Ikulu yawajibu Maaskofu wa Pentekoste kuhusu Wajumbe wa Bunge la Katiba

Ikulu yawajibu Maaskofu wa Pentekoste kuhusu Wajumbe wa Bunge la Katiba

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
Ikulu imetoa taarifa ndefu kuhusu madai ya maaskofu wa pentekoste (PCT) kuwa wametengwa kwa mjumbe wao kutokuchaguliwa katika bunge la katiba licha ya kupeleka majina kwa rais.

Kwa ufupi ikulu imesema baada ya uchunguzi imegundua kuwa maaskofu wa pentekoste hawakuwasilisha majina kwa njia ya kawaida, kujiteua ama kwa kuchelewa kwani database ya ikulu haijaonyesha ripoti ya maaskofu hao kutuma majina kwao.

Aidha ikulu imesema mjumbe mmoja alieteuliwa kwenye taasiai za dini Bi Edna Adam ametoka kanisa la EAGT ambao ni miongoni kwa wanachama wa baraza la maaakofu wa Pentekoste licha ya kwamba jina lake liliwasilishwa na taasisi nyingine ya dini na sio Baraza hilo la Maaskofu wa Pentekoste. Hivyo ikulu imewaomba maaskofu hao kumtumia mjumbe huyo kama mwakilishi wao na kuwa watawakilishwa kikamilifu.

Nitaiweka statement yote later licha ya kwamba ni ndefu sanaaa.
 
Hata Mtikila ni Pentecoste si wangle sema ndio mwakilishi wao? Kingunge anawasilisha wachawi, JK angeweka waliookoka si majini ya Kingunge yangekosa nguvu...
 
mtikila leo BBC kasema mle yeye anaenda kudai Tanganyika tu. Amesema tanganyika ilitajwa na kutabiliwa toka enzi katika Biblia kitabu cha mwanzo na matendo ya mitume na mipaka yake imetajwa. Basi pentekoste wafanye huyu ndio mwakilishi wao!
 
Ikulu imetoa taarifa ndefu kuhusu madai ya maaskofu wa pentekoste (PCT) kuwa wametengwa kwa mjumbe wao kutokuchaguliwa katika bunge la katiba licha ya kupeleka majina kwa rais.

Kwa ufupi ikulu imesema baada ya uchunguzi imegundua kuwa maaskofu wa pentekoste hawakuwasilisha majina kwa njia ya kawaida, kujiteua ama kwa kuchelewa kwani database ya ikulu haijaonyesha ripoti ya maaskofu hao kutuma majina kwao.

Aidha ikulu imesema mjumbe mmoja alieteuliwa kwenye taasiai za dini Bi edna adam ametoka kanisa la EAGT ambao ni miongoni kwa wanachama wa baraza la maaakofu wa pentekoste licha ya kwamba jina lake liliwasilishwa na taasisi nyingine ya dini na aio baraza hilo la maaskofu wa pentekoste. Hivyo ikulu imewaomba maaskofu hao kumtumia mjumbe huyo kama mwakilishi wao na kuwa watawakilishwa kikamilifu.

Nitaiweka statement yote later licha ya kwamba ni ndefu sanaaa.
Ili kuondoa malalamishi, Ikulu watuwekee orodha Kama ilivyowasilishwa na makundi mbalimbali na uteuzi uliofanyika. Hii wanaosemwa bado watu wataendelea kuamini kuwa Ikulu haikufuata kikamilifu mawasilisho ya makundi Kama walivyopendekeza.
 
mtikila leo BBC kasema mle yeye anaenda kudai Tanganyika tu. Amesema tanganyika ilitajwa na kutabiliwa toka enzi katika Biblia kitabu cha mwanzo na matendo ya mitume. Basi pentekoste wafanye huyu ndio mwakilishi wao!
Huyu mtikila anabwabwaja hawezi kuwawakilisha. Yeye ana msimamo mmoja tu ambao sidhani kama ni vyema na ukumsikiliza sana na kuangalia matendo yake pia utagundua kuwa hata yeye haamini anayoyasema!
 
Mtikila nami ningekuja kwenye hilo baraza ningedai Tanganyika hivyo tungekuwa wawili
 
Nimeskia channel ten

Kimsingi ofisi ya pinda na kubwa jinga letu wanaigiza mambo

Ngoja kesho tuwaskie maaskofu waaminifu wa Pentecostal si hawa majambazi
 
Uwepo wa mtikila na prof lipumba umebeba maana na uwakirishi mkubwa wa Tanganyika nzuri yenye kuakisi matumizi mazuri ya rasilimali zetu kukidhi hali ya uchumi wa taifa letu barikiwa.
Fanyeni kazi nzuri msiendeshwe/yumbishe na mihemko ya kisiasa.
 
Hapa Ikulu imechemka tena na huenda ikawasha moto zaidi.
Mtu ambaye hakutumwa na Baraza la Maaskofu wa Pestecoste aende tu kuwawakilisha kwa kuwa ni muumini wa EAGT tu, how? Na hiyo taasisi iliyomtuma kwenda kuiwakilisha kama ina mapendekezo yake yanayopingana na Baraza la Maaskofu wa Pestecoste?

Yaani mjumbe mmoja aende kuwakilisha taasisi mbili tofauti tena kubwa?

Wakati mwingine kukiri kosa ni uungwana sana, Ikulu ikiri tu kuwa ilikosea.
 
Ikulu imetoa taarifa ndefu kuhusu madai ya maaskofu wa pentekoste (PCT) kuwa wametengwa kwa mjumbe wao kutokuchaguliwa katika bunge la katiba licha ya kupeleka majina kwa rais.

Kwa ufupi ikulu imesema baada ya uchunguzi imegundua kuwa maaskofu wa pentekoste hawakuwasilisha majina kwa njia ya kawaida, kujiteua ama kwa kuchelewa kwani database ya ikulu haijaonyesha ripoti ya maaskofu hao kutuma majina kwao.

Aidha ikulu imesema mjumbe mmoja alieteuliwa kwenye taasiai za dini Bi Edna Adam ametoka kanisa la EAGT ambao ni miongoni kwa wanachama wa baraza la maaakofu wa Pentekoste licha ya kwamba jina lake liliwasilishwa na taasisi nyingine ya dini na sio Baraza hilo la Maaskofu wa Pentekoste. Hivyo ikulu imewaomba maaskofu hao kumtumia mjumbe huyo kama mwakilishi wao na kuwa watawakilishwa kikamilifu.

Nitaiweka statement yote later licha ya kwamba ni ndefu sanaaa.

Ina maana maaskofu wa kipentekoste mlishindwa kujiteuwa! Mnatia aibu sasa, kumbe mnalalamika bure, tatizo lenu, mna umimi kama wapemba, ubaguzi.
 
Nahisi labda Serikali inawachukulia wapontekoste kama jamii ndogo sana, Watu duni sana nk. Maana mara kwa mara kwenye mambo mengi sana ya kitaifa inakwepa kuwatambua na kuutambua mchango wao.

Jaribu kuchunguza hili utaliona kabisa.
 
Kingunge 4.jpg
 
Kwa hoja hii ya Ikulu ilifaaa kabisa TEC ikawakilishwa na Anne Makinda , BAKWATA na Sadifa JUMA etc ......Ikulu inachemka sana , itakuwaje mtu kwa kuwa ni Mumiani wa dini fulani basi awe mwakilishi wao automatically? Kuna haja gani ya kuwa na wawakilishi?
 
Chaguo la Mungu leo kawageuka, ndiyo wajifunze sasa. Halafu hawa waliotoa taarifa hii akili wanazo kweli. Maana haiwezekani mtu katumwa na taasisi alafu aiwakilishe taasisi nyingine?
 
Kienyeji enyeji tu.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Nimeskia channel ten

Kimsingi ofisi ya pinda na kubwa jinga letu wanaigiza mambo

Ngoja kesho tuwaskie maaskofu waaminifu wa Pentecostal si hawa majambazi

Serikali ya ccm imelaaniwa kwa kushindwa kuwatambua watumishi wa Mungu,wanaokesha wakiiombea taifa.Ni dharau kubwa kushindwa kuwaheshimu pct yenye watanzania robo ya watu wote wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom