Ili jamii iweze kuendelea kiuchumi, wizi ni lazima. Efficient Market Mypothesis (EMH) haipo na wala hai-exist

Ili jamii iweze kuendelea kiuchumi, wizi ni lazima. Efficient Market Mypothesis (EMH) haipo na wala hai-exist

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
2,650
Reaction score
4,065
Ukiona rais anayeingia madarkani anasema atakomesha wizi huyi ni mwongo wala ukweli haumo ndani yake.

Hata Mungu amesharuhusu wizi pale aliposema mwenye nacho ataongezewa na asiyenacho hata kile anachoamini anacho atanyanganywa (ataibiwa)
 
Ukiona rais anayeingia madarkani anasema atakomesha wizi huyi ni mwongo wala ukweli haumo ndani yake.
Kwa ujumla wanasiasa wote ni waongo, hawastahili kuongoza nchi wala kijiji
 
Huu uzi nhauna ukweli. Nchi zilizo na maendeleo makubwa, wizi ni kwa kiwango kidogo sana. Umaskini ndio chanzo cha wizi na ukiukwaji za haki za wato.
 
Ukiona rais anayeingia madarkani anasema atakomesha wizi huyi ni mwongo wala ukweli haumo ndani yake.

Hata Mungu amesharuhusu wizi pale aliposema mwenye nacho ataongezewa na asiyenacho hata kile anachoamini anacho atanyanganywa (ataibiwa)

Evidence is contrary to what you are proposing. Nchi zenye wizi kidogo sana kama Finland na Sweden na Norway, nimetoka huko majuzi, zimeendelea saana kuliko Nchi zenye wizi mwingi kama Bongo, Congo, Kenya.

Kule nilikuwa nahisi barabara wamejenga mpaka wakapitiliza, yaani Barabara mbele, kushoto, kulia magari yana move all directions.

Nilikuwa nje ya Nchi kama wiki 6 hivi, nje ya mji km 30 hivi, fikiria Bunju, lakini ilinichukua dakika chini ya 20 kufika mjini Kila siku. Barabara ziko designed kiasi kwamba magari yanatembea Kila mahali!

Kuna Mabasi, treni, metro, na trams Kila uelekeo! Hii treni tunashangilia Sasa hivi ni kitu Cha Karne iliyopita kwao!

Ukiumwa ghafla unapiga simu ambulance inakuja unawahishwa hospitali, unatibiwa kwanza. Ukipona bill yako itakukuta nyumbani baada ya wiki mbili. Na itakuwa kubwa au ndogo kulingana na kipato chako. Balance Serikali inalipa. Yes, wanajua kipato chako kwani hakuna za wizi.

Watoto wanakula chakula shuleni kuanzia kindergarten mpaka university. Watoto wa sekondari mpaka chini ni bure, watoto wa high school na University Wana bei zao zilizo na ruzuku. Chakula kinakuwa bora kabisa, sio kama huku kwetu Canteen ya Waalimu ni tofauti na ya Wanafunzi utafikiri miili Ina mahitaji tofauti. Sisi ni taifa linalowanyima watoto chakula shuleni, kwasababu ya wizi.

Mwalimu kule anasoma mpaka Masters. Awe wa kindergarten au high school, alichosomea anasoma mpaka Masters. Mshahara uko juu. Sisi Mwlimu ni yule aliyefeli form 4 na 6 na akapelekwa chuoni! Angalau siku hizi DUCE wanatoa Wenye degree.

Sisi tunanunua mashangingi ya Serikali kuliko Serikali ya Sweden wanaotupa misaada! Toyota Japan wanashukuru sana kuwepo kwa wa Afrika sisi!!

Ukienda Nchi za watu ukaona system zinavyofanya kazi, utagundua Efficient Markets do exist, ila si kwa mtu mweusi! Sisi bado sana, na kibaya zaidi rumeanza kuamini haiwezekani!!!
Itafika mahali vizazi vya mtu mweusi vitachoka, vitasema no, we can be efficient.

Ni kweli walio nacho wanaongezewa, nilikutana na vi hotpot vya delivery vinatembea vyenyewe barabarani, robots! Nikajiuliza: sisi wabongo tunaosema wizi ni lazima si tutakiiba njiani?😂 Kwanza barabara za chenyewe kupita hatuna, hata Masaki ni mashimo hakiwezi kupita!. Kumbuka nimekwambia barabara wamejenga mpaka wamepitiliza.

Sisi wa Afrika tunaibiwa; tunanyang'anywa hata kidogo tukicho nacho, kwa uzembe wetu wenyewe kwasababu hatuna teknolojia, na hata uendeshaji wa tulicho nacho hatuwezi, tunaweza tukazidiwa ujanja hata kwenye mikataba! Kwa hiyo unaposema asiye nacho hunyang'anywa hata kidogo alicho nacho hujakosea, sema ulikuwa hujang'amua kuwa huyo anaye nyang'anywa ni wewe!!

Watakabahu!
 
Pale aliposema aliyenacho ataongezewa na asiyenacho hata kile anachodhani anacho basi atanyanganywa which means ataibiwa.

Pia soma:
Mungu alitumia lugha laini sana kuwaambiwa kuwa tajiri au mwenye hela ana uhalali wa kumuibia asiyenacho

Mwenye akili na aelewe.
 
Huna sababu ya kupindisha maandiko ya Mungu kwa masilahi yako hapa jamvini, ili uonekane mchekeshaji au unajua kitu.

Cha muhimu ni kustable kwenye Imani yako na kuikiri Imani kwa kinywa chako hakuna sababu ya kujitafutia laana
 
Hakuna contradiction hapo. Ni either akili yako ndogo au huna akili kabisa. Au labda unajitoa akili makusudi.
Sasa alikuwa na maama gani kusema mwenye ambaye hana kitu hata kile alicho nacho atanyanganywa? Huoni huo ni wizi. Think beyond
 
Pale aliposema aliyenacho ataongezewa na asiyenacho hata kile anachodhani anacho basi atanyanganywa which means ataibiwa.

Mungu alitumia lugha laini sana kuwaambiwa kuwa tajiri au mwenye hela ana uhalali wa kumuibia asiyenacho

Mwenye akili na aelewe.
Hapo inaongelewa utajiri wa imani na sio mali.
 
Pale aliposema aliyenacho ataongezewa na asiyenacho hata kile anachodhani anacho basi atanyanganywa which means ataibiwa.

Mungu alitumia lugha laini sana kuwaambiwa kuwa tajiri au mwenye hela ana uhalali wa kumuibia asiyenacho

Mwenye akili na aelewe.
Unaongelea kitu gani? Mungu ni nani? Una ID yake na picha utuonyeshe?

Je aliongea hayo lini? Unaweza kutupa tarehe?
 
Pale aliposema aliyenacho ataongezewa na asiyenacho hata kile anachodhani anacho basi atanyanganywa which means ataibiwa.

Mungu alitumia lugha laini sana kuwaambiwa kuwa tajiri au mwenye hela ana uhalali wa kumuibia asiyenacho

Mwenye akili na aelewe.
Kwa macho ya kiroho , andiko Mathayo 13:12 lina fundisha kuwa na shukrani ( gratitude) kwa Mungu sio wizi kama unavyopotosha .
 
Back
Top Bottom