Ili kuboresha soka nchini Tanzania , Simba na Yanga " ziuawe " ni mbovu mno !

Ili kuboresha soka nchini Tanzania , Simba na Yanga " ziuawe " ni mbovu mno !

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nimesikitishwa sana na kiwango kibovu cha soka kilichoonyeshwa na timu hizi kwenye game ya jana , ni aibu sana kwa timu hizi zinazosemekana zinafundishwa na makocha wa kigeni .

ili soka la Tanzania lipande hizi timu ni lazima zihujumiwe na zitokomezwe , ni mfano mbaya sana kwa vijana wanaochipukia ambao kila kukicha wanawaza kuchezea timu hizi mbovu , kwa tamaa ya vijihela vidogo sana wanavyolipwa

Timu yangu ya Simba ndio iliyonisikitisha zaidi , ilishindwa kutumia pengo la red card ya Yanga kuongeza magoli , nadhani wachezaji wazee ndio tatizo , sasa kwa uchezaji ule ni kipi cha kujivunia kuwa na kocha eti wa kifaransa ? mbona hana tofauti na Jamhuri Kiwelu , Mziray , Kataraia Minziro au Sunday Kayuni ?

Game ya Simba VS Yanga siku hizi haina tofauti na Ndondo cup , ambapo sasa vituko vya nje ya uwanja vinaburudisha zaidi kuliko dimbani .

Poor Simba na Yanga !
 
Mkuu mpira siku hizi Bongo hakuna, mimi nimeacha kwenda uwanjani muda mrefu sana. Viwango vinavyoonyeshwa na wachezaji wetu kwenye ligi ya Premier enzi tunasoma sekondari ilikua ni viwango vya UMISETA,
 
Nimesikitishwa sana na kiwango kibovu cha soka kilichoonyeshwa na timu hizi kwenye game ya jana , ni aibu sana kwa timu hizi zinazosemekana zinafundishwa na makocha wa kigeni .

ili soka la Tanzania lipande hizi timu ni lazima zihujumiwe na zitokomezwe , ni mfano mbaya sana kwa vijana wanaochipukia ambao kila kukicha wanawaza kuchezea timu hizi mbovu , kwa tamaa ya vijihela vidogo sana wanavyolipwa

Timu yangu ya Simba ndio iliyonisikitisha zaiidi , ilishindwa kutumia pengo la red card ya Yanga kuongeza magoli , nadhani wachezaji wazee ndio tatizo , sasa kwa uchezaji ule ni kipi cha kujivunia kuwa na kocha eti wa kifaransa ? mbona hana tofauti na Jamhuri Kiwelu , Mziray , Katarsia Minziro au Sunday Kayuni ?

Wacha zako wewe
Ulitaka wachezeje
Yanga walishindwa mchezo Katikati,Mbele
lakini nawapongeza Beki walijitahidi sana
 
Usikute Una Miaka 20+
Ka mie
Hahahaa, mie nimeishi kipindi kile mtu unaingia uwanjani kwenda kumuona mchezaji fulani, watu waliokua wanaujua mpira na mpira unawajua, watu mafundi wa mpira na vipaji vya hali ya juu sana...hapana mimi sio 90+ hahahaha
 
Wacha zako wewe
Ulitaka wachezeje
Yanga walishindwa mchezo Katikati,Mbele
lakini nawapongeza Beki walijitahidi sana
kwa vizee vya simba hata mimi ningekuwa beki wa Yanga ningevidhibiti
 
Hahahaa, mie nimeishi kipindi kile mtu unaingia uwanjani kwenda kumuona mchezaji fulani, watu waliokua wanaujua mpira na mpira unawajua, watu mafundi wa mpira na vipaji vya hali ya juu sana...hapana mimi sio 90+ hahahaha

Mh! Yani nauzee wote huo unaweza kugusa Smartphone na ukaandika Vizuri
Unamacho bwana
 
Back
Top Bottom