Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
1,353
Reaction score
2,846
Taarifa nilizozipata muda huu ni kuwa Waandishi wa habari wameitwa Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi lengo ni kuwaonyesha Hati Ya Muungano na kukata mzizi wa Fitina Kwa wajumbe wa bunge la Katiba. Tutawajulisha hapa hapa...




Hii ni sehemu ya Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar...

 

Attachments

  • Saini.jpg
    25.2 KB · Views: 21,970
Taarifa zilizonifikia muda huu ni kwamba, Ikulu imewaita waandishi wa habari, Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue ndiye atazungumza nao na tetesi ni kuwa anataka kuwaonyesha waandishi wa habari Hati Ya Muungano...

Don't go away...
 
Antipas Lissu amewatwanga kitu!! hadi wamekodi UNGO kwenda UN!!! madude ya CCM yamekwisha!!
 
Kwani inatakiwa na waandishi au wajumbe wa katiba? Harufu ya uchakachuaji na kujihami imeanza kuonekana.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Yote haya kasababisha Pasco wa JF kauliza maswali magumu wanataka kumjibu kwa majibu mepesi
 
Katibu kiongozi anatoa nakala ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar!
 
kama nilivyosema anaongelea Hati ya Muungano, anasema hati ipo, na Rais amesema katibu mkuu ailete hati hiyo mbele ya wanahabari, anasema maneno yamekuwa mengi na yanayosemwa ni mengi na hati imetunzwa vizuri sana hadi sasa, na mwenyekiti wa bunge akiiomba basi wataipeleka huko bungeni na nakala ya hati hii itapelekwa makumbusho ili kila mwananchi aweze kuiona,
 
waandishi ndo wanataka kuionnyesha na ameionyesha mbele ya wanahabari na wanaipiga picha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…