ErastoMashauri
New Member
- May 25, 2024
- 1
- 1
Utangulizi: Ukifuatilia kwa umakini zaidi kuhusu Maendeleo ya Nchi nyingi zilizoendelea hapa Africa, America na hata Ulaya, Utagundua kabisa kuwa mambo mengi au vitu vingi ukiacha miundo mbinu iliyofanywa na serikali!, Vingi pia vya kuvutiaKama Hoteli kubwa, Shule, Viwanda Nk. vimefanywa na Wananchi kutokana kuwa na kipato kikubwa kwa Raia mmoja mmoja!
NINI KIFANYIKE: Serikali yetu inapaswa kupunguza kodi kwenye Viwanda Vyetu, Taasisi zote pamoja na kampuni kubwa zote zinazoendesha biashara nchini, kisha izielekeze kuongeza mishahara kwa Wafanyakazi wake, na ili liweze kutekelezeka hilo ihakikishe inalisimamia ipasavyo.
FAIDA: Hii itasaidia kuwapaisha kiuchumi ambao utawawezesha Nao kuanzisha biashara zingine Nyingi kutokana na kwamba kila mmoja ana Ndoto kimaendeleo yake ambayo Anatamani kuitimiza. Mfano kwenye Sekta ya Madini kuna watu wengi ambao wanalipwa mishahara mizuri inayowaridhisha, na kutokana na hilo wapo baadhi wamejenga hotel Kubwa Mijini ambayo serikali inanufaika na Kodi, wapo pia waliojenga Shule za binafsi(Private School) nk.
Lakini pia kwenye Sekta Ya Utalii, ni Sekta ambayo inaiingizia Serikali mapato ya kutosha, pia kule wapo wengi waliokuwa waajiriwa lakini kwa sasa nao wana kampuni zao za Utalii. Lakini pia hii itasaidia kutokomeza au kupunguza tatizo la Ajira lililopo nchini.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUTIMIZA HILO: Ili kuwezesha kutimiza hilo lisiweze kukwama, Serikali inapaswa kuanza kutoa Elimu ya Ulipaji Kodi kwa Wananchi kuanzia Watoto Waliopo shule Za Msingi, hii itawafanya watoto wakue wakijua umhimu wa kulipa Kodi, Kisha iweke njia zinazorahisisha Mtu yeyote mwenye nia ya kutaka kufungua Kampuni au Biashara, Anapata Vibali kwa haraka zaidi, tofauti na sasa ambapo kuna mzungu mkubwa sana ukilinganisha na nchi zingine nilizozitaja hapo Awali.
Pia itunge Sheria kali ambayo itazibana zile kampuni au Taasisi zitakazoenda kinyume na ulipaji mishahara mizuri sasa kwa wafanyakazi wake lisha ya kupunguziwa Kodi, bila kuathiri ukuaji au uendeshwaji wa kampuni hizo! Mfano kampuni iliyokaidi ipigwe faini ambayo italipa ndani ya miaka miwili au zaidi, na kisha iamuliwe moja kwa moja kuwalipa wafanyakazi wake.
Kisha Sheria hiyo pia itawabana Wote watakaoshindwa kulipa Kodi, Watalipa faini isiyokandamizi ambayo itasaidia kuzifanya bishara zao au kampuni zao ziendelee kuwepo.
HASARA ZINAZOWEZA KUTOKA KUTOKANA NA HILO: Zipo Hasara Ndogo zinazoweza kutokana na Utekelezaji wa jambo hilo, Na kama mjuavyo huwezi kupanda mlima bila kushuka Kwanza Mteremko, hivyo zitajitokeza hasara kadhaa kama Serikali kupungukiwa Mapato ya kuendesha miradi yake wakati ikitekeleza hilo, Lakini likitekelezwa ipasavyo linaweza kuleta Matunda Makubwa Baadae.
Erasto Mashauri✍

Upvote
1