Ileje: Binti Mjamzito auawa kwa kuchomwa Kisu na Mwili wake kuchomwa Moto

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe, Subira Kibona(16) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha mwili wake kuchomwa moto na anayesadikika kuwa mume wake, Shukrani Kamwela (16) kabla ya kutupa mabaki ya mwili huo kwenye korongo.

Kamada wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, ASP Janeth Magomi, akizungumzia tukio hilo, amesema walipokea taarifa za tukio hilo juu ya mwanamke huyo ambaye alipotea nyumbani tangu Januari 13, mwaka huu.

ASP Magomi amesema baada ya kutoonekana kwa marehemu huyo wananchi walifanya juhudi za kumtafuta ndipo walipokuta mwili wake ukiwa umetupwa katika korongo lililopo katika moja ya pori mkoani humo huku ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kuchomwa moto.

Credit: Millard Ayo

Wakuu ngapi ngapi hadi sasa?
 
Ishaletwa humu hii mkuu, uzi wake upo...

 
Ishaletwa humu hii mkuu, uzi wake upo...



 
Ila miaka 16. Duuh!
 
ASP n cheo ambacho mtu hawez kuwa kamanda wa mko labda n ACP

ASP ..

SP

SSP

ACP

Kama sikosei mtiririko upo hivyo
 
kubarehe ❌ kubalehe ✅
kishwahili❌ kiswahili✅
hizo ni typing errors cha msingi umeelewa nachomanisha ...

ukitaka uamini hao ni watu wazima angalia wamefanya matukio ambayo hata wewe inawezekana huwezi kufanya.

hapo ndio utajua Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…