Ila Gen Z wanatisha: Rais Ruto afuta Bajeti ya Ofisi ya Mke Wake!

Ila Gen Z wanatisha: Rais Ruto afuta Bajeti ya Ofisi ya Mke Wake!

Kama Samia anataka apendwe na watanzania wote basi atimize yaliyopendekezwa na generation z.Maana mambo ya hovyo ambayo wtz hawayataki ndiyo hayo ambayo yameondolewa Kenya.Lakini akiendelea kuziba masikio kama anavyojiita bibi chura kiziwi,ipo siku yatamtokea puani
 
Hii nimeona ni kali zaidi yaani Ruto amebanwa hadi amefuta Bajeti ya Ofisi ya Mke wa Rais

Kwa sasa Gen Z ndio wanatengeneza Sera za Nchi yao, Wazee wamepumzishwa.
---

Rais wa Kenya, William Ruto ameondoa bajeti ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ofisi ya Mke wa Rais, Mke wa Naibu Rais na Mke wa Waziri Kiongozi na amefuta Mashirika 47 ya Serikali na kusitisha safari zisizo za lazima kwa Wafanyakazi wa Serikali pamoja na kuzuia ununuzi wa magari mapya ya Serikali.

Akihutubia Taifa la Kenya leo July 05,2024 Ruto ametangaza kupunguza idadi ya Washauri wake kwa 50% ambapo ameanzisha hatua nyingine kadhaa za kubana matumizi ili kupunguza gharama kubwa ambazo Serikali inaingia na pia amekata bajeti za ukarabati wa majengo ya Serikali kwa 50%.

Ruto pia amesema hakuna Afisa wa Serikali atakayeruhusiwa kushiriki katika shughuli za kuchangisha pesa zinazoendelea na amewaagiza Maafisa wa Serikali kuacha shughuli za hisani, hasa walioonekana wakionyesha pesa nyingi wakati wa hafla za kutoa misaada ambayo imezua taharuki kutoka kwa Wakenya.

Ruto amesema kufuatia mashauriano mapana na wenzake wameafikiana kupunguza gharama mbalimbali zikiwemo kufuta angalau Mashirika 47 ya Serikali yenye vipengele vinavyoingiliana lengo likiwa ni kuboresha huduma za Serikali kwa Wananchi na kuwafanya Wakenya wapate huduma sahihi kutoka Serikalini.

PIA SOMA
- Rais Ruto kushiriki mjadala na Wakenya kwenye X Space, Julai 5 kwa saa tatu
Gen Z wametumia muda mchache sana kuielezea Serikali wanataka nini na wameeleweka.
 
Huku Gen Z wetu wako bize kukesha kitambaa cheupe wakicheza amapiano.
Kwa bajeti hizi za kuchangiwa changiwa na wahisani, ni ngumu kuendelea muda mrefu kupiga piga raia wakiingia mtaani huku wakiwa na hoja.

Kwa sababu wale jamaa wanaochangia hawataki hizo issue za kupiga raia ovyo, hivyo ukiwazingua utahatarisha huo uchangiaji wao, maana hawakawii kughairi kuchangia

Magufuli (RIP) alipokataa tu watoto waliopata mimba shuleni kurudi shule baada ya kujifungua, ilikuja kuharibu kila kitu, kwani wahisani waligoma bajeti.

Ujue ilipita miaka miwili au zaidi bila Marekani kuchangia bajeti ya vitabu, naye naweza kusema ndiye mmoja wa wachangiaji wakuu wa bajeti ya vitabu mashuleni, hata kwa kiada na ziada.

Kwa hiyo miaka miwili hakuna kitabu cha kiada wala ziada kilichoenda mashuleni.

Ova
 
Kwa bajeti za kuchangiwa changiwa na wahisani, ni ngumu ukiendelea kupiga piga raia wakiingia mtaani huku wakiwa na hoja.

Kwa sababu wale jamaa hawataki hizo issue za kupiga raia, kwa hiyo utahatarisha huo uchangiaji wao hawakawii kughairi.

Magufuli (RIP) alikataa tu watoto waliopata mimba shuleni kurudi shule baada ya kujifungu, ikaharibu kila kitu, kwani wahisani waligoma.

Ujue ilipita miaka miwili bila Marekani kuchangia vitabu, naye naweza kusema ndiye mmoja wa wachangiaji wa vitabu mashuleni, hata kwa kiada na ziada.

Ova
Asante kwa elimu hii b...
 
Nasema hivi, japo tuangalie tu maudhui ya mada zinazoletwa humu JF
Ndio tutajua kama hata hao Gen Z tunao au tumebarikiwa na mbululas
 
He is not doing that because is scared of them ….he is humble and listener president…
He didnt listen when they were planning this, until youth took it to the streets. So without pressure there is no change
 
Back
Top Bottom