tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Wakuu leo tuchambue kidogo ubunifu uliofanywa kwenye huu wimbo wa NANI uliochapishwa na Diamond dakika 30 zilizopita kwenye channel yake ya You Tube.
Tukianzia story telling aliyoitumia hadi setting zake zimekaa kiubunifu sana hasa mazingira ya shule ilivyoanza anatambulishwa kama mwalimu mpya na muda wa utambulisho yeye anakuwa njiani bado anahangaika na usafiri hadi kufika na kuzama kwenye penzi na mwalimu mwenzake. Nimependa sana story telling kwasababu imepiga kwenye uhalisia, kutoka kuwa walimu hadi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
Scene zimenyooka, hazina miktadha ya kuvunja maadili na uhusishwaji wa matusi, hakuna scene zinazoonyesha wadada kuvaa utupu, ametumia lugha ya mafumbo pale alipoona anachokirejelea kinaweza kutokuwa na maadili. Kwa ufupi ni wimbo ambao unaweza kuskilizwa na kila mtu na kila mahali.
Kitu gani ulichokiona humo ndano kilichokuvutia sana na umeona kuwa Msanii amekitendea haki kama kazi ya sanaa inavyopaswa kuwa