Leo ni tar 28/10/2013
HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA
SHULE YA SEKONDARI ILBORU
UTARATIBU WA KUFUATWA ILI MWANAFUNZI AWEZE KUPOKELEWA SHULENI BAADA YA SHULE KUFUNGWA (17.09.2013)
A) Sambamba na sheri,kanuni na taratibu za shule mwanafunzi anatakiwa kukubali kuwa;
1. Hatapatikana nje ya shule bila kibali cha Mkuu wa Shule ikiwa ni pamoja na kutokuonekana katika nyumba za watumishi bila kibali cha Mkuu wa shule.
2. Usafi shuleni ni jukumu la kila mwanafunzi tangu kidato cha 1-6,na badiliko lolote litatokana na uamuzi wa Mkuu wa shule.
3. Mfanyakazi yeyote wa shule bila kujali jinsia ataingia Bwenini bila kizuizi cha mwanafunzi yeyote.
4. Mwanafunzi atapangiwa na mwalimu husika darasa na bweni na kuwajibika kutii sheria na kanuni zilizopo shuleni kama ilivyoambatanishwa.(Kiambatisho cha 2)
5. Hakuna Mwanafunzi atakayeruhusiwa kumiliki chumba ama ofisi shuleni.
6. Ni marufuku mwanafunzi kufanya marekebisho yoyote ya miundombinu ya shule.
7. Katika ukaguzi wowote shuleni mwanafunzi yoyote yuko chini ya mamlaka akaguliwe na mtumishi yeyote wa shule.
8. Mwanafunzi akubali kula chakula kitolewacho shuleni kulingana na uwezo na maelekezo ya serikali.
9. Sare ya shule inayotakiwa kwa mwanafunzi anayetakiwa kurejea shuleni izingatie vipimo na isibanwe wala kuongezwa mtindo tofauti na maagizo ya masharti ya kujiunga na shule. (suruali upana chini iwe kati ya inchi 17-18)
10. Kila mwanafunzi awajibike binafsi kutoshiriki kikao ama mkutano wowote au matangazo yasiyo na kibali cha mkuu wa shule.
11. Ni marufuku mwanafunzi kutohudhuria darasani,kutokufanya ama kugomea mtihani ama masomo.
12. Hairuhusiwi mwanafunzi kubaki shuleni wakati wa likizo au amri ya kuondoka shuleni.
13. Mwanafunzi haruhusiwi kujadili au kuhoji maamuzi halali iliyofikiwa na vikao vya wafanyakazi,uongozi wa shule ama bodi ya shule.
14. Ni marufuku mwanafunzi kumkataa mwalimu,kukataa kufanya kazi darasani.
15. Ni makosa makubwa kuchelewa kurudi shuleni kutoka likizo.
16. Mwanafunzi atapokewa akiwa amelipa ada na michango yote ya shule. Pamoja na wale wanaolipiwa na Halimashauri
17. Makosa yafuatayo adhabu yake ni kufukuzwa shule.
1; Wizi 2;Uasherati,ubakaji,ushoga 3;Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya 4;Uvutaji wa bangi 5; Makosa ya jinai 6; Kupigana au kupiga 7; Kuharibu kwa makusudi mali ya umma. 8; kudharau bendera ya Taifa 9; Kuoa 10;Kusababisha mimba ndani na nje ya shule 11; Kushiriki kutoa mimba 12;Kugoma kuchochea na kuongoza ama kuvuruga amani na usalama wa shule 13; Kukataa adhabu 14; Kukamatwa na simu shuleni.
Hayo ndio masharti bodi ya shule kongwe ya Ilboru imeweka kwa wanafunzi wao.
Wanafunzi wote wamerejea shuleni na vipengele hivyo leo.
Nitarudi!
Copy kwa
kifumbiko lane