Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Baada ya kuona matamanio ya baadhi ya watanzania juu ya kuwa na kizazi cha Gen Z kama cha Kenya, nimejikuta najiuliza ni kwa nini tuwatamani vijana wa kenya wakati na sisi tuna vijana wetu wasomi kama wao!?
Lakini pia huwa humu kunakuwa na mijadala ya jinsi vijana wa China walivyoiendeleza nchi yao kupitia Elimu ya Teknolojia waliyo nayo.
Hapa kwetu, watunga na wapanga sera wetu ambao ni wanasiasa, wana mchango gani kwenye kuifanya Elimu yetu iwe bora ili ichochee ukuaji wa uchumi wetu na maendeleo ya kijamii kwa ujumla!?
Je, unaona kwa kiasi gani wanasiasa wetu wanajishughulisha na kujali ubora wa Elimu yetu?