Ila nyie Dunia ina mambo, kuna watu kazi yao kukaa Mahakamani kusubiri wenye kesi wapate chochote!

Mama Edina

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
850
Reaction score
2,019
Yaani makubwa haya kama hujui kuna mengi ya ajabu sana kwenye hii dunia.

Kuna wakati unashangaa Lakini ndio ukweli wenyewe. Binadamu ana namna mbalimbali za kujippatia Riziki.

Utakuta vishoka. Hii ya vishoka mahakamani inatia woga. Wakati wewe unahangaika kutafuta Riziki kkwa njia zako wapo wanaoshinda mahakamani kusubiri wenye kesi walioshitakiwa, na wanaoshitaki. Kikubwa kwao ni kukusaidia kufanikisha jambo lako lier halali au haramu. Kikubwa wao waingize Chochote kitu.

Nilifanya juu chini nikaona wapo lawyer wanahakikisha kesi haiishi Ili wapate 30,000 ya nauli kila unapomhitaji. Kusimamia kesi ni jambo lingine.

Siwazuilii wanaojua mambo ya Sheria kunirekebisha lakini Kuna mengi.

Mahakamani Kuna makampuni yanafanyakaz za kumtafuta mshtakiwa au mshtaki. Inafika wakati MTU amekushtaki halafu hafiki, kampuni maalum inakutafuta, na mtafutiwaji analipa.

Wapo wengine wanakushtaki, Ili waendelee kupata pesa wanafanya kukusumbua kwenda,kirudi mahakamani Ili mradi anaamini atakuja kupata pesa wakati flan
 
Mambo ya riziki hati ndugu yangu, wengi wao wana familia na hizi familia zinawategemea na pia huwa zinawaombea kwa Mungu wafanikiwe kwenye utafutaji wao huo .
Maadamu hakuna crime Waache waendelee tu.
 
Yaani makubwa haya kama hujui kuna mengi ya ajabu sana kwenye hii dunia.

Kuna wakati unashangaa Lakini ndio ukweli wenyewe. Binadamu ana namna mbalimbali za kujippatia Riziki.

Utakuta vishoka. Hii ya vishoka mahakamani inatia woga. Wakati wewe unahangaika kutafuta Riziki kkwa njia zako wapo wanaoshinda mahakamani kusubiri wenye kesi walioshitakiwa, na wanaoshitaki. Kikubwa kwao ni kukusaidia kufanikisha jambo lako lier halali au haramu. Kikubwa wao waingize Chochote kitu.

Nilifanya juu chini nikaona wapo lawyer wanahakikisha kesi haiishi Ili wapate 30,000 ya nauli kila unapomhitaji. Kusimamia kesi ni jambo lingine.

Siwazuilii wanaojua mambo ya Sheria kunirekebisha lakini Kuna mengi.

Mahakamani Kuna makampuni yanafanyakaz za kumtafuta mshtakiwa au mshtaki. Inafika wakati MTU amekushtaki halafu hafiki, kampuni maalum inakutafuta, na mtafutiwaji analipa.

Wapo wengine wanakushtaki, Ili waendelee kupata pesa wanafanya kukusumbua kwenda,kirudi mahakamani Ili mradi anaamini atakuja kupata pesa wakati flan
Haya yote ni matokea ya mfumo mbovu wa utawala. Kila mtu atavuna mabovu ya uongozi mbovu kwa wakati na muda wake. Na kuna nyingine ambayo pengine hujui. Hakimu au Jaji anakuwa na ukaribu na wakili. Kesi inaendeshwa kiaina, wakili anawasilisha utetezi unaoonekana kama ni mzuri lakini una technical errors nyingi, hukumu inatoka, unashindwa. Aliyeshinda anatoa mgao kwa wakili, na wakili anatoa mgao kwa hakimu.
 
Ni mbya mbya sna
 
Tatizo siyo mfumo. Tatizo ni watu wasiokuwa na maadili ya taaluma zao walizosomea wakati taaluma hizo, zinahitaji crime itendeke kwanza halafu ndiyo wao waweze kujipatia kipato chao. Watu wasiokuwa na maadili waliosomea taaluma za aina hii ni tatizo kwa nchi yoyote ile duniani na si Tanzania tu, hadi siku Yesu anarudi
 
Mbona wengine tunasubiri mpate UTI
Mimi nadhani ndo maisha
Police officer anasubiri uibiwe
 
Yaani makubwa haya kama hujui kuna mengi ya ajabu sana kwenye hii dunia.

Kuna wakati unashangaa Lakini ndio ukweli wenyewe. Binadamu ana namna mbalimbali za kujippatia Riziki.

Utakuta vishoka. Hii ya vishoka mahakamani inatia woga. Wakati wewe unahangaika kutafuta Riziki kkwa njia zako wapo wanaoshinda mahakamani kusubiri wenye kesi walioshitakiwa, na wanaoshitaki. Kikubwa kwao ni kukusaidia kufanikisha jambo lako lier halali au haramu. Kikubwa wao waingize Chochote kitu.

Nilifanya juu chini nikaona wapo lawyer wanahakikisha kesi haiishi Ili wapate 30,000 ya nauli kila unapomhitaji. Kusimamia kesi ni jambo lingine.

Siwazuilii wanaojua mambo ya Sheria kunirekebisha lakini Kuna mengi.

Mahakamani Kuna makampuni yanafanyakaz za kumtafuta mshtakiwa au mshtaki. Inafika wakati MTU amekushtaki halafu hafiki, kampuni maalum inakutafuta, na mtafutiwaji analipa.

Wapo wengine wanakushtaki, Ili waendelee kupata pesa wanafanya kukusumbua kwenda,kirudi mahakamani Ili mradi anaamini atakuja kupata pesa wakati flan
Maafisa madoko hao, wengi waliwahi kufungws au kuwa maabusu kwa kesi nzito, kule ndani huwa wanafundishana techniques za kushinda kesi. Akifanikiwa anakuwa hachezi mbali na Mahakama akiwa amevaa suti Kali kuliko mawakili au mahakimu,ukijichanganya umeliwa
 
Wdau nichangie jambo hapa kwa maslahi mapana.

Kwanza pole sana Mkuu kama ulikutana na hali hiyo.

Sikatai kabisa kuwa kweli wapo watu wanaojinasabaisha na mawakili watu hawa hujulikana kama 'vishoka'.

Hawa watu wanaichafua sana taswira ya mhimili mzima wa Mahakama, hawa ni chanzo cha maovu mengi katika huu mhimili na watenda kazi wake.

Lakini nitoe elimu kidogo juu ya hili.

Kwanza hili ni kosa chini ya sheria ya mawakili. Ni kosa kwa mtu asiye wakili kufanya shughuli za kiwakili, haijalishi kama mtu huyo ana digrii au taaluma ngazi yoyote ya sheria. Ni kosa.

Sasa kama una kesi Mahakamani au Baraza la ardhi au Tume ya Usuhishi kisha ukakutana na mtu wa namna hiyo, fanya jambo moja muhimu. Muulize jina lake kamili pia mwambie akupatie namba yake ya uwakili.

akikupatia hizo taarifa mbili muhimu, fanya uhakiki kwa kuingie google kisha andika MJUE WAKILI, itafunguka tovuti ya Mahakama ya Tanzania, utaandika hilo jina au namba ya uwakili aliyokupatia. Kama ni wakili zitakuja taarifa zake ikiwa ni picha yake na kama anaruhusiwa kufanya kazi ya uwakili.

Sasa baada ya hapo, ikiwa huyo mtu ni wakili, tumia akili ya kawaida jiulize maswali juu ya weledi wake, mpime kisha ona kama unaweza kufanya kazi naye kama wakili wako. (Rahisi ni ghali).

Kama sio wakili unaweza ukamripoti hapo hapo Mahakamani kwa msajili wa mahakama kama ni Mahakama kuu au ofisi ya chama cha mawakili Tanganyika mkoa husika, au kwa njia ya mtandao. Au kituo cha polisi sababu wapo wanaotumia mihuri ya mawakili hii ni jinai

Zaidi ya yote, watanzania tuwe na desturi ya kufuata taratibu.

Hakuna wakili mwenye weledi anaweza kusababisha gharama kwa mteja wake sababu ipo namna anaweza akabeba hizo gharama wakili yeye binafsi.

Mwisho kabisa, muwe mnalipa mawakili mliowapa kazi, wapo watu hawalipi ada kwa wakili kisha anataka kazi yake ifanyike.

Hapa nieleze kuwa wakili haruhusiwi na sheria kufanya kazi kisha akalipwa baadae, hilo ni kosa linaloweza kusababisha akafungiwa leseni yake ya uwakili.

Ikumbukwe pia kuwa wakili anatoza ada na gharama kwa mujibu wa sheria ya malipo ya mawakili, na kutoza ada ndogo ni kosa kwa wakili vile vile kutoza ada kubwa bila sababu za msingi ni kosa pia.

Haya mambo yatambulike.

Siku moja nitakuja na uzi juu ya mambo yote haya.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom