Ila Mondi kwenye huu wimbo mpya wa NANI ubunifu ni wa viwango vya kimataifa, tuujadili kidogo

Ila Mondi kwenye huu wimbo mpya wa NANI ubunifu ni wa viwango vya kimataifa, tuujadili kidogo

Kwani nyimbo zake anaandikiwaga?

Ndio na ni kawaida hata waimbaji wengine duniani na wanaweka wazi hadi jina la mtunzi inajulikana. Baadhi wasio na kipaji haswaaaa cha kutunga nyimbo zao wenyewe na wale wakiishiwa ya kuandika wao huwa wananunua na kuimba.

Kwa yeye hajaanza jana wala juzi nilivyosikia kitambo ila haweki wazi kwamba ananunua na hataki mtunzi aseme.
 
october hakikisha unatiki
Wakuu leo tuchambue kidogo ubunifu uliofanywa kwenye huu wimbo wa NANI uliochapishwa na Diamond dakika 30 zilizopita kwenye channel yake ya You Tube.

View attachment 3486501

Tukianzia story telling aliyoitumia hadi setting zake zimekaa kiubunifu sana hasa mazingira ya shule ilivyoanza anatambulishwa kama mwalimu mpya na muda wa utambulisho yeye anakuwa njiani bado anahangaika na usafiri hadi kufika na kuzama kwenye penzi na mwalimu mwenzake. Nimependa sana story telling kwasababu imepiga kwenye uhalisia, kutoka kuwa walimu hadi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Scene zimenyooka, hazina miktadha ya kuvunja maadili na uhusishwaji wa matusi, hakuna scene zinazoonyesha wadada kuvaa utupu, ametumia lugha ya mafumbo pale alipoona anachokirejelea kinaweza kutokuwa na maadili. Kwa ufupi ni wimbo ambao unaweza kuskilizwa na kila mtu na kila mahali.

Kitu gani ulichokiona humo ndano kilichokuvutia sana na umeona kuwa Msanii amekitendea haki kama kazi ya sanaa inavyopaswa kuwa
 
Ndio na ni kawaida hata waimbaji wengine duniani na wanaweka wazi hadi jina la mtunzi inajulikana. Baadhi wasio na kipaji haswaaaa cha kutunga nyimbo zao wenyewe na wale wakiishiwa ya kuandika wao huwa wananunua na kuimba.

Kwa yeye hajaanza jana wala juzi nilivyosikia kitambo ila haweki wazi kwamba ananunua na hataki mtunzi aseme.
Sidhani kuwa anaandikiwa wakati unaona kabisa ni uandishi wake sema huwa wanasaidiwa kuandikiwa mfano mzuri msanii ambaye anaandikiwa ni nandy unajua Kuna utofauti mkubwa wa kuandikiwa na kusaidiwa kuandika ndio maana huwa hawatoi credit Mfano wimbo nasema nawe wa diamond verse ya pili aliandika Ommy dimpoz ya Kwanza ndio yeye na chorus
 
naujuaje!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

......hayo yako, na sie tujuao tunajua yetu.
ciao!
 
Wasanii wetu wanasemaje juu ya mauzo na views kwenye platform za music?

Kila mtu lazima kimrambe kwa wakati wake. Wajitahidi tu kuchukua show za CCM kwa sasa.

😅
Views wa wasanii wote wa bongo zimepungua hata diamond mwenyewe ila kwenye wimbo kufanya vizuri zinafanya kiasi chake
 
Kuna neno nilitaka kukupa ila kwa heshima nimeamua kuliacha tu!
.... ....
Huwa mnakera kila kitu mnataka mgeuze kiwe cha kisiasa we mbona kazi uachi ili usapoti vizuri harakati?ili ni jukwaa la burudani we unaingiza siasa ni ushamba huo kwani siasa si Lina jukwaa lake
 
Najitolea kukuchangia jembe ukalime tu

Hakuna wimbo hapo uchafu tu
 
si ni ukweli alipakwa wese?
Kwahiyo kusema hivyo ndio kutanifanya nikasirike nani kakudanganya? Mimi huwa sijawahi kuumizwa kwa matusi kabisa. Mimi nimekushauri kwa Nia njema sio kila Jambo ni kuingiza siasa na ndio maana kukawekwa humu majukwaa
 
okay sawa. Jadili na wenzio, i'm out.
 
Back
Top Bottom