Ile taasisi ya kimataifa inayofanya utafiti kuhusu furaha za wananchi wa mataifa mbalimbali ije baada ya miezi sita

Ile taasisi ya kimataifa inayofanya utafiti kuhusu furaha za wananchi wa mataifa mbalimbali ije baada ya miezi sita

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Wapendwa Heri ya Mapumziko ya Pasaka.
Poleni Watanzania wenzangu kwa kumpoteza kipenzi chetu,
Wanawake hongereni kwa kutuongoza,
napendekeza kuanzia Leo na nyinyi fanyeni mageuzi,anzeni kututongoza sisi wanaume,tupeni of mbalimbali na Mambo Kama hayo.
Nauliza hivi ile taasisi ya Kimataifa inayofanyaga utafiti kujua Ni nchi gani wananchi wake wana furaha Sana hapa duniani na nchi gani wananchi wake hawana furaha kabisa hapa duniani,ambapo miaka miwili iliyopita Tanzania ilishika nafasi ya tatu kutoka mwisho kama sijakosea,naomba Kama Kuna mwenye kunbukumbu sahihi aliweke sawa hili.

Naomba taasisi hiyo ije miezi sita Kutokea mwezi huu wa nne kuona Kama Pengine labda mabadiliko ya uongozi wa nchi yatatupandisha chati,mabadiliko ninayoyasemea Ni mabadiliko ya kutoka kutongozwa na wanaume na Sasa tunaongozwa na Mwanamama,Kama inavyojulikana Mama wana upendo,wapole,wanna utu,huruma,faraja,kudekeza n.k.
Pengine chati yetu ya furaha itapanda.

Simba wao wameshamaliza yao, wao wanatupandisha chati Kila Mara
Samahani Sana kwa watani.
Sasa Ni zamu ya furaha za wananchi, je furaha zetu Watanzania zimepanda?au Ni Kama miaka miwili iliyopita?
Kama mnavyojua tumepata bahati ya kuwa na Rais Mzuri kwa sura,sauti nzuri,anaongea vizuri,macho mazuri,roho nzuri,haiba nzuri na siha nzuri
Huenda furaha ikaongezeka.
Msininukuu vibaya.
 
Back
Top Bottom