Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
UTEKELEZAJI WA HII ILANI NA SIFA ZA KIONGOZI
Serikali itakayoongozwa na NCCR-Mageuzi itaweka mkazo katika kuimarisha mifumo ya kiutendaji ya serikali kuu na serikali za mitaa ili ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani uwe wenye tija kwa umma wa watanzania. Serikali itahakikisha usimamizi wa miradi ya serikali unafanywa kwa uwazi, uadilifu na kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria, na mipango mbalimbali ya maendeleo hasa ile ya maendeleo endelevu ya dunia (2015-2030), dira ya taifa 2025 na ajenda ya Africa 2063.
Serikali hiyo itaongozwa na Watanzania wenye uwezo wa:
NCCR-Mageuzi inaamini katika utawala wa kisheria, na uongozi shirikishi katika kujenga maendeleo endelevu katika jamii kwa kutumia itikadi ya UTU. Lengo kuu la kuanzishwa kwa chama chetu lilikuwa ni kupata Katiba Mpya, kama kiini cha kujipangia taratibu zenye kuleta maendeleo kwa wote. Maendeleo yenye kulinda UTU wa kila mtanzania na uhai wa mazingira yetu.
Takwimu za kimataifa za mwaka huu kuhusiana na furaha ya mwanadamu, Tanzania tumeshika namba ya 153 kati ya mataifa 156 . Furaha ya mwanadamu inaanzia katika kupata mahitaji msingi kulingana na mazingira aliyomo.
Hapa kwetu mahitaji hayo ni Afya njema, Uhuru wa kujiamulia, na fursa ya kujipatia kipato. Afya njema hutokana na kujipatia chakula bora na cha kutosha, maji safi na salama, malazi na makazi bora. Uhuru wa kujiamulia umejikita katika haki ya kutoa mawazo na haki ya kujumuika kwa sababu mbalimbali bila ya kuvunja sheria. Fursa ya kujipatia kipato inaanzia katika haki ya kupata elimu bora iliyo sawa kwa wote, mifumo ya uchumi iliyo rafiki kwa wafanyibiashara na isiyo na ubaguzi wa aina yoyote kama ilivyoanishwa katika Kati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mikataba mbalimbali tuliyoridhia ya kikanda, kibara na kimataifa.
Kwa kuzingatia hayo, agenda zetu katika uchaguzi huu ni kama ifuatavyo:

- Kusimamia zaidi maslahi ya mama Tanzania akiwa popote, ndani au nje ya nchi;
- Kusimamia na kutetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kulinda haki za binadamu;
- Kuzuia upitishwaji wa sheria mbovu zinazokandamiza haki za watu;
- Kuwa wazi katika utendaji kazi wa serikali na anayethamini katika dhana dhana ya ushirikishwaji wa wananchi katika mipango ya maendeleo ya umma ;
- Kuamini katika maendeleo shirikishi yenye kuinua uchumi na kuweka mazingira bora ya ajira;
- Kuwajibika na kuwa tayari kufanya maamuzi magumu yenye tija kwa taifa letu kwa kuwawajibisha viongozi wengine wanaposhindwa kutimiza majukumu yao;
- K Kusimamia utekelezwaji wa miradi ya maendeleo kwa umakini
- Kuwa mahiri katika kusimamia rasilimali za nchi yetu ikiwemo kupinga mikataba isiyo na tija kwa taifa;
- Kukataa kupokea au kutoa rushwa, na kuwa tayari kuondoa mifumo ya rushwa na ubadhirifu nchini;
- Kuthamini kwa dhati misingi ya usawa wa kijinsia kwa mapana yake;
- Kusimamia na kutetea maslahi ya watu anaowaongoza
NCCR-Mageuzi inaamini katika utawala wa kisheria, na uongozi shirikishi katika kujenga maendeleo endelevu katika jamii kwa kutumia itikadi ya UTU. Lengo kuu la kuanzishwa kwa chama chetu lilikuwa ni kupata Katiba Mpya, kama kiini cha kujipangia taratibu zenye kuleta maendeleo kwa wote. Maendeleo yenye kulinda UTU wa kila mtanzania na uhai wa mazingira yetu.
Takwimu za kimataifa za mwaka huu kuhusiana na furaha ya mwanadamu, Tanzania tumeshika namba ya 153 kati ya mataifa 156 . Furaha ya mwanadamu inaanzia katika kupata mahitaji msingi kulingana na mazingira aliyomo.
Hapa kwetu mahitaji hayo ni Afya njema, Uhuru wa kujiamulia, na fursa ya kujipatia kipato. Afya njema hutokana na kujipatia chakula bora na cha kutosha, maji safi na salama, malazi na makazi bora. Uhuru wa kujiamulia umejikita katika haki ya kutoa mawazo na haki ya kujumuika kwa sababu mbalimbali bila ya kuvunja sheria. Fursa ya kujipatia kipato inaanzia katika haki ya kupata elimu bora iliyo sawa kwa wote, mifumo ya uchumi iliyo rafiki kwa wafanyibiashara na isiyo na ubaguzi wa aina yoyote kama ilivyoanishwa katika Kati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mikataba mbalimbali tuliyoridhia ya kikanda, kibara na kimataifa.
Kwa kuzingatia hayo, agenda zetu katika uchaguzi huu ni kama ifuatavyo:
- Katiba Mpya
- Elimu
- Muafaka wa Kitaifa
- Afya na Ustawi wa Jamii
- Mazingira na Makazi
- Uchumi (Ardhi, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mifugo, Viwanda, Biashara, Madini, Nishati, Maliasili na Utalii, Sanaa, Utamaduni na Michezo, na Miundombinu ya usafiri)
- Ulinzi, Usalama, na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
- Masuala Mtambuka (Rushwa, na Makundi Maalumu