Ila baridi, nakula lakini nasikia njaa haraka baada ya kula😃😃....

Ila baridi, nakula lakini nasikia njaa haraka baada ya kula😃😃....

Wakuu habari ya leo,.
(Chit-chats and jokes)

Leo em mniambie kwanza Kuna uhusiano gani kati ya hali ya hewa (baridi) na kula sana. kipindi cha baridi nakuwa njaa mda wote,. Yaani nakula kama kiwavi😌

Mfano leo,. Wakati natoka nyumbani nlikunywa uji mandazi mawili nikachukua na maziwa mtindi na maji nikajiambia hapa nishashiba maziwa mtindi na maji yatanisogeza Hadi jioni nitarudi kula nyumbani,. Mwe!😅

Picha linaanza kabla ya sa3 njaa ikaanza kuuma nikanywa maziwa yote haijapita hata nusu saa najiona kama sijala kitu nikaagiza supu nimekunywa,. Nikanywa na maji mengi lakini sa6 sita sa7 njaa tena ikaniuma, nikaagiza chips nimekula nimekunywa maji meengi lakini tumbo naliona liko empty .. Saizi Tena nimekula parachichi na yogurt nimemaliza lakini Bado naona kama tumboni Kuna vitu vinacheza vinaniambia inabidi Nile tena maskini😭😂View attachment 3366943


Dawa za minyoo nazinywa sana lakini hali naona Bado,. Nashindwa kujizuia kula .. Anayejua tatizo nini please au ndio baridi??
Kweli we Kiwavi tena sio jeshi ni kiwavi komando unakula Sana mtindi, supu, mandazi, maharage, mara parachichi, yogurt, chips,maji meengi dah!
 
Kweli we Kiwavi tena sio jeshi ni kiwavi komando unakula Sana mtindi, supu, mandazi, maharage, mara parachichi, yogurt, chips,maji meengi dah!
Daaah😂😂😂,.
Hapa enyewe nimetoka kula sambusa 5 imagine
 
Kwani Yeye Amesema Anakula Majani??Mbona Ameorodhesha Mlolongo Mzima Wa Menyu Yake,,Kwa Upande Wangu Sijasoma Hilo Swala La Kutafuna Nyasi...
Mtoto huyu ni vita bwashee
 
Sio mwembamba sio mnene niko Saizi ya kati,. Mwezi March nlikua Nina 51kg saizi sijui nina ngapi

Sio mjamzito

Yeah huku niliko saizi ni msimu wa baridi
Kumbe ni cha upepo, alafu unakula hivyo na Una kilo 51! dah sema nini....
 
Tumeumbiwa Sisi Hizo Vita Bwashee,,Sharti Ni Kupambana Na Kukabiliana Nazo Kwa Namna Yoyote,,Na Kama Ujuavyo Bwashee Vita Haina Droo,,Ni Upasuke Au Upasue Bwashee....###ChaguziNiYako###
Mchukue sasa bwashee halafu unitag mimi kumchukua kutoka kwako ili bato iwe bato kwel🤣
 
Mimi Popote Pale Ni Vita Iwe Ni Ya Akili,,Nafsi,,Au Kimwili....
Upo nnje ya mada wewe unaunganisha matatizo yako ya kukosa pesa na mambo nyeti ya dunia , nikisema hivyo nakosea bwashee?
 
Mkuu kwa hivyo vyakula? Ni halali kabisa.

Maandazi mawili 👀
Chipsi 👀
Yoghurt 👀
Parachichi 👀

Hivyo vyafaa kua vionjo, asubuhi piga Uji wa ulezi na Mkate wa ngano, Magimbi, Mang'amba au mihogo.

Mchana dona la nguvu au wali wa kutosha + mboga7 + matunda + maji.

Hivyo ulivyovitaja ni viburudisho vya kujazia jazia kama ukipenda.

Njaa utaisikia tu!!
Na kweli hapo hamna msosi.
 
Back
Top Bottom