Pendragon24
Member
- Aug 8, 2018
- 68
- 97
Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na propaganda inayoenezwa na wanasiasa, wafanya biashara na viongozi wengine wa serikali inayowakandamiza na kuwajaza hofu vijana wengi wa taifa hili ambazo kwa namna moja ama nyingine zimewakosesha uelekeo vijana wengi katika kupigania uhuru wao wamawazo na saa nyingine kupoteza kujiamini na kuacha kabisa ushiriki wao katika mambo mengi ya kijamii ambayo yanamchango mkubwa katika maendeleo yao kama vile zoezi la kupiga kura, mikutano ya hadhara na makongamano ya kitaifa.
Hali hiyo imepelekea mpaka jamii nzima ya kitaifa na kimataifa kukosa imani na kundi kubwa la vijana wa kitanzania wakiamini kwamba vijana wengi wa kitanzania si waaminifu, elimu zao haziwasaidii na wengine wanaenda mbali zaidi wanasema hata vyeti walivyonavyo havina maana yeyote utadhani wao wenyewe hawakupita kwenye mfumo huu wa elimu ambao leo hii wanaubeza vikali.
Taasisi husika za serikali zinafumbia macho swala hili bila kuchukua hatua yeyote hawajui vitu vya namna hii vinatengeneza chuki na hasira kubwa sana ndani ya kundi kubwa la vijana waliopo katika taifa hili.
Wengi wanaoeneza propaganda hizo sio kwamba wanajari hali za vijana wa taifa hili bali wana hofu kubwa ya kupoteza vyeo na nafasi walizonazo ambazo katika uhalisia hawazimudu kutokana na uwezo wao mdogo kitaaluma njia wanayoitumia ni kuiaminisha jamii kwamba vijana wasomi hakuna kitu ili waendelee kubaki wao kisha watoto wao waje kurithi.
Bahati mbaya iliyopo ni kwamba wapo baadhi ya vijana waliopata nafasi ndani ya taasisi na vyama vya kisiasa nchini walipaswa kukemea vikali na kuweka msimamo wa vijana katika uzushi huo lakini ajabu ni kwamba wapo kimya wamebeba misimamo ya vyama vyao na kusahau jukumu la kuwakilisha vijana wenzao katika nafasi walizonazo.
Tumejikita katika kuwatetea wajasiriamali wa kisiasa na vyama vyao na kuacha wimbi kubwa la vijana wenzetu likizama katika matatizo ya afya ya akili, ukosefu wa ajira, matumizi ya madawa ya kulevya, ushoga na usaganaji, utapeli pamoja na wizi.
Na njia pekee ya kuamka ni kuacha mara moja kutumika na wajasiriamali wa kisiasa ambao kwa siku zote wamekuwa wakiwabebesha mzigo mzito vijana wa taifa hili kwa ujira mdogo sana na saa nyingine kuingia hata matatizoni, chuki na upande fulani huku wao na familia zao wananufaika siku zote.
Tunapaswa kupaza sauti zetu na kuweka misingi kwenye matatizo yanayowakabili vijana katika kila pembe ya nchi yetu kama vile haki za vijana, ushiriki wa vijana katika vyombo mbalimbali vya kimaamuzi na uwezeshwaji kiuchumi.
Vijana wamekataliwa kila pahali pamoja na taaluma na ujuzi walionao hata hiko kinachoitwa uwekezaji hakina nguvu kwa vijana badala yake wawekezaji wakigeni kama vile wachina wamekuwa wakinufaika na rasilimali na hata kufanya kazi na uwekezaji zinazowastahili vijana wazawa.
Sasa kama vijana ni lazima tuchukue hatua ili kuwa huru kiuchumi, tunapaswa kuamka ili kuokomboa wakati wetu wa sasa na ule ujao na kujenga wakati mwingine bora kwa ajili ya vijana waliopo nyuma yetu waweze kunufaika na matunda ya nchi yao.
Kama hatutawakomboa vijana kutoka kwenye wimbi hili kubwa la ukosefu wa nafasi katika kutoa mawazo na kueleza changamoto zao zinazowakabili ipo siku vijana hawa watachoka na ukandamizaji huu na kuamua kutumia nguvu ya wingi walionao na mabavu ili kukidhi haja na mahitaji yao katika maisha yao ya kila siku, ili tusifike huko ni lazima sasa tuanze kuwapatia nafasi na kusikiliza mahitaji yao kwa umakini mkubwa.
Ili kuelekea katika TANZANIA TUITAKAYO hatuna budi kutengeneza nafasi na ushiriki wa vijana katika maendeleo ya taifa kwani tusipofanya hivyo mbeleni kuna hatari kubwa sana ya vijana kutumia uwingi wao kutafuta haki zao wenyewe, hizi ni baadhi tu ya njia zinazoweza kutumika ili kuchochea ushiriki wa vijana katika nafasi ndani ya taifa lao.

- Ni lazima kuwa na ilani ya taifa ya vijana itakayobeba mustakabali wa pamoja wa haki na maendeleo ya kweli ya vijana na kuchagua viongozi watakao kuwa tayari kuitekeleza.
- Wabunge na madiwani lazima wawe na ukomo kama ilivyo kwa Raisi ili kutengeneza nafasi kwa vijana kugombea na kuleta mawazo mbadala.
- Uwepo wa walau asilimia 15 au zaidi wa uwakilishi wa vijana katika nafasi za uongozi kama ilivyo kwa wanawake na makundi maalumu.
- Nafasi za ajira katika miradi kama vile migodini,mbuga za wanyama,utalii,viwanda na uwekezaji wowote mkubwa ni lazima asilimia walau 30 za nafasi za juu na za kawaida zichukuliwe na vijana hasa wazawa wa eneo husika.
- Kuwepo kwa muda maalumu wa watumishi kustaafu hii itasaidia ongezeko la vijana wengi kupata nafasi katika ofisi tuachane na miaka sitini au hamsini, mtumishi akikaa miaka 20 au 25 katika taasisi inatosha.
- Pasiwepo na kujirudia rudia kwa watu fulani peke yao katika nafasi kila awamu pasipo ufanisi badala yake wapishe mawazo mapya kwa kuwaachia watu wengine hasa vijana kushika nafasi hizo.
- Pasiwepo na kuamishwa amishwa kwa nafasi badala yake mtu akishindwa kuwajibika ipasavyo katika nafasi moja aondolewe ili kutoa nafasi kwa wananchi wengine kushika nafasi hizo hasa vijana ili kupata maono na mitazamo mipya ya utendaji kazi.
- Kupunguza idadi kubwa ya watu wasio wazawa katika taasisi ili kuchochea nafasi na ushiriki wa vijana katika uwekezaji, biashara na utumishi.
- Viongozi wa umma wenye nafasi zaidi ya moja wanapawsa kupunguziwa nafasi hizo ili watu wengine hasa vijana wapate nafasi ya kuleta mawazo mbadala.
- Kitendo cha Jamii fulani kutumia majina ya ukoo na ukabila zao ili kupata nafasi kuna wanyima vijana wengi nguvu ya ushiriki katika kujitokeza na kugombea nafasi mbalimbali.
- Kuwapunguzia makodi,usumbufu na urasimu kwenye shughuli mbalimbali zilizowekezwa au zitakazowekezwa na kundi kubwa la vijana kama vile uwakala, michezo,ubunifu,umachinga,mama ntilie,bodaboda na udereva.
- kuruhusu mgombea binafsi na kupunguza umri wa kugombea nafasi ya uraisi walau miaka 35 ili kuongeza ushiriki wa vijana katika nafsi na shughuli za jamii na nchi kwa ujumla.
Upvote
0