Ikulu ya Marekani yadai Wapiganaji 30,000 wa Wagner Group wameuawa vitani Ukraine

Pia mbona hawajasema ni wanajeshi wangapi wa Ukraine walio fariki? Au wino uliwaishia wakashindwa kuandika?
 
Ubaya wa jeshini au vitani hauruhusiwi rudi nyuma bila ruhusa ya CO wako.

Kuna wanajeshi wanawekwa kwenye defence line hawaruhusiwi ondoka
Brother hii inatokana na muundo wa jeshi na maamuzi ya uwanja wa medani, kwa mfano urusi wao muundo wao ni " Top down decision making system '' Yaani makamanda ambao wako front wanapokea order directly kutoka kwa wakubwa wao ambao wengine wanakuwa stationed kwenye commanding post. Hata ikitokea mmezungukwa mnaweza kudead au kutekwa kama amri haitoka juu kuwa mnapaswa kurudi nyuma.

Kumbuka mwanzo mwa uvamizi aliingia kwa mfumo wao wa " battalion tactical group ) hapa unakwenda na comprised units na regiment zote. Maamuzi kama haya yalipelekea st javelin zikapata umaarufu kwa kuvikaanga vifaru na magari ya urusi.

Hii ni tofauti na baadhi ya majeshi ambayo huwapa makamanda wa mstari wa mbele kufanya maamuzi kama withdrawing kama ikitokea mmezidiwa mapigo na adui.
 
Sasa si washinde kama wanapigana na wafugwa wasio na mafunzo?

Hawa wajinga badala waelekeze nguvu kwenye mapambano, wenyewe wanaelekeza nguvu kwenye propaganda!
Usitumie hasira ku argue maana utapoteza rationality ndugu. Huwezi kutenganisha vita na propaganda hasa unataka kupata morale victory ya askari na wananchi wako. Pia propaganda zinatumika kushusha morale ya adui yako kwa kumzushia taarifa za uongo au za kweli. Kwa mfano unaweza kuchapisha taarifa kuwa leo tumeoa battalion nzima ukaweka ushahidi wa uongo ili kumuogopesha adui.
 
Vitu vingine tutumie akili kama wanauawa wengi hivyo kwanini NATO wanawaogopa? Kwanini nchi kama Mali iliwafurumusha NATO (France) na kuwakaribisha Urusi (Wagner group)?

Embu tutumie akili bado asubuhi akili hazijachoka.
Wewe ndio ujaribu kutumia akili.Eti NATO inawaogopa wagner!!dunia nzima kuna utaratibu wa UN juu ya majeshi na wanaotakiwa kupigana vitani,sasa unakuwa na kundi ambalo halina mafunzo ya kijeshi ndio hayo ya kuchukua wafungwa magerezani na kuwapeleka vitani bila mafunzo yoyote!!hata kujua haki za mateka wa vitani hawajui wao ni pesa tu kwa aliyewakodi!!Huko bukinafaso mwezi dec wamefanya mauaji makubwa ya raia ,Huwezi ukajiuliza ni kwanini baada ya nchi nyingi za W.Africa kufanya mapinduzi mfululizo ndio wakamuona MRUSI kuwa ndio kimbilio lao?kwani mrusi/china wao kitu demokrasia na haki za binadamu hazina maana kwao.Ukanda wote ule wa SAHEL ni tabu tupu,badaye hata hao wagner watakimbia.
 
Toilet paper![emoji24][emoji24][emoji24]
 
Chanzo BBC🤣🤣🤣 anyway kama wewe ni mtaalam wa kusoma language utagundua NATO wamekubali kushindwa kuulinda mji wa Bakhmut(sizitaki mbichi hizi) kwenye bandiko kuna lugha ya kujifariji kwasana
 
Marekani isiyompemda marekani ndo imzingumzie urusi
 
Kwa hiyo wewe ulichoeleza hapa ndo unachojua tusichokijua wengine?
 
Na hao Wagner ukiwapanga dhidi ya jeshi la USA, na wote wakawa na silaha sawa nani atapigwa?
Kwanza uwezekano wa Wagner kupata silaha sawasawa na jeshi la Urusi ni mkubwa sana, mwanzoni mwa operation Wagnerites wachache waliokuwa frontline na Kadyrovites walipewa silaha nzuri kuliko jeshi. Vita ilipokuwa sio ya kitoto, Kadyrovites wakaondoka kutoka frontline wakaachana na kujirekodi Tiktot na boss wao alirudi zake Chechnya kuishi kifahari, ila Prigozhin akaingia magerezani kufanya recruitment na kupata wapiganaji wapya ambao ni less skilled na less motivated. Ndio hawa sasa wanakuwa moped down en masse, hawapewi silaha bora kwa sababu ni wengi na less skilled.

Wagner silaha zote iko supplied na Russian MoD, fronts wanatofautiana na jeshi ila logistics centres ni zilezile hivyo kupata silaha similar uwezekano upo. Meanwhile hakuna namna Wagner watapata silaha sawa na Marekani, wanaweza ambulia kupata bunduki sawa ila artillery, radars, ndege na vingine hamna.
Na hawawezi kamwe kuwa na training sawa, hata training ya jeshi la Marekani na gharama yake ni kubwa kuliko training ya jeshi la Urusi lenyewe. So hakuna namna Wagner inakuwa on par with US.

Kasome Wagner ilipokutana na US forces kipi kilitokea. Battle of Khasham - Wikipedia


Nimetaka kuweka link ya Wagner wenyewe mwezi huu wakifanya anniversary ya 5 years hilo tukio walieleza ilivyokuwa ila nimeshindwa. Channel yao Telegram ni Grey Zone ila ni Kirusi itabidi ufanye translation. Kuna mambo yao mengi utayapata wanajadili maana Russian media inawapa uzito kidogo
 
Wamewahesabu vipi? Siku zote wamarekani wanapenda kujisifia kwa kukandia wengine kwamba wao so wajuzi wa vita ma silaha zao ni hafifu. Waliwahi kusema drone na silaha za Iran ni hafifu na duni...at the same time wanalia kama Mbwa chokoraa wakisikia Iran wanapeleka drone na makombora yao Urusi. The same to North Korea wanasema kule silaha zao ni mbovu outdated..at the same time North Korea anaendelea kurusha makombora Yao kupitia anga la Japan bila mifumo wanayoiita ya kileo ya modern world ya kijapan kufanya chochote. So don't trust red necks.
 
Ubaya wa jeshini au vitani hauruhusiwi rudi nyuma bila ruhusa ya CO wako.

Kuna wanajeshi wanawekwa kwenye defence line hawaruhusiwi ondoka
Hao sio wanajeshi wa Urusi ni wahalifu waliokuwa jela African be ware they will use for canon fodder like Tarimo don’t send your children to die and they don’t even respect black people in Russia racism is massive
 
Inasikitisha sana ,yanini vita? Ardhi mmeikuta na mtaiacha....Dunia ina miaka zaidi ya bilioni 4 na nusu wakati maisha ya binadamu ni miaka 70 ukitoboa sana 80.
 
Haiwezekan ikitokea Wagner na jeshi la urus wakapambana supply ya silaha +support ya ndege vita na mengineyo watapata sawa
 
Umejuaje NATO inawaogopa?
Vitu vingine tutumie akili kama wanauawa wengi hivyo kwanini NATO wanawaogopa? Kwanini nchi kama Mali iliwafurumusha NATO (France) na kuwakaribisha Urusi (Wagner group)?

Embu tutumie akili bado asubuhi akili hazijachoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…