Ilala: Kesi ya viwanja ya wanaCCM Masunga na Abdallah Bulembo yapigwa kalenda

Ilala: Kesi ya viwanja ya wanaCCM Masunga na Abdallah Bulembo yapigwa kalenda

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Kesi ya jinai inayomkabili mfanyabiashara ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UWT-CCM Wilaya ya Kinondoni, Frolence Masunga (45) mkazi wa Kimara Suka jijini Dar es Salaam imeahirishwa tena.

1583816425416.png
Kesi hiyo imetajwa kwa mara ya pili leo Machi 9,2020 ambapo ilishatajwa kwa mara ya kwanza Januari 22,2020 katika mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, inayoendeshwa na Hakimu mfawidhi Martha Mpanze.

Masunga anashtakiwa kwa Kosa la kuchukua Fedha za Abdallah Majora Bulembo, kwa njia ya udanganyifu.

Imeelezwa kuwa mnamo Disemba, 2019 katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam Masunga alipokea kiasi cha fedha za kitanzania millioni 100 kutoka kwa Bulembo kwa lengo la kumuuzia nyumba iliyopo Kinyerezi ndani ya manispaa ya ilala, ambapo baadae hakuweza kukabidhi nyaraka za nyumba hiyo kwa Bulembo hivyo nyumba hiyo kuendelea kubaki mikononi mwake.

Kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Martha Mpanze imeahirishwa ambapo imetajwa kusikilizwa tena machi 25/2020 mahakamani hapo.

1583816387614.png

MY TAKE:
Haya mambo ya Viwanja wangemalizana ndani kwa ndani kindugu na kirafiki ili kulinda heshima ya chama na Umoja wa WanaCCM. Ukizingatia Bulembo alikuwa Meneja Kampeni wa urais 2015 aliyefanikisha Magufuli kuingia Ikulu na akatunukiwa Yeye Burembo na Mwanaye Ubunge wa Viti Maalum.

Ni aibu kwa Bulembo kupeleka hii kesi Mahakamani kulinganisha na Mambo CCM iliyomfanyia. Wametoka mbali na Masunga. Kala vingi vya Masunga.
 
Mlioni 100 ilitolewaje huku kukiwa hakuna nyaraka yoyote? Inashangaza!

Mzee Tupatupa
 
Back
Top Bottom