Na wanajua hakuna wa kuwaghasi.Wakati Kenya bajeti ya Ofisi ya Mke wa Rais inafutwa huku Tanzania bajeti ya kuwalipa viinua mgongo, mafao na marupurupu wake za ma-Rais zinaanzishwa.
Wewe imefanya nini kwenye nchi hii unataka nani akupiganieBila kusahau kubet na kushabikia Simba na Yanga.
Unataka nani akupiganie weweGen Z ya huku wenyewe bado wanabishana kati ya Caf dogo na Caf kubwa lipi ni kombe kubwa.
Unataka nani akupiganieBodaboda mbona umeenda mbali. Wanawekea tamasha la Diamond bila kiingilio na Tshirt zenye sura ya mama kuupiga mwingi. Wakitoka hapo ni mwendo wa mapambio tu.
ningekujibu ila utasema nimekuvunjia heshima.Unataka nani akupiganie
Jibu swali unataka nani akupiganie wewe ukiwa hapa jamii forumningekujibu ila utasema nimekuvunjia heshima.
Gen Z wametumia muda mchache sana kuielezea Serikali wanataka nini na wameeleweka.Hii nimeona ni kali zaidi yaani Ruto amebanwa hadi amefuta Bajeti ya Ofisi ya Mke wa Rais
Kwa sasa Gen Z ndio wanatengeneza Sera za Nchi yao, Wazee wamepumzishwa.
---
Rais wa Kenya, William Ruto ameondoa bajeti ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ofisi ya Mke wa Rais, Mke wa Naibu Rais na Mke wa Waziri Kiongozi na amefuta Mashirika 47 ya Serikali na kusitisha safari zisizo za lazima kwa Wafanyakazi wa Serikali pamoja na kuzuia ununuzi wa magari mapya ya Serikali.
Akihutubia Taifa la Kenya leo July 05,2024 Ruto ametangaza kupunguza idadi ya Washauri wake kwa 50% ambapo ameanzisha hatua nyingine kadhaa za kubana matumizi ili kupunguza gharama kubwa ambazo Serikali inaingia na pia amekata bajeti za ukarabati wa majengo ya Serikali kwa 50%.
Ruto pia amesema hakuna Afisa wa Serikali atakayeruhusiwa kushiriki katika shughuli za kuchangisha pesa zinazoendelea na amewaagiza Maafisa wa Serikali kuacha shughuli za hisani, hasa walioonekana wakionyesha pesa nyingi wakati wa hafla za kutoa misaada ambayo imezua taharuki kutoka kwa Wakenya.
Ruto amesema kufuatia mashauriano mapana na wenzake wameafikiana kupunguza gharama mbalimbali zikiwemo kufuta angalau Mashirika 47 ya Serikali yenye vipengele vinavyoingiliana lengo likiwa ni kuboresha huduma za Serikali kwa Wananchi na kuwafanya Wakenya wapate huduma sahihi kutoka Serikalini.
PIA SOMA
- Rais Ruto kushiriki mjadala na Wakenya kwenye X Space, Julai 5 kwa saa tatu
Kwa bajeti hizi za kuchangiwa changiwa na wahisani, ni ngumu kuendelea muda mrefu kupiga piga raia wakiingia mtaani huku wakiwa na hoja.Huku Gen Z wetu wako bize kukesha kitambaa cheupe wakicheza amapiano.
Asante kwa elimu hii b...Kwa bajeti za kuchangiwa changiwa na wahisani, ni ngumu ukiendelea kupiga piga raia wakiingia mtaani huku wakiwa na hoja.
Kwa sababu wale jamaa hawataki hizo issue za kupiga raia, kwa hiyo utahatarisha huo uchangiaji wao hawakawii kughairi.
Magufuli (RIP) alikataa tu watoto waliopata mimba shuleni kurudi shule baada ya kujifungu, ikaharibu kila kitu, kwani wahisani waligoma.
Ujue ilipita miaka miwili bila Marekani kuchangia vitabu, naye naweza kusema ndiye mmoja wa wachangiaji wa vitabu mashuleni, hata kwa kiada na ziada.
Ova
Mchana wako viwanda vya betting ......Huku Gen Z wetu wako bize kukesha kitambaa cheupe wakicheza amapiano.
Naona unadandia gari kwa mbele au unawwashwa?Wewe imefanya nini kwenye nchi hii unataka nani akupiganie
He didnt listen when they were planning this, until youth took it to the streets. So without pressure there is no changeHe is not doing that because is scared of them ….he is humble and listener president…
Ndiyo rahaa ya kushiba,Mapiano lazima yachezeke ili chakula kishuke alafu kesho tule tena!!!Huku Gen Z wetu wako bize kukesha kitambaa cheupe wakicheza amapiano.
Mwanaume hakimbii matatizo, huwa ana ya face, na ndicho alichofanya Ruto!!Ruto kaonesha udhaifu mkubwa, angwachia ngazi tu.
Wakishauwana sana, Mzee Kikwete yupo tutampeleka akawapooze.Mwanaume hakimbii matatizo, huwa ana ya face, na ndicho alichofanya Ruto!!
jifunze kuandika basiWakishauwana sana, MzeeKiweteyupo tutampeleka akawapooze.