Ilani za uchaguzi za vyama sio "serious documents" kuongoza nchi katika maendeleo

Ilani za uchaguzi za vyama sio "serious documents" kuongoza nchi katika maendeleo

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Tanzania haihitaji kuchagua kiongozi wala kuongozwa na ilani ya chaguzi ya chama bali sera chache za kimkakati za kitaifa zilizoandaliwa kwa makini na wataalam wenye uzoefu wa eneo husika.

Badala ya ilani ya uchaguzi ya chama inayoorodhesha kila kitu kutoka ngoma, uganga n.k mpaka mambo ya Simba na Yanga, MGOMBEA anapaswa kuandaa sera mbili au tatu kwa kina namna atakavyofanya kutatua matatizo ya msingi ya nchi na sio kuja na kakitabu kamoja cha chama kalichorundikwa vita atakavyofanya akipewa madaraka.

Taifa letu kiuhalisia linachagua watu na sio chama kuongoza nchi kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa. Kitabu cha kurasa kadhaa ambacho kina orodha ya mambo chungu nzima yanayaposwa kufanyiwa kiza hakiwezi kuwa muongozo makin wa nchi, ni hadaa na mbwembwe za wanasiasa tu.
 
Back
Top Bottom