Ikulu yetu haina taarifa za Rais zaidi ya picha zake na wazungu?

Ikulu yetu haina taarifa za Rais zaidi ya picha zake na wazungu?

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Tangu rais aende kwenye mkutano wa Davos nimekuwa nafuatilia mafanikio ya ziara hiyo kiuchumi bila mafanikio.

Kila taarifa inayotolewa na Ikulu mitandaoni, haina maelezo ya manufaa zaidi ya Rais kasimama na huyu, akiwa mkutanoni, anapewa zawadi, n.k. Hatusikii kazungumza lipi na nani la manufaa ya kiuchumi.

Kama hakuna manufaa ya ziara ya Rais, alikwenda kufanya nini? Mbona Museveni alikua arabuni na mikataba ya kibiashara?

Nadhani ifikie kiwango cha viongozi wetu pia waongozwe. Hatuhitaji kuona picha za rais na wazungu aliokutana nao.
 
Halafu kuna kurugenzi ya mawasiliano ambayo waajiriwa wake wanalipwa.

Washukuru kuwa kuna wana JF huwa wanajaribu kufuatilia ziara hizi kwa ukaribu na kutupia thread.
 
Nionavyo mimi, Sasa safari zimekuwa kama matembezi ya kuijua dunia. Mambo ya kiswahili na kupongezana; mimi nilishafika Davos, hata Washington nilifika, Dah! miaka ile nilitembea sana!

Dunia hii unawaacha mabalozi wa nchi marafiki wa EU wakiwa hapa Dar, unakwenda kwenye mkutano wa uchumi wa Dunia nasi hatusikii nasaha zozote za kiuchumi kutoka kwako! Basi danganyeni lolote kama alivyofanya yule wa TBC kwamba Trump kamsifu JPM, angalau wasioisoma dunia waamini uongo huo. Picha zinatia kichefuchefu. Bora zile za Peter (Pila) wa Royal tour.
 
Unaripoti Kutokea wapi ndugu Zygot?😳😳
 
Pengine kiingereza kinakupiga chenga kamanda lakini Jana madame Zuhura alitoa press release taarifa ya ziara ya Rais na mpango mkakati wa serikali kuboresha kilimo kwa 3.6% mpaka 10% ifikapo 2030 na kuhimiza wawekezaji kuwekeza.

Hii ni faida kubwa kwa uchumi wa nchi ikizingatiwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa.

Leo tena kuna taarifa imetolewa mhe. Rais ushirikiano na ubia kwenye sekta ya nishati.

Kama haya hujayaona basi kuna tatizo kubwa katika Elimu yako.
 
Tangu rais aende kwenye mkutano wa Davos nimekuwa nafuatilia mafanikio ya ziara hiyo kiuchumi bila mafanikio. Kila taarifa inayotolewa na Ikulu mitandaoni, haina maelezo ya manufaa zaidi ya rais kasimama na huyu, akiwa mkutanoni, anapewa zawadi, n.k. Hatusikii kazungumza lipi na nani la manufaa ya kiuchumi.

Kama hakuna manufaa ya ziara ya rais, alikwenda kufanya nini? Mbona Museveni alikua arabuni na mikataba ya kibiashara? Nadhani ifikie kiwango cha viongozi wetu pia waongozwe. Hatuhitaji kuona picha za rais na wazungu aliokutana nao.
Je, hiyo taarifa?
20230119_190257.jpg
 
Back
Top Bottom