Sisa Og
JF-Expert Member
- Apr 18, 2024
- 201
- 504
Kwanini Bongo Flava Ni Ngumu Kufika Mbali Kama Afrobeats, Amapiano au AfroHouse
Tusipoteze muda twende kwenye points
* WAANDJI (Producers)
Hawa jamaa wamekosa ubunifu. Wanasubiri dunia ilete style mpya wao ndo waje kufanya blending kwneye Bongoflva. Wakati mwingine hawafanyi blending wanakopy kama ilivyo.
Wengi hawana elimu ya mziki, wamejifunza mtaani, hata uelewa wa Musical genre.Ndo maana mpaka leo hakuna official rhythm ya BongoFlava. Sababu tunafanya blending na aina nyingi za nyimbo, RnB, hiphop, Afrobeats, Reggae. Kila producer ana Rhythm yake. Mfano, Kayumba, Mbosso, Barnaba wanaimba BongoFlava ila kutokana na kublend aina nyingi za nyimbo hivyo kunatokea utoafuti mkubwa sana.
* WASANII SASA
Wengi hawana ubora. Ni wasanii wa studio.
Maisha yao ya ajabu sana. Wanatangaza kiki kuliko kazi. Mfano, unakuta msanii anatrend kuliko kazi zake. Leo hii nikikwambia, uniambie dem wake Wizkid, Rema, Burna Boy au Olamide, hakika utateseka sana. Ila Bongo sasa!
Msanii akiwa ni mtu wa kutrend sana watu tunasahau kazi tunadeal na maisha yake. Mfano; Watu tunajua skendo nyingi za Kanye West kuliko mziki wake.
Wengi wao huku, hutanguliza kiki kabla ya kutoa ngoma. Na ngoma zote huishia humuhumu sababu walengwa ni sisi. Mafano, nyimbo za Harmonize anamwimbia Kajala nani anazo kwenye devices zake mpaka leo.
* PRODUCTION MBOVU
Hapa nazungumzia sound nzima, beat making, vocal mixing na Mastering. Kwa upande wa beat wengi wanajitahidi ila mastering bado. Kazi hazina ubora. Mixing za nyimbo zinasoud local. Hamna ubunifu. Hata ukisikia nyimbo, back vocal, harmonization, compressing yake. Kwa hili, Lizer na mixing killer wanajitahidi sana.
Sababu maproducer wetu hawaendi shule. Na hicho wanachofundishana hamna wanachoongeza. Kwa watu ambao mnasikia mziki wa jirani zetu Rwanda, Kenya na Burudndi - mtakubaliana nami kuwa jamaa wanatuzidi sound japo ndo hivyo bado hawajajipata. Ila hasa Rwanda na Burundi wana sound kali sana. Sikia kazi za Theecember, Drama T, Element, Chris Eazy, Nillan na wengine wengi.
Kazi ambayo haina sound kali (good beats na sound) haivutii.
*LUGHA
Aliyesema mziki ni universal language leo tumuache kwanza. Kuna kitu hakukiweka wazi.
Unaposikiliza mziki ambao una ushairi unauelewa ni rahisi kuutunza moyoni na kuuplay kila upumzikapo au unapo feel kuenjoy mziki. Hizi ambazo hatuelewi lugha ni nyimbo za kuruka nazo hasa clubs, uko na wana. Na si rahisi kumzingatia msanii sababu hata uelewi anachoimba. Kama ungeelewa ungemfuatilia ili awe anakuhamasisha hasa kama nyimbo zake ni za kushauri, kuhamasisha. Mfano Despactito hatuelewi walichokiimba ila ukiuliza watu nani aliimba na kama wanamjua basi wangapi waliendelea kumfuatili baada ya hiyo kazi, ni wachache sana.
Itoshe kusema, kiswahili ni changamoto katika mzimi wetu kwenda mbele.
* UTAMADUNI
BongoFlava ni mziki ulioambatana na utamaduni wa mswahili kwa asilimi kubwa. Ndo maana unatumia kiswahili, midundo ya kipwani hasa kwa wasanii wanaoblend na Baibuda. Mada zinaimbwa ni kutokana na utamaduni wetu. Mafano, vijembe, umbea, nk.
Siku zote ambao umeambatana na utamaduni sana ni ngumu kwenda mbele. Ndo maana wahindi, wachina, wakorea nao wanaimba sana huko kwao ila ngoma zak haziendi popote. Sisi tulikuwa tunawasikiliza wahindi lakini hatukuwapend ndo maana tunakimbilia kublend Amapiano, afrobeat, RnB na hiphop na sio wahindi.
*LABEL NA MAMENEJA
Kwanza label zinazojulikana na za uhakika ni WCB na King Music. Lakini ukweli usemwe, WCB ndo imejitahidi kufika level za Afrika.Ila label zililzobaki sielewi zinafanya nini. Msanii anakaa kwenye label miaka mitatu anatoka hana hata pikipiki na lawama kibao.
Sasa hapa mziki unakuwaje?
Mtu akipata hela basi anaanza kumiliki wasanii anakuwa manager. Huyo mtu muda mwingine hajui mziki unaendaje, anataka kunyenyekewa sana. Na msanii akikorofishana naye basi anaacha kazi zote na kuanza kupambana msanii asifikw popote.
*MUSIC PROMOTION
Wasanii wetu ni outdated. Wanakomaa na YouTube. Labda wanashindwa kujua kuwa, YouTube sio platform ya mziki. Mziki ni sehemu ya part tu.
Mpaka leo hakuna msanii aliwahi fikisha hata stream 1.5 milioni huko Spotify. Diamond akinitahidi ni 1.3 milioni basi.
Hii inaonesha nguvu kubwa ipo YouTube, Boomplay, na Interviews za redio.
Hii inaonesha jinsi gani mziki wetu tunapiga mwenyewe na tunasikiliza wenyewe. Maana Boomplay ni platform ambayo ina watumiaji wengi kutoka huku.
* MASHABIKI
Asili ya Tanzania ni ujuaji, ushindani na umbea. Haya mambo yapo hata kwenye mziki sasa.
Master Jay akisimama kuwambia ukweli, maana jamaa ni expert wa mziki sisi ndo tuko busy kumponda bila sababu. Kwa kufanya hivyo tunawabwetesha wasanii wetu.
Lakini pia mashabiki wengi wanapakua nyimbo kutoka kwa Dj Mwanaga, yinga media na beka boy. Hapa msanii hapati chochote labda aandae show.
Hii inasbabisha wasanii wadogo waende kuwalipa hela hao mablogger ili wapost kazi zao. Hata mimi nishawahi fanya huu mchezo.
Mashabiki hao hao wanamjazia comment Rayvanny na kumdhihaki eti ni mtu wa Remix. Au huu ni utani.
*MAZOEA
Msanii akitoa album, kitu ambacho anafanya cha maana ni listening part. Anapost platforms na kuandaa kiki halafu anaanza kufosi interview ili kazi iende.
Sijui hizi strategies walizitoa wapi?
Wakati Tems, Burna Boy au Wizkid na wengine wakitoa album wanaandaa Tour za album nchini na nje na wanaperform kazi zao.
Wasanii wanatoa nyimbo kama post za FB. Msanii anatoa nyimbo 5 ndani ya miezi miwili na zote hazina proper promo strategies.
Mfano. Diamond ni msanii mkubwa ila kazi zake haziko documented. Kujua nyimbo kaandaa nani, kaandika nani, ni aina gani, imeshika chart nchi gani. Wasanii kama Tems, Ngoma zao zaidi ya nusu zipo Wikipedia and well detailed.
Hii inaonesha userious na ni best for future use.
Wasanii hata mashabiki wengi hawana uelewa juu ya Grammy Award. Kutwa wanamzomea Diamond kwanini hana grammy. Sidhani kama kuna msaniibhapa Bongo yupo Academy kama mwanachama. Sasa mtu hata hajajiunga Academy anawaniaje Grammy.
Ntazungumzia hilu next time.
NB: Tunasikiliza nyimbo za Wanaijeria na Wasauzi sababau wana ladha tofauti na yetu, ila tunataka haohao watusikilize sisi baada ya kufosi kufanana wao.
Nini kifanyike....
Next time. Ntazungumza hili