Ila sisi wadada jamani...

Ila sisi wadada jamani...

Pole mkuu.. agiza mirinda barrriidi halafu relax jF kama familia yako tunakusihi uwe mtulivu wakati tunatafakari cha kufanya juu ya wadada wenye tabia hii!
 
Nimeshindwa kuvumilia akii tena..! Nitawasalimia tu hata kesho wapendwa wangu,

Leo bwana nimejitokea zangu huko duniani kwenye mihangaiko, nikafika zangu kituoni, nikasubiri daladala ya ninakoelekea, ikaja nikapanda,

Sasa tumepanda zetu kama watu kadhaa hivii, sina zangu hili wala lile, kulikuwa na seat mbili jirani kabisa na mlangoni pale, akatangulia mkaka akakaa, kisha nikafuatia mie nikakaa,

the next person kupanda akawa mdada, ila akafika pale pembeni yetu cha ajabu akasimama motionless for few seconds akanitazama kwa macho ya khasira halafu akaenda kukaa seat nyingine ya mbele yetu ipo upande wa dirishani..!

Sasa nikashindwaa, kwani this girl nimewahi ona wapi.? Ni nini mbaya naye.? Ni nini nimefanyiana naye mbona kanitazama kwa macho kama vile niliwahi patana naye sehemu.??

Nikawachana tu naye, nikachukua kisimu changu nikadumbukia JF, after a while nikaona yule mrembo akageuka then akawa ana discuss na huyo jamaa aliyeko jirani yangu kuwa washuke kituo gani..!!

Ndiyo nikaelewa, anhaaa' hawa watu kumbe wapo pamoja, nikajiambia tu huyu dada kwa lile jicho kanikata walaqhi' huyu pembeni yangu itakuwa ni kifaa yake, angekuwa brother ake asingeni maindi vile.!

Luckily, wakashuka zao baada ya vituo kadhaa, nikaona afadhali wapeleke ukuch kuch hotae wao huko mbele, (ain't jealous hata)..

Ila wadada hii wivu nyingine muwachane tu nayo, It's a public transport, ingawa ningejua they're together I swear nisinge interfere ningewapisha kabisa.!

I ain't even that mad though, Jioni njema kwenu.!
Umeanza lini kutumia Public transport??

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Daaah nlikua mm af nlipanga kukuomba namba ya simu ....anyway nipe no ako..
 
Sasa alishindwa nini kukuomba tu kistaarabu akae na mtu wake kama siti zingine zilikua wazi!
Ana akili za kitoto, msamehe tu bure dadangu
Labda sio kwa purukushani zile za Dar.....utapata wapi muda wa kuombana.

Ila mimi namwonea wivu huyo jamaa. Wadada mimi nikiwahi kwenye seat huwa wanapita wanaenda kukaa nyuma.

Kuna siku nimezuia wana na wazee kama watano kisa tu atokee mdada nikae nae...nikaambulia sifuri...

Nikaishia kumruhusu bibi na kumsaidia kupaka mjukuu wake aliyeishia kunikojolea.
 
Labda sio kwa purukushani zile za Dar.....utapata wapi muda wa kuombana.

Ila mimi namwonea wivu huyo jamaa. Wadada mimi nikiwahi kwenye seat huwa wanapita wanaenda kukaa nyuma.

Kuna siku nimezuia wana na wazee kama watano kisa tu atokee mdada nikae nae...nikaambulia sifuri...

Nikaishia kumruhusu bibi na kumsaidia kupaka mjukuu wake aliyeishia kunikojolea.
Hahahaaa pole sana. Ila sasa kwanini wadada wanapitiliza kwenda kukaa nyuma?
 
Kwa mimi hua nakaa na yoyote, sina ubaguzi kabisa. Usafiri unavyokua wa shida half nirembe kuchagua seat kwa basi, hapana aisee
Tena sisi wakaka tunaombaga seat zikose alafu ibakie option ya kupakatwa tu na ukute uko karibu yangu[emoji4]
 
Back
Top Bottom