Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
ILI KUINUA ELIMU NCHINI TUNAHITAJI KUWAJIBIKA
Ili kuweza kuinua ubora wa elimu tunapaswa kutambua kinaganaga maeneo yote ya uwajibikaji, kutambua wakati maeneo hayo yanapokuwa na tatizo, mahali panapokuwa na tatizo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Hii ndiyo maana ya uwajibikaji. Kukosekana kwa uwajibikaji ndicho chanzo cha mrundikano wa changamoto.
Ikumbukwe kila mmoja wetu anao wajibu katika kuinua kiwango cha ubora wa elimu. Hii inaanza na wananchi wenyewe wakisaidiwa na asasi za kiraia pamoja taasisi za utafiti ambazo huonesha masuala yaliyoachwa katika kuinua ubora na usawa kwenye elimu.
Uwajibikaji hapa ni mchakato unaolenga kuwasaidia watendaji kutekeleza majukumu yao na kufikia lengo. Uwajibikaji haumlengi mtendji mmoja tu ila wote wanaohusika. Suala la elimu bora ni jukumu la wote na siyo suala la kutafuta wa kumlaumu kwa sababu kila mmoja anawajibika.
Mifumo ya uwajibishaji inaweza ikawa na madhara mkubwa kama ikiandaliwa vibaya. Tafiti zinaonesha kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwa kigezo cha kuwajibisha kwa kuangalia matokeo ni kigezo bora.
Ukweli unaosikitisha katika elimu ni kwamba "ni rahisi sana kumlaumu mwingine kuliko kutatu changamoto". Suala la elimu bora ni jukumu la wote "collective responsibility".Watu hufanya vizuri kama wakiwajibishwa kutokana na mamuzi kuliko matokeo ambayo yanaweza kuwa juu ya uwezo wao. Mazingira wezeshi huwawezesha watendaji kutekeleza majukumu yao. Hakuna mkabala wa uwajibikaji unaweza kufanikiwa kama hakuna mazingira wezeshi. Mazingira wezeshi yanatawaliwa na:
1. Taarifa sahihi
2. Zana za kuwezesha kukamilisha shughuli
3. Uwezo wa watendaji kutekeleza wajibu wao.
4. Motisha au hamasa ya kutekeleza wajibu.
Watendaji wote hutegemeana Ili kufikia malengo ya pamoja ya elimu. Kufikia malengo ya elimu kunahitaji ushirikiano na mawasiliano. Imani ya wanajamii na michango yao hupata nafasi ikiwa watendaji wataweka mlengo yanayotekelezeka kulingana na raslimali zilizopo. Jakubowsk (2017) Katika utafiti wake alionesh mkanganyiko wanaoupata wananchi wa Mexico na Poland kutokana na kukosekana kwa ubora kwenye maeneo ya uwajibikaji jambo lilowafanya viongozi kulaumu wananchi.
Licha ya Serikali ya Mexico kuazimia kufanya ugatuaji na ukasimishaji wa madaraka ngazi za chini Ili kuipunguzia Serikali kuu mzigo mwaka 1999 bado azimio hili halijatimizwa katika ukamilifu wake (Jakubowsk, 2017).