia unamdismiss mtu, mtu mliyempa access makumi ya miaka, kafanya kazi kwenye ma newsroom tangu enzi za kina Mkapa pamoja na uongozi sehemu nyingi, kumdismiss kwa style hii kunaonyesha chuki, uvivu wa kufikiri, ufinyu wa mawazo, kupenda michezo ya kisiasa na kisaikolojia kuliko kufuatilia maswala, kuendekeza dhana za "sisi dhidi ya wao" ambazo zinakuwa sahihi yako siku hizi (what with your signature waislam non-issues) na mengine kama huo.

Lete hoja, usilete viroja.
 
Kazi kweli tunayo mpaka huyu MNYARWANDA leo anakuwa na ubavu wa kutukosoa...kazi kweli kwelo...i wonder who will be next katika hilo kundi lao la ma INTERAHAMWE!

Hapa CCM Chama cha mafisadi ndo mnapo nikosha,
Oscar Mkassa mganda wa kuazaliwa ubunge mna mpa tena kwa kupora haki ya wananchi fukara wa b'mlo kwa uharamia wa kubadilisha matokeo,

Ulimwengu kuwakosoa, kaisha kuwa nterahamwe! iam sure, angejitokeza kugombea ubunge kwenye chama chenu cha kifisadi, munge pinga kwa garama zozote zile kwamba yeye ni mzawa tena mwenye uchungu sana na Taifa lake,

By the way, aliyo yasema ni kweli tupu, haijalishi kayasema muiraki, msomalia, mchina ama mzaramo, ukweli wa hoja yake una simama, na tujadili hoja si mtu!
 
GT,

Ukweli utabaki ukweli tu, kama umesemwa na interahamwe au GT. When you come come correct if not don't come at all.Kuleta distractions za interahamwe na sideshows zingine kama hizo hakuondoi ukweli uliosemwa.

Gari likiwa linakuja kukugonga interahamwe akakwambia gari hilo linakuja kukugonga hutasikiliza kwa sababu huyu anayekwambia ni interahamwe?

Jadili hoja, kama hoja ina u interahamwe that is another matter, elezea vizuri tutakusikiliza.Lakini kujitia unamdismiss mtu, mtu mliyempa access makumi ya miaka, kafanya kazi kwenye ma newsroom tangu enzi za kina Mkapa pamoja na uongozi sehemu nyingi, kumdismiss kwa style hii kunaonyesha chuki, uvivu wa kufikiri, ufinyu wa mawazo, kupenda michezo ya kisiasa na kisaikolojia kuliko kufuatilia maswala, kuendekeza dhana za "sisi dhidi ya wao" ambazo zinakuwa sahihi yako siku hizi (what with your signature waislam non-issues) na mengine kama huo.

Lete hoja, usilete viroja.
Nakubaliana na wewe mkuu. Kuna wakati kuna juhudi za kuua hoja kwa viroja.Au pengine ni juhudi za kutaka hoja anazoziona yeye kama hoja ndo tu zijadiliwe
 
Back
Top Bottom