Ilala Dar: Watoto watembea kilomita 15 kufuata elimu

Ilala Dar: Watoto watembea kilomita 15 kufuata elimu

Kabewa

Senior Member
Joined
Oct 30, 2009
Posts
136
Reaction score
56
Watoto wadogo wa shule za msingi Msongola, Yangeyange na Msongola Mpya kata ya Msongola wilaya ya Ilala waishio Chakenge Richmond, na Yangeyange wamekuwa wakipata adha kubwa ya kutafuta elimu kwa kutembea kwa zaidi ya Km 15 kwenda katika shule za Msongola, Yangeyange na Msongola Mpya ambapo shule zote tatu zimejengwa kwenye eneo moja Msongola ambapo ni zaidi ya Km 15 kutoka maeneo wanayotoka watoto hawa wadogo wenye umri mdogo wa madarasa ya awali- darasa la 7.

Licha ya umbali huo wa km 15 bado miundombinu si rafiki ambapo kuna mabonde mengi yanayofurika maji hasa vipindi vya mvua jambo linalopelekea watoto kukosa masomo nyakati za mvua

Licha ya wakazi na wananchi kufanya juhudi ya kujenga shule katika maeneo jirani bado kumekuwa na uzito mkubwa kuanza kwa ujenzi wa shule.

Tunaiomba Serikali itupie jicho maeneo haya ili kuwaondolea adha watoto wadogo wanaoteseka na adha hii kubwa.
 
Back
Top Bottom