Ikulu ya Marekani yadai Wapiganaji 30,000 wa Wagner Group wameuawa vitani Ukraine

Walikufa wanajeshi wangapi wa USA?
Silaha zipi na kiasi gani za USA zilikamatwa na Wagner?
Hizo ni propaganda, hio ni saikolojia ya vita.
Hao USA hawatosahau kichapo toka kwa WAGNER GROUP walichopewa Alleppo Syria
 
Kiufupi jeshi la Russia katika uwanja wa mapambano linaongozwa kisiasa zaidi.
 
Ni muda mzuri kwa NATO kuingia wenyewe sasa ili wakawapige hao Wagner wasio na mafunzo mazuri ya VITA

Maana kama tu Ukraine na udhaifu wake anaweza kuua 9000 wanajeshi wa Wagner naimani NATO baba lao anaweza kuwapiga Wagner hadi kuingia Urusi ndani ya mwezi vita ikaisha

NATO waingie kumsaidia Ukraine mazima mazima wasikae nyuma kumpatia silaha huku akiendelea kudhoofika mwenzao

Naamini kama ingekuwa ni Taifa lingine pale ulaya mfano Belarus ndio angeivamia Ukraine hvyo sa hizi hadi Raisi wao angekuwa ameshanyongwa.
 
Msingi wa swali langu nilitaka kukupima kama unauelewa wa kutosha kati ya Regular Army ya nchi na Private Military Contractors.

1. Kwa namna yoyote ile PMC haiwezi kuwa na weledi zaidi ya Regular Army ya nchi.

2. PMC uwaga wanatumika kwenye very specific assignments. Hata hao US walikuwa wanawatumia Blackwater kule Iraq, Syria etc, je Blackwater ni zaidi ya US Amry?

Ipo siku utakuja kusema kwamba waasi wa M23 ni zaidi ya JWTZ kisa tu kuna wanajeshi wa JWTZ waliuliwa kwenye peacekeeping missions kule Congo.
 
Yani marekani aingie vitani na urusi? Unajua NATO iliundwa ajili gani?[emoji1787] Urusi sio chato mkuu
 
DEMOKRASIA mfumo wa hovyo bora uzidi kufeli kila eneo

Waacheni WAGNA wawatwange MANAZI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wargner Un skilled wamewatwanga UKRAINE pale SOLEDAR na bado wanachukua maeneo kila leo na wameikamatia pakubwa ARTEMOVSK

Sasa wagner na UKRAINE wapi ni UN skilled bado tu mmelemazwa na propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Propaganda tu hizo za nchi za magharibi
 
Jeshi la Urusi linazingatia huo msingi unaosema? Jeshi gani duniani huwa linafanya mobilization ya watu hawajawahi pigana kabisa kisha within 2 months wanakuwa frontline?

Hawa mobilised Russian forces waliotelekeza silaha Kherson bila hata kuziharibu unaona ni modern army. Wewe uliona wapi kwingine jeshi linaacha silaha very intact tena modern ili adui azichukue nzima nzima. Yani hata kumwagia gasoline kuzichoma moto walishindwa.

Kwani sasahivi kinachofanywa na hawa wawili kina tofauti gani, Wagner wameiteka Soledar kwa kupoteza wapiganaji wengi na vile vile Regular Army wamepigana na kushindwa Vuhledar mara ya pili baada ya kufeli tena November mwaka jana. At a certain time hizi ni armour za jeshi nahesabu 10 kwa pamoja zimeharibiwa sehemu moja haizidi hata uwanja wa mpira, hiyo ni modern army?
Urusi pale Vuhledar wanadrive into landmine.

Sasa kinachofanywa na Wagner kina tofauti gani na Regular, tena Wagner hawana artillery ya uhakika hawana air cover.
 
Wargner Un skilled wamewatwanga UKRAINE pale SOLEDAR na bado wanachukua maeneo kila leo na wameikamatia pakubwa ARTEMOVSK

Sasa wagner na UKRAINE wapi ni UN skilled bado tu mmelemazwa na propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
Neno less limetumika kufanya comparison ya Wagner walioanza vita na Wagner waliobebwa kutoka magerezani hawa kina Tarimo. Unategemea Tarimo mgombea ubunge mwaka 2020 awe mpiganaji sawasawa na Russian mariner aliyefukuzwa kwa matumizi ya madawa ya kulevya mwaka 2016 kisha akaingia Wagner na kwenda Syria, kisha akaingia Ukraine 2022?
 
Hizo ni propaganda, hio ni saikolojia ya vita.
Hao USA hawatosahau kichapo toka kwa WAGNER GROUP walichopewa Alleppo Syria
Unajifurahisha. Kuna uwezekano Wagner hawakuona hata mwanajeshi mmoja wa Marekani. Kwanza intelligence ya Marekani iliwaona Wagner mapema, zinaandaliwa AH-64 Apache na drones na gunship nyingine AC-130. Artillery ndio ilianza.

US Marines na Green Berets 40 hakuumia hata mmoja wakati Wagner walikuwa around 500. Walichoachiwa ni kurudi baadae kuokota maiti za wenzao. Kwanza ilikuwa usiku Marekani wanapigana kwa thermal na night vision hao wenzako wazitolee wapi. Video za Wamarekani nimezikosa na hata hivyo utazikataa, nakupa picha za Wagner wenyewe wakijutia ujinga wao, hiyo frame ya mwisho unaona kilichobaki ni helmeti. Russia iliwauza haikuwapa air cover.
 
Hivi marekani ndo anapigana vita ukraine, mbona kama yupo well informed na hizi ishu kuliko hata ukraine mwenyewe
 
Blackwater au makampuni mengine ya ulinzi ya Marekani hayaendi mstari wa mbele kupigana kama ilivyo kwa Wagner na Urusi.

Hao Blackwater walikuwa wanafanya kazi za ulinzi wa makambi, viwanja vya ndege, VIP protection na kusafirisha vifurushi. Hawakuwa jeshi linalopigana katika uwanja wa mapambano kama mamluki wa Wagner.
Usichanganye mambo.
 
UKRAINE wanabeba vijana mitaani wanawamobilise kilazima

Hawa sidhanii kama wanawapitisha hata kwenye hio miezi miwili ya mazoezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawawezi kua sawa

Lakini awali hukulisema hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…