Uchaguzi 2020 Ilani ya CCM ya 2020 inataka kujenga uwanja mwingine Dodoma?

Uchaguzi 2020 Ilani ya CCM ya 2020 inataka kujenga uwanja mwingine Dodoma?

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi jana katika uwanja wa Jamuhuri, Magufuli alifurahishwa sana jinsi watu walivyojaa ndani na nje ya uwanja hivyo kuahidi kujenga uwanja mwingine mkubwa jijini Dodoma.

Je, ilani ya CCM inasemaje kuhusu ujenzi wa viwanja vipya?
Je, uwanja ulioahidiwa na Mfalme wa Morocco umeanza kujengwa?
Je, uwanja wa Jamuhuri utavunjwa?
 
Ahadi za kutoa mambo kichwani kutegemea na muonekano wa hadhira unataka kusikia nini?!! Hapo kuna nini? Ujinga wa waafrika wengi ndio mtaji wa wana siasa!! Na ni mchakato mrefu sana kuja kubadirisha fikra hizo, na ndio maana viongozi wanajua kuwa umasikini kwa wananchi ndio silaha tosha!!! Mtu akipewa hela ya kula leo tu, ya kesho anasema mungu atajua kwani alinileta kwa makusudi yake, hawezi acha nikafa!!! Hata uyazindue vipi hayasikiiii!!!
 
Mfalme wa Morocco hajatuma pesa na sidhani Kama ataituma Tena. Ameona uelekeo wa kisiasa sio mzuri
 
Hata familia huwezi kuendesha hivi mkuu.
Yah! Hata familia inaasi ikiwa na baba wa hivi japo Angalau anaweza kujitetea kwa kujitapa kua yeye ndie analipa ada, anawalisha, anawalisha nk....
Sasa sisi ni watz tuliomwajiri tunamlipa mshahara ni lazima atuheshimu na atusikilize
 
Huo uwanja utajengwa na mkandarasi wa ujenzi wa bwawa la Nyerere.

Kwenye CSR waarabu ama wakandarasi waliahidi kutumia 2% ya pesa ya mradi kujenga vituo vya afya na elimu ila toka mwaka jana serikali inajadiliana na mkandarasi ajenge uwanja wa mpira badala ya hospitali na shule.

Mkandarasi amesema anaweza kujenga ila asilazimishwe maana uwanja haupo kwenye makubaliano yake ya awali ya matumizi ya CSR(Corparate Social Responsibility).

Hivyo serikali bado inaendelea kujadiliana na mkandarasi na kumshawishi akubaliane nao ajenga uwanja wa mpira na barabara za kuzunguka. CSR ni zaidi ya Billion 200.
 
Ahadi za kutoa mambo kichwani kutegemea na muonekano wa hadhira unataka kusikia nini?!! Hapo kuna nini? Ujinga wa waafrika wengi ndio mtaji wa wana siasa!! Na ni mchakato mrefu sana kuja kubadirisha fikra hizo, na ndio maana viongozi wanajua kuwa umasikini kwa wananchi ndio silaha tosha!!! Mtu akipewa hela ya kula leo tu, ya kesho anasema mungu atajua kwani alinileta kwa makusudi yake, hawezi acha nikafa!!! Hata uyazindue vipi hayasikiiii!!!
Uwanja unawasaidia nini watu wa kawaida wasio wacheza mpira. Wakati mwingine Magufuli huwa anafurahisha sana kwenye speech yake. Tutakuwa proud kama huduma za afya zitakuwa nzuri na zinafikika kwa kila mtanzania, tungefurahi kama nchi ingekuwa ina Democracy ili haya tunayoyaandika yaweze kufanyiwa kazi siyo tunafuatiliwa na hao TISS, Tungefurahi kuona maisha ya kila mtanzania yanakuwa bora, kazi zinaongezeka na uchumi wetu unapanda. HIZI NDEGE HAZITUSAIDII SANA, Mashirika binafsi yanaweza kununua ndege na kufanya vizuri.
 
Ahadi za kutoa mambo kichwani kutegemea na muonekano wa hadhira unataka kusikia nini?!! Hapo kuna nini? Ujinga wa waafrika wengi ndio mtaji wa wana siasa!! Na ni mchakato mrefu sana kuja kubadirisha fikra hizo, na ndio maana viongozi wanajua kuwa umasikini kwa wananchi ndio silaha tosha!!! Mtu akipewa hela ya kula leo tu, ya kesho anasema mungu atajua kwani alinileta kwa makusudi yake, hawezi acha nikafa!!! Hata uyazindue vipi hayasikiiii!!!
Hivi yule mfalme wa Morocco hakuleta pesa za uwanja
 
Inawezekana hata hao wanaoambiwa wamesahau km mfalme wa morocco aliahidi kujenga uwanja
Mkuu tuna safari ndefu sana!! Na kujinasua ni vigumu, kwani wananchi wanapofikia kujitambua huwa inafikia watawala wanaanza kuingia na woga!! Mfano nchi ya MALI, si umeona kilichotokea, kila siku bora ya jana, wamekomaa kimeeleweka japo hata anayekuja anaweza kuwa wale wale lakini ndio demokrasia hiyo!!! Sasa hapa mtu anakuambia upinzani ni sumu haionjwi!!!
 
Wakati tumeonja maisha yenye uchumi duni duu!
 
kwani Laptop na ile pesa ya kila kijiji vipi zilifika?
 
Hivi yule mfalme wa morocco hakuleta pesa za uwanja
Moroco ni third world country hana mafuta anategemea misaada na utalii.
Mfalme na Magufuli walifanya makubaliano hayo kwa sababu Tanzania kuunga mkono msimamo wa Morocco kwa swala nyeti la kutwaa jimbo hilo iliokuwa Spanish Sahara (Western Sahara) kwenye kikao cha Ummoja wa Mataifa.
No Free Lunch
 
Kwa akili kama hizi ndio mtu anaamua kununua vitu ambavyo havina manufaa kwa nchi kwani yeye anaangalia interests zake sio za umma.
 
Back
Top Bottom