Ileje: Binti Mjamzito auawa kwa kuchomwa Kisu na Mwili wake kuchomwa Moto

Aiseee inashangaza Sana, Mimi nilidhani kwa makosa makubwa Kama hayo (Kuua na Kulawiti/Kubaka) wanawekwa kwanza kwenye hizo jela za watoto wakifikisha miaka 18 wanahamishwa gereza la wakubwa kuendelea na kifungo kumbe ni tofauti!!!

Ndio maana Lulu wa Kanumba alipigwa miaka miwili sababu alikua na 17 wakati tukio linatokea.
Kilicho mfanya Lulu afungwe miaka miwili Ni Kwa Sababu alidanganya umri wake kituo cha polisi akisema ana miaka Kumi Na nane Kwa Sababu alikuwa Na leseni ya driving mean she was driving so nadhani aliogopa kusema ana miaka 17 angeulizwa leseni kaipataje vinginevyo angefungwa kifungo cha nje miaka miwili ma sio cha ndani.

Hiyo sheria inatakiwa kufanyiwa marekebisho haraka iwezekanavyo
 
miaka 18 ni mpango wa Shetani mtoto wa kike anabarehe akiwa na miaka 9 na wa kiume miaka 14 hayo mambo ya eti mtoto anaitwa mtu mzima akiwa na miaka 18 sio mpango wa Mungu

Mungu yupi huyo?

Nitajie mahali huyo Mungu aliposema au andika kuwa mtu wa umri uliotaja anatakiwa kuoa na kuolewa..
 
16 + 16 = 32 - 2 (miaka ya kuishi kinyumba) = 30 (jela)

Nawaza kwa nini mara nyingi wanapolingana umri wenza huwa huishia kugombana gombana etc

Huyu Dogo Kama Mie nagawa miaka 30 Kwa wazazi pande zote Na Dogo, 30 divide by 5, they get 6 years each!
 
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe, Subira Kibona(16) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha mwili wake kuchomwa moto na anayesadikika kuwa mume wake, Shukrani Kamwela (16) kabla ya kutupa mabaki ya mwili huo kwenye korongo.

Kamada wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, ASP Janeth Magomi, akizungumzia tukio hilo jana, amesema walipokea taarifa za tukio hilo juu ya mwanamke huyo ambaye alipotea nyumbani tangu Januari 13, mwaka huu.

ASP Magomi amesema baada ya kutoonekana kwa marehemu huyo wananchi walifanya juhudi za kumtafuta ndipo walipokuta mwili wake ukiwa umetupwa katika korongo lililopo katika moja ya pori mkoani humo huku ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kuchomwa moto.

Hata hivyo, ASP Magomi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kuchunguza na tayari linamshikilia mtuhumiwa.

Diwani wa kata hiyo, Yotamu Ndile, amesema mume wa marehemu kumwambia mke wake waende kwa Mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya tumbo maarufu kama kata kamba kwani marehemu alikuwa na ujauzito wa miezi saba.

Aidha, akizungumza na wananchi wa eneo la tukio Afisa Tarafa ya Bulambya, Joyce Chale amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na hofu ya Mungu kwani jamii inapaswa kutoa elimu kwa vijana namna ya kutatua migogoro inayojitokeza kwenye ndoa na si kukatisha uhai mtu ambaye nitegemezi kwa taifa.

Afisa huyo amewataka wananchi hao kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za matukio kwani jeshi hilo linafanya kazi kwa kushirikiana na wananchi kwa lengo la kuwakamata waharifu na kuondoa dhana ya pindi wakitoa taarifa watakamatwa.

Aidha, amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwafanya watoto wa kike kama kitega uchumi bali wawapeleke shule ili kuepusha ndoa za utotoni.

Imeelezwa kuwa tukio hilo limekuwa la pili kutokea kijijini hapo la wanawake kuchomwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni kisu huku wananchi wakiomba serikali kuchukua hatua za makusudi kukabili hali hiyo.

Malunde blog
Mimi nina swali tu, Tangu lini RPC Akawa na cheo cha ASP (Assistant Superintendent). Nyota 3

Ni makosa ya uhandishi au ni kweli??
 
Wote wana umri wa miaka 16. Naliona tatizo hapa Kwa hawa watoto kuoana badala ya kuwa shuleni. Mtoto wa kivulana hakuwa tayari kutunza hiyo mimba na kitoto ambacho kingezaliwa. Ila suluhisho alilochukua si la busara. Ataishia lupango na baada ya miaka mitatu kesi itaanza kuunguruma.
 
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe, Subira Kibona(16) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha mwili wake kuchomwa moto na anayesadikika kuwa mume wake, Shukrani Kamwela (16) kabla ya kutupa mabaki ya mwili huo kwenye korongo.

Kamada wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, ASP Janeth Magomi, akizungumzia tukio hilo jana, amesema walipokea taarifa za tukio hilo juu ya mwanamke huyo ambaye alipotea nyumbani tangu Januari 13, mwaka huu.

ASP Magomi amesema baada ya kutoonekana kwa marehemu huyo wananchi walifanya juhudi za kumtafuta ndipo walipokuta mwili wake ukiwa umetupwa katika korongo lililopo katika moja ya pori mkoani humo huku ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kuchomwa moto.

Hata hivyo, ASP Magomi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kuchunguza na tayari linamshikilia mtuhumiwa.

Diwani wa kata hiyo, Yotamu Ndile, amesema mume wa marehemu kumwambia mke wake waende kwa Mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya tumbo maarufu kama kata kamba kwani marehemu alikuwa na ujauzito wa miezi saba.

Aidha, akizungumza na wananchi wa eneo la tukio Afisa Tarafa ya Bulambya, Joyce Chale amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na hofu ya Mungu kwani jamii inapaswa kutoa elimu kwa vijana namna ya kutatua migogoro inayojitokeza kwenye ndoa na si kukatisha uhai mtu ambaye nitegemezi kwa taifa.

Afisa huyo amewataka wananchi hao kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za matukio kwani jeshi hilo linafanya kazi kwa kushirikiana na wananchi kwa lengo la kuwakamata waharifu na kuondoa dhana ya pindi wakitoa taarifa watakamatwa.

Aidha, amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwafanya watoto wa kike kama kitega uchumi bali wawapeleke shule ili kuepusha ndoa za utotoni.

Imeelezwa kuwa tukio hilo limekuwa la pili kutokea kijijini hapo la wanawake kuchomwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni kisu huku wananchi wakiomba serikali kuchukua hatua za makusudi kukabili hali hiyo.

Malunde blog
Nlijua jamaa mchaga
 
Kilicho mfanya Lulu afungwe miaka miwili Ni Kwa Sababu alidanganya umri wake kituo cha polisi akisema ana miaka Kumi Na nane Kwa Sababu alikuwa Na leseni ya driving mean she was driving so nadhani aliogopa kusema ana miaka 17 angeulizwa leseni kaipataje vinginevyo angefungwa kifungo cha nje miaka miwili ma sio cha ndani.

Hiyo sheria inatakiwa kufanyiwa marekebisho haraka iwezekanavyo
Ile ya lulu ilikuwa manslaughter,

Lakini kwa kesi kama ya huyu kijana watamhukumu kwa kuangalia sheria inayomlinda mtoto
,
Ijapo pia wataanagalia uhatari wake kama wakimwachia maana anaweza enda kuua tena
 
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe, Subira Kibona(16) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha mwili wake kuchomwa moto na anayesadikika kuwa mume wake, Shukrani Kamwela (16) kabla ya kutupa mabaki ya mwili huo kwenye korongo.

...
... kwa context hiyo huyo sio mwanamke; ni msichana.
 
Hahahaaa hili tukio lingekuwa limetokea Kilimanjaro, sasa hiv ingekuwa wachaga wana roho mbaya sana, hawafai kabisa,

Uhalifu upo kila mahali kwa kila kabila,!!
 
Sheria ya Watoto ya mwaka 2009 ya kijinga Sana mtuhumiwa mwenye umri wa miaka chini ya

Kumi Na nane Ni Mtoto Na anahukumiwa kwenye mahakama ya Watoto Na adhabu yake mara nyingi huwa maximum miaka miwili nje ya gereza. Niliwahi shuhudia Dogo dereva wa Lori ana miaka 17 kamlawiti Mtoto WA miaka miwili halafu akafungwa miaka miwili kifungo cha nje.

It is high time now sheria ibadilishwe HII kuwe Na categories za umri WA watoto.

This kid Must be given a life he was so cold
Lakini pia anaweza kushitakiwa kama mtu mzima. Yaani ameoa halafu ashitakiwe kama mtoto!
 
Mungu yupi huyo?

Nitajie mahali huyo Mungu aliposema au andika kuwa mtu wa umri uliotaja anatakiwa kuoa na kuolewa..
mimi sijasema kuoa au kuolewa nimesema kubarehe ...
kama hujui kiswahili rudi shule
 
Back
Top Bottom